Salamu – Juni, 2016

 JIFUNZE KUMTOLEA MUNGU KWAUSAHIHI

Tunawasalimu katika jina la Yesu Kristo aliye hai. Pole ya kazi zote mbalimbali. Mwezi watano tunatarajia kuwa na semina Sumbawanga, Na tutafunga hema na tukimaliza tutaelekea Tunduma baada ya Tunduma tutakwenda Vwawa.

Ni semina tatu mfululizo. Na tunamshukuru Mungu ambaye ametuweka tayari ili tumtumikie katika semina hizo tatu. Ebu turudi kwenye kona yetu ya salamu za mwezi kutoka kwetu. Naamini unabarikiwa na salamu hizi tunazokutumia kutoka kwangu mimi na mke wangu. Tunatamani kila tarehe moja ya mwezi tuwetumekuletea salamu hizi. Bahati mbaya tunamambo mengi sana tunachelewa kuwaletea salamu hizi. Tuombeeni ili tuyamudu haya.

Katika salamu zilizopita  tuliendelea kujifunza katika yale maswali ambayo watu wengi waliniuliza kuhusu zaka. Natamani tuendelee mbele tena. Tuliendelea kuona kuhusu zaka inatakiwa tuitoe wapi.  Ebu tuone eneo lingine ambalo zaka unaweza kuitoa angalia mistari hii. “tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na sadaka zetu za kuinuliwa, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu.Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.”(Nehemia 10:37-39).

Ukiipitia hiyo mistari utaona kuwa zaka, wakati wa Nehemia zaka  iliamuliwa kuletwa nyumbani mwa Mungu na kuiweka kwenye vyumba maalumu vya kutunzia sadaka zilizotolewa na Wana wa Israeli. Mfumo huo unatumiwa hata leo na madhehebu mbalimbali. Watu wanaleta zaka hapo na inakusanywa na hupelekwa mahali maalumu na wanaigawa  sawasawa na utaratibu waliojipangia.

Si dhambi kufanya hivyo. Ninachotaka kukufundisha ni kilekile FAHAMU ZAKA ZI MALI YA WAKUSANYAJI ZAKA VYUMBANI KATIKA NYUMBA YA MUNGU!!!!  Ukilijua hili itakua ni rahisi sana kumuuliza Mungu juu ya kupata muongozo wa kuitoa. Kama atakuelekeza uitoe hapi nyumbani mwa Mungu uitoe pasipo shaka. Au anaweza kukuongoza UKAMPE MOJA KWA MOJA MLAWI WAKO yaani mtumishi yule AMBAYE MUNGU AMEMUINUA KWA AJIKI YAKE ILI AKUJENGE WEWE NA UWE MKAMILIFU. Kumbuka sana hili.

Ninachotafuta hapa ni kukuonyesha  eneo lingine zaka inaweza kutolewa na watu. Unajua kunawatu ambao wanamfumo  wakutoa zaka zao kwa mtindo wa kuzikusanya toka kila pembe ambako wanawaumini. Na zaka hizo hugawanywa kutokana na utaratibu waliouchagua. Si dhambi, kwani hata kipindi cha Nehemia  walikua na mtindo huohuo.  Kuna uzuri wake na pia kuna hasara zake kwamtindo huo.  Unajua ni rahisi sana kuwagawia wastahilio na wasio stahilli.

Unaweza kujiuliza unamaana gani? Angalia mfano. Fikiria hiyo zaka ikigawanywa hapo kanisani je! Kuna ainangapi ya watumishi?  Je! Na wao wanapewa mgao huo? Nimewasikia watu wengi sana ambao ni viongozi wa kanisa wakisema mapato yamepungua kanisani na watu wanaishi maisha magumu kiuchumi na viongozi hao kila mara wanawahimiza watu kutoa zaka na watu wanatoa lakini  kila mara watu wanaona kama hakuna faida hivi.

Moja ya jambo la kujifunza ni hili ninalokuambia kuwa kuna watu ambao ni watumishi na wanahaki ya kupewa huo mgao hapo kwenye dhehebu lao lakini kutokana na mfumo uliopowa kutokuwatambua kuwa hao nao ni watumishi utaona  ni vigumu kupewa mgao wa zaka hizo na Mungu baadaye huizuia zaka yake isipelekwe huko.

Sikiliza Mungu anaouwezo wa kuwazuia watu kutoa zaka. Kumbuka zaka ni mali yake kama haija kaa sawasawa fahamu anao uwezo wa kuwazuia watoa zaka wasitoe zaka!!! Unaweza sema utajuaje kuwa amezuia? Wewe utaona utayari wa watu wa kuitoa hiyo zaka.

Mfano angalia maneno haya Mungu akigombana na makuhani wake ambao ndiyo waliyopewa jukumu la kusimamia  hata habari za sadaka jinsi walivyolidharau jambo hili la ugawaji wa hizo sadaka.   “Na sasa, enyi makuhani, amri hii yawahusu ninyi.Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu, asema BWANA wa majeshi, basi nitawapelekeeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.Angalieni, nitaikemea mbegu kwa ajili yenu, nami nitapaka nyuso zenu mavi, naam, mavi ya sadaka zenu; nanyi mtaondolewa pamoja nayoNanyi mtajua ya kuwa mimi nimewapelekeeni amri hii, ili agano langu liwe na Lawi, asema BWANA wa majeshi.Agano langu naye lilikuwa agano la uhai na amani; nami nikampa ili aogope, naye akaniogopa, akalicha jina langu.”(Malaki 2:1-5).

Mungu akiwataka kuwalaani makuhani wake ni kuwafanya watu kutokupata mazao au uchumi wao uyumbe ili wasitoe zaka na sadaka zingine. Ili kuwaondolea  hao makuhani nafasi ya kupewa kitu kutoka kwa Watu wa Mungu. Kumbuka makuhani walipewa nafasi ya kupewa hizo sadaka  mbalimbali. Sasa walipomkorofisha Mungu akaamua kuzuia watu kutokutoa sadaka kwa kuwaletea ukame. Msikie asemavyo.”Angalieni, nitaikemea mbegu kwa ajili yenu, nami nitapaka nyuso zenu mavi, naam, mavi ya sadaka zenu; ” mbegu ilikemewa kwa sababu ya makuhani kutokuheshimu  mfumo wa sadaka walizopokea.

Inaonekana wazi kuwa makuhani hawakuwagawia Walawi haki yao. Sasa sikia ikiwa leo hii kunawatumishi wengi sana ambao hawagawiwi haki yao ya kupewa hiyo zaka unafikiri kitatokea nini? Naamini Mungu atazuia watu wasiitoe hiyo zaka. Kwa hiyo kunauzuri wake kama utaratibu wa Paliouweka Mungu utafuatwa. Pia nirahisi watu kufanya utoaji wa kimapokeo. Unajua ningumu sana watu wa aina hiyo kutoa zaka mahali pengine hata kama Mungu alitaka wasitoe hapo. Watu wengi waliozoea kutoa kwa mfumo huo hawaoni kama wanaweza mpa zaka hiyo mojakwa moja  mchungaji wao au kiongozi au mtumishi mwingine.

Si wamezoea kutoa ili ikagawiwe huko ofisi kuu!!! Sasa watu wanamna hiyo ni rahisi sana kutoa kwa mazoea hata wakisemeshwa watoe sehemu nyingine na Roho Mtakatifu kwao inakua ni ngumu sana. Naamini umenielewa ebu tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.

Mungu akubariki sana.

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila

Salamu – Mei, 2016

Ninawasalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo. Bwana Yesu Kristo  asifiwe sana!!! Leo hii nimekuletea salamu kutoka kwetu. Mimi na familia yangu ni wazima tunamshukuru sana. Bila ya kupoteza muda naenda moja kwa moja kwenye salamu za mwezi huu wa tano.Kumbuka tunajifunza somo lenye kichwa.

JIFUNZE KUMTOLEA MUNGU KWA USAHIHI

Katika salamu zilizopita nilikuambia kuwa nitakuletea salamu maalumu nikijaribu kujibu maswali ya watu wengi waliyoniuliza kuhusu habari za zaka. Nilianza kwa kujibu swali lile la Zaka ni mali ya nani?. Nilikuambia zaka ni mali ya Mungu. Ebu tusogee mbele tujifunze kwa swali lingine.

Watu wengi wameniuliza je! Zaka inatakiwa itolewe wapi? Sikiliza. Kama umejua kuwa zaka ni mali ya nani, itakua ni rahisi kwako kujua kuwa unatakiwa umsikilize sana mwenye mali akikupa muongozo ni wapi hiyo zaka yake anataka uipeleke wapi. Na unaweza kuwa na swali ntapataje kujua muongozo wa wapi niitoe zaka. Hapo nijumlishe na sadaka zako zote..

Jambo la kwanza lazima umsikilize Mungu asemavyo au atufundishavyo kuhusu habari za kutoa zaka. Na tunaanza kumsikiliza Mungu au tunaanza kupata muongozo kwa kupitia Neno lake. Ebu tuangalie ni maeneo gani Maandiko yanasema zaka inaweza pelekwa.

Angalia misrari hii. “Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu.Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.”(Hesabu 18:25-28)

Ukiyaangalia maneno hayo utagundua hapo kuna maeneo mawili yametajwa zaka inaweza pelekwa. Eneo la kwanza ni zaka ya wana wa Israeli kupokelewa na Walawi. Na eneo la pili ni zaka kupokelewa na Kuhani Haruni. Ngoja niseme kidogo hapo. Walawi ni kabila teule lililokua limechaguliwa na Mungu katika kumtumikia Mungu. “Nami, tazama, nimewatwaa ndugu zenu Walawi miongoni mwa wana wa Israeli; kwenu ninyi watu hao ni kipawa alichopewa BWANA, waufanye utumishi wa hema ya kukutania.Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.”(Hesabu 18:6-7).

Katika agano la kale Walawi walichaguliwa kumtumikia Mungu. Hawakua na kazi nyingine zaidi ya hii ya kumtumikia Mungu. Mungu ili awatunze hao ndugu aliamua kuwapa zaka ambayo ni mali ya Mungu hao ndugu.  Kumbuka zaka ni mali ya Mungu. Sasa mwenye mali alifanya maamuzi ya kuwapa hao watumishi zaka.  Pia Mungu aliwaamuru hao Walawi na wao watoe zaka katika zaka yao waliyoipokea kutoka kwa wana wa Israeli.

Zaka hiyo waliambiwa waipeleke kwa kuhani. Kuhani naye alichaguliwa kumtumikia Mungu tu. na Mungu akampa nafasi ya kuzipokea zaka kutoka kwa Walawi. Angalia mistari hii.”Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe. Kisha BWANA akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.”(Hesabu 18:19-21).

Moja ya sadaka ya kuinuliwa waliyoamuliwa Walawi waitoe ni zaka katika zaka waliyoipokea kutoka kwa Wana wa Israeli. Angalia hapa anasema hivi. “Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA”

Ninapoisoma hiyo mistari naona  Maeneo mawili ambayo Mungu aliamuru zaka yake ipelekwe. Sasa kama Mungu alisema kipindi kile fahamu hata leo anaweza sema zaka yake ipelekwe huko.  Unajua katika agano jipya ndiyo kuna kitu kipana zaidi. Unajua unapozungumzi habari za Watumishi unaona Mungu aliishafanya mabadiliko makubwa yanamna alivyowapa watu nafasi ya kumtumikia.  Katika agano jipya utaona kuwa Mungu amewapa watu wa makabila yote na mataifa yote ili wamtumikie. Angalia mistari hii.”Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”(Ufunuo 5:9-10).

Ukiipitia hiyo mistari utaona kuwa Mungu alifanya maamuzi ya kutupatia nafasi ya utumishi kwa kutumia damu ya Bwana Yesu Kristo. Kila mtu wa jamaa yoyote wa kabila lolote na taifa lolote na wa lugha yoyote ilimladi amenunuliwa kwa damu ya Bwana Yesu Kristo amepewa nafasi ya kuwa mtumishi wa Mungu. Unajua kwasasa yaani agano jipya Mungu analundo kubwa la watumishi.  Na hajawaondolea nafasi ya kuipokea zaka.

Angalia mfano. Leo hii kuna watumishi wa idara zifuatazo. Wapo Wachungaji, Mitume, Wainjilisti, Manabii Waalimu. “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; “(Waefeso4.10-11)

Ukiwaangalia hao watumishi utaona wamewekwa kwenye idara tano tofauti kabisa. Ila cha kufurahisha zaidi ni hiki IDARA HIZO ZOTE ZIMEWEKWA KWA KUSUDI MOJA TU LA MUNGU NALO NI.”kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; “Unajua ni rahisi kuwaona watumishi hao wa tofauti za idara zao, ila usione wakifanyacho wote watano ni KIMOJA. Kila mmoja hutumika ili KUSUDI LA MUNGU LITENDEKE LA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU NA KUWAJENGA  kwenye maeneo ambayo Mungu anataka kanisa lake liwe.

Pia ukisoma maandiko utaona huko ndani kuna watumishi wa Mungu waitwao waombaji, waimbaji, viongozi, wote hao ni watumishi. Sasa unapotaka kumtolea Mungu zaka yake unatakiwa uwe makini sana.  Unajua bahati mbaya watu wengi hawaoni upana wa HUDUMA YA MUNGU ILIVYO HIVI SASA!!! Watu wengi hufikiri kuwa mtumishi wa Mungu ni mchungaji tu!!! Au ni mtume tu!! Au ni nabii tu. sikia hata mwinjilisti ni mtumishi wa Mungu na hata waalimu na hao waombaji na waimbaji nao ni watumishi wa Mungu. Kila mmoja humtumikia Mungu kwa utofauti kutokana na idara au vitengo walivyowekwa.

Watu wengi hawaamini kuwa kuna mtumishi anaye itwa mwalimu. Wengi humuona mwalimu kama mtumishi mdogo hivi, eheheee!! Wengi watoapo toleo kwa mwalimu au mwinjilisti huona kama hiyo si sadaka ni MSAADA HIVI!!!  Bahati mbaya sana watu wengi hufikiri zaka ni mali ya mchungaji wao tu. kwasababu hapo kanisani pao HAWAJUI KUWA KUNA MTU ANAITWA mwalimu ila si mchungaji, na bahati mbaya wengi hawaidhamini kazi ya mwinjilisti. Nimeona kuna wainjilisti wa aina mbili. Kuna walioamiliwa na madhehebu. Na kuna wainjilisti ambao hawaja ajiliwa kanisani. Lakini ni mwinjilisti. Anafanya kazi ya kuhubiri lakini si chini ya mwamvuli wa dhehebu.

Bahati mbaya watu wengi hawaioni au hawajui kuwa huyo naye ni mwinjilisti. Unajua wote tumeitwa kumtumikia Mungu ila kwa mifumo tofauti tofauti. Wapo walioajiliwa na wapo ambao hawaja ajiliwa mahali ila wamepewa jukumu la kumtumikia Mungu. Sasa unapolijua hilo ni rahisi sana kutoa zaka mahali pale Mungu amekuongoza utoe zakayake. Binafsi kwenye eneo hili namshukuru Mungu amenisaidia sana kulijua. Sitoi zaka kimapokeo. Natoa kwa kuongozwa sana nayeye.

Watu wengi hutoa zaka ila hawajui zaka ya Mungu waliyonayo waipeleke wapi. Wengi wanaitoa kimazoea. Fikiria kidogo, hivi mzee wa kanisa ni mtumishi wa Mungu au? Mwombaji je? Mwimbaji je? Yule mfagiaji kanisani je? Au mtunza mlango au bustani je? Hivi yule mfunga vyombo kanisani au yule mtunza choo cha kanisa? Tanua mawazo yako utaona nikwanini humuoni Mungu akikubariki.

Angalia mifano hii.”alikuwa amemtengenezea chumba kikubwa, hapo walipoweka zamani sadaka za unga, na ubani, na vyombo, na zaka za nafaka, na divai, na mafuta, walivyoamriwa kuwapa Walawi, na waimbaji, na mabawabu; tena sadaka za kuinuliwa zilizokuwa za makuhani.”(Nehemia 13:5). Ukiipitia hiyo mistari utaona wazi kuwa zaka walipewa waimbaji, walawi, mabawabu na makuhani. Unajua kazi ya kuhani ninini?  Ni mtu wakati afanyaye upatanisho kati ya watu na Mungu. Leo kila aliyenunuliwa kwa damu ya Bwana Yesu Kristo mepewa nafasi ya kuwa kuhani.

Fikiria leo hii wapo makuhani wangapi ambao usiku na mchana wanaifanya kazi hii ila SI MITUME WALA SI WACHUNGAJI? Unafikiri hao si watumishi? Nakuuliza hayo ili ukipata jibu utaelewa eneo hili la zaka unatakiwa uitoe wapi.  Ebu ni ishie hapo Mungu akipenda tutaonana tena  katika kona hii mwezi ujao. Barikiwa

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila

Salamu – Aprili, 2016

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ninamshukuru Mungu sana kwa kutupa uzima na nafasi ya kukuletea salamu za mwezi huu. Tunamshukuru Mungu sana kwa sababu ameendelea kututendea mema na kutupa nafasi ya kumtumikia.  Katika salamu zilizopita tulijifunza kuhusu aina ya sadaka ya Nadhiri au ahadi.

Na nilitaka katika  salamu za mwezi huu tuanze kujifunza kuhusu aina ya sadaka nyingine. Lakini kuna kitu moyoni mwangu ambacho nimekiona kutokana na maswali mengi ambayo tunaulizwa kuhusu ZAKA.

Watu wengi wamekuwa na maswali haya yafuatayo.

  1. Zaka ni mali ya nani hasa?
  2. Ni vitu gani ambavyo tunatakiwa tutoe zaka?
  3. Kuna aina ngapi za Zaka?
  4. Zaka inapaswa kutolewa wapi?
  5. Nani anatakiwa atoe zaka?
  6. Namna ya kuikomboa zaka kwa kutoa sehemu ya tano ya zaka.

Kutokana na aina hii ya maswali ambayo tunauliswa na watu wengi sana inawezekana hata wewe unamaswali kama hayo, nikaona ebu tuludi nyuma tujifunze kwa ufupi. Naamini Mungu atakupa kitu cha kukusaidia.

Hebu tuanze kuliangalia swali la kwanza  zaka ni mali ya nani hasa.? Ukiisoma Biblia utaona wazi kuwa zaka ni mali ya Mungu. Angalia mistari hii.”Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.Na kama mtu akitaka kukomboa cho chote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake.Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA.”( Mambo ya Walawi  27:30-32).

Ukiisoma mistari hiyo utagundua kuwa zaka ni mali ya Mungu mwenyewe.  Unaweza usinielewe kutokana na mapokeo yaliyojengeka mioyoni mwa watu wengi. Watu wengi wamefundishwa kuwa zaka ni mali ya watumishi, wachungaji, waalimu, mitume au wainjilisti au manabii. Na hata watumishi inawezekana ninapokufundisha neno hili haunielewi kwa kuwa umeamini kuwa zaka ni mali yako.

Zaka si mali ya mtu, au kanisa furani au faragha furani au kikundi furani. Zaka ni mali ya Mungu. Natamani ujue na uendelee kujua kuwa, Mungu  anapompa wapa nafasi watumishi waichukue zaka  HAINA MASNA KUWA ZAKA NI MALI YA HAO WALIOPEWA HIYO ZAKA WAICHUKUE. Watumishi wengi wanaona moyoni kuwa zaka ni mali yao. Huo ni utovu wa nidhamu sana. Na ni rahisi hata kutokumuheshimu Mungu  akupaye wewe ule hiyo zaka.

Watu wengi sana ndani ya mioyo yao wamefikiri zaka ni mali ya dhehebu lao. Mioyoni hawamuoni mwenye mali yaani Mungu huliona dhehebu lao kuwa ndiyo lenye haki ya kupewa zaka. Sikia, Mungu kukupa kibari cha kuitoa zaka dhehebuni kwenu basi zaka hiyo ni mali ya hilo dhehebu. (NATAKA UNIELEWE SINA MAANA USIITOE ZAKA HAPO KAMA UMEONGIZWA) ila nataka nikuondolee wazo la kuona kuwa zaka ni mali ya mtumishi au ni ya huko kanisani kwenu.

Natamani uwe na adabu wewe mtoaji zaka na kila mtu apokeaye zaka. Zaka si mali yenu, ni mali ya Mungu. Ngoja nikupe mfano huu. Angalia maneno haya.”Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli, akamwambia, BWANA asema hivi, Je! Mimi sikujidhihirisha nafsi yangu kwa nyumba ya baba yako, walipokuwa katika Misri, wakiitumikia nyumba ya Farao?

Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema?Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.”(1Samweli  227-30)

Ukiipitia hiyo mistari utaona kuwa, hao ndugu walimvunjia Mungu heshima kwasababu  alipowapa nafasi ya kupokea sadaka  yake wao hawakuoona kuwa hiyo sadaka ni mali ya Mungu aliyewapa wao. Angalia anasema. “Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu;” Unajua ni rahisi sana kuona toleo furani watu wakupalo mtumishi ni KAMA MALI YAKO HIVI. Kumbe Mungu ndiye mwenye hilo toleo ila kawaamuru watu wakuletee wewe.

Sasa kunakitu hakija kaa sawa, hata hao waletao hilo toleo pia hajui kuwa wameamuliwa na Mungu, wengi humwangalia apewaye hilo toleo badara ya kumuangalia mwenye toleo aliyewaamuru watoe. Ukija kwangu ukaniuliza au ukaniambia zaka ni mali ya nani mimi ntakujibu ni mali ya Mungu wala si mali ya mchungaji au ya kanisa furani.

Hebu angalia tena mfano huu. Siku moja Mungu aliwaambia watoto wake kuhusu habari za kumwibia. Alisema hivi. “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.”(Mwanzo 3:8).

Watu wengi huuona uwizi kwenye eneo la watu kutokutoa zaka tu, nataka leo hii uuone wizi mwingine hapo katika kona hii. Watu wengi WAIPOKEA ZAKA WANAFIKIRI NI MALI YAO NA HUWAAMBIA WATU KUWA HIYO ZAKA NI MALI YAO!!! Huo ni wizi wapendwa!!!!  Unajua ukilijua hili ninalo kuambia ni rahisi sana kumuheshimu Mungu akupaye hiyo zaka. Na pia ukiona watu hawajakuletea zaka hutababaika kwasababu utajua kuwa MWENYE MALI HUENDA KAWAELEKEZA WAIPEREKE SEHEMU NYINGINE AITAKAYO MWENYE MALI ZAKA HIYO IPELEKWE!!!!!

Naamini umenielewa . Hebu tufuatane tena katika kona hii mwezi ujao. Barikiwa sana.

Wako

Mr Steveni & Mrs Beth Mwakatwila.

Salamu – Machi, 2016

Nifuraha yetu leo hii tukiwakaribisha tena kwenye kona hii ya Salamu za mwezi. Mimi na familia yangu ni wazima kabisa. Naamini hata wewe ni mzima kabisa.

Hebu tusogee mbele kidogo kwenye salamu tulizonazo ambazo zimebeba somo lenye kichwa Jifunze kumtolea Mungu kwa usahihi. Kumbuka tunaangalia sehemu ya aina za sadaka. Na tunajifunza sadaka ya Nadhiri au Ahadi.

Sadaka hii ni sadaka inayotolewa kwa mdomo. Au ni sadaka ya kinywa. Ni sadaka ambayo mtu anamuahidi Mungu kuwa atampatia kitu furani. Mara ntingi sadaka hii huwekwa na watu wakitafuta kitu kwa Mungu na humuwekea Mungu ahadi kuwa iwapo atawatoa iwekwenye teso au kuwapa kitu furani wakitakacho, au hata kama Mungu amewaahidi kuwa atawapa kitu furani. Nawao kwa upendo humuwekea Mungu ahadi kuwa, atakapo wapa kitu furani walichomuahidi basi na wao watampatia Mungu kitu furani.

Katika kipindi kilichopita nilikuonyesha kwa sehemu tu sadaka hii. Leo nataka niingie ndani kidogo.  Ngoja nikupe mifano ya watu ambao walimuwekea Mungu nadhiri zao na waliziondoa hizo nadhiri.

Mfano wa Kwanza: Mfalme Daudi.”Nitaingia nyumbani mwako na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu;Ambazo midomo yangu ilizinena; Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni

Kafara za vinono nitakutolea, Pamoja na fukizo la kondoo waume, Nitatoa ng’ombe pamoja na mbuzi.Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.Nalimwita kwa kinywa changu, Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.” (Zaburi 66:13-17).

Ukiyaangalia maneno hayo unaona kuwa sadaka hii ni sadaka aitoayo mtu kwa kupitia kinywa chake. Mfalme Daudi alipokua shidani, alimuahidi Mungu vitu atakavyompa akimtoa kwenye taabu yake. Anasema “Nitaondoa kwako nadhiri zangu;Ambazo midomo yangu ilizinena; Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni”

Sadaka hii ni sadaka nzuri sana, ni sadaka pekee ambayo mtu anaamua yeye kumpa Mungu toleo la aina furani kwa hiari yake mwenyewe.  Si unajua sadaka karibu zote watu hutoa wakiwa wamepewa agizo la kuzitoa toka kwa Mungu. Sasa hii ya ahadi ni mtu yeye anaamua kuweka ahadi. Maandiko yanasema usipomuwekea ahadi wala si dhambi. “Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.”(Mhu 5:5)

Ukisoma pia kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Tolati, maneno ya Mungu yanasema hivi.”Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.”(Kum 23:21-23).

Sadaka hii mtu yeye ndiye anayeamua kumwekea Mungu nadhiri au asiweke. Ni sadaka pekee mwanadamu kwa hiyari yake anaamua kumpa Mungu kitu KWA NJIA YA AHADI. Fahamu ahadi hutolewa na mtu ambaye anatarajia kumpa mtu ahaidiwayo kitu furani huko mbeleni. Sasa wapo watu wengi sana humuahidi Mungu kumpa vitu.

Mfano wa Pili . Hana. “Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la BWANA. Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana.Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.”(1Samweli 1:9-11)

Ukiangalia maneno hayo utaona kuwa  mwanamke huyo alimuwekea Mungu ahadi ya kumtolea Mungu mtoto atakaye zaliwa kama Mungu atampa mtoto. Angalia si Mungu aliyemwamuru Hana atoe hiyo sadaka ya nadhiri ya mtoto. Ni Hana mwenyewe aliyeiweka hiyo nadhiri.

Watu wengi humuwekea Mungu nadhiri mbalimbali, hasa wanapokua taabuni, husema kwa vinywa vyao hata kama watu hawajasikia Mungu huwa anasikia. Lakini wengine wanapopewa vitu walivyovihitaji cha ajabu utaonahawaitoi hiyo nadhiri. Neno la Mungu linatufundisha kuwa kama tulimuwekea nadhiri lazima tujifunze kuweka bidii ya kuitoa.

Kumbuka somo letu ni kutoa kwa usahihi, watu wengi hapo hatujawa sahihi kabisa kwa Mungu kwenye eneo hili. Watu wengi huahidi kanisani, lakini hawatimizi ahadi zao. Wengi kwa vinywa vyao wanaahidi kutoa vitu furanifurani, lakini hawatoi kama walivyoahidi. Wengine ndiyo hawatoi kabisaa wanajifanya wamesahau hivi. Mungu hajaisahau ahadi uliyomuahidi kuwa utampatia.  Maandiko yanasema hivi. “Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.”(Kum 23:21-23).

Mungu anaisubiri ahadi ile uliyomuwekea, hajaisahau toa kwa usahihi kabisa. Yakobo alimuwekea Mungu ahadi  kule Betheli, alimuwekea ahadi ya kumjengea nyumba, kumpa zaka au sehemu ya kumi katika kila atakachompa, alimuahidi kuwa atamfanya Mungu kuwa Mungu wake. Unajua alipobarikiwa na akatulia tu huko kwa mjomba wake Labani, Mungu alimpelekea ujumbe kuwa ANATAKIWA AENDE KUITOA AHADI YAKE  HIYO ALIYOMUWEKEA MUNGU.

Angalia maneno haya uone. “Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani.Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.”Mwanzo 31:11-13).

Kumbuka Yakobo alimuambia Mungu kuwa kama akimludisha nyumbani salama basi atamfanya Mungu kuwa Mungu wake na atamjengea nyumba akalimiminia jiwe mafuta. Sasa Mungu ilibidi akamsitue, akamkumbusha kuwa sasa tayari nimeisha kupa mali. Ludi kayatimize yote uliyoahidi. Si unaona hapo anamkumbusha habara za nadhiri alizoweka Yakobo.

Swali langu kwako je! Umeziondoa nadhi zako ulizomuwekea Mungu? Ngoja niishie hapo tuonane tena mwezi ujao katika kona hii ya salamu za mwezi. Mungu akubariki sana.

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila