Salamu – Agosti, 2010

Mmm! Nina kusalimu katika jina la Bwana wetu mwema Yesu Kristo, tunamskuru sana Mungu aliyetulinda na kutupa tena uzima mimi Steven na mke wangu Beth, Tunaamini Bwana amekupigania na kukulinda katika mwezi uliopita, nina amini umekutana na mambo mengi sana, mengine yamekufanya ufurahi na mengine yalikupa wakati ngumu sana, Tunakuombea kwa Bwana akuwezeshe katika kila Jambo,ulipokita katika magumu Mungu akufungulie mlango wa kutoka mwezi huu, Hizi ni salamu zetu kwako. Sikiliza neno la Bwana lisemavyo “Mwanangu, usisahau sheria yangu,bali moyo wako uzishike amri zangu, Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima,na amani, Rehema na kweli zisifarakane nawe; zifungue shingoni mwako; ziandike juu ya kibao cha moyo wako.Mtumaini Bwana kwa moyo wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyoosha mapito yako, Usiwe mwenye hekima machoni pako; mche Bwana,ukajiepushe na uovu” (Mithali 3:1-7)