Bwana Yesu asifiwe sana.Mimi na familia yangu ni wazima kabisaa. Tumekuletea Salamu za mwezi wa nne. Karibu tujifunze

Kumbuka tuna salamu zenye kichwa.

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKAIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA AU KUOLEWA).

Mwezi huu ebu tusogee mbele kidogo. Tuangalia jambo hili.

UKIMPENDEZA BWANA UTAMWEPUKA MWANAMKE AU MWANAUME AMBAYE MUNGU HAKUKUPANGIA

Inawezekana sasa hivi umekuwa na swali na unafikiri moyoni mwako nifanye nini ili nipate kumwepuka mwanamke ambaye Mungu hakunipangia nimuoe au nifanyenini ili nipate kumwepuka mwanaume ambaye Mungu hakunipangia anioe. Ili leo hii upate kumwepuka mwanamke ambaye Mungu hakukupangia umuoe au mwanaume ambaye Mungu hakupanga uolewe naye unatakiwa uhakikishe unafanya jambo moja kubwa nalo ni hili, Umpendeze Mungu! Neno la Mungu linatupa maarifa kuwa ili upate kumuepuka mwanamke wa namna hiyo mwenye uwezo wa kukusaidia ni Mungu peke yake. Na ili Mungu akupe wewe msaada huo inatakiwa uhakikishe unampendeza yeye, Ebu sikiliza maneno ya Bwana yasemavyo “Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye” (MHUBIRI 7:26).

Ili leo hii upate kumwepuka mwanamke wa namna hiyo ni lazima uhakikishe unampendeza Mungu mpendwa. Kinyume cha hapo ni rahisi sana kunaswa na mwanamke wa namna hiyo. Maneno ya Mungu yanasema wazi kuwa yupo mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo umeziona sifa za huyo mwanamke? Sikiliza mwanamke wa namna hiyo Mungu hawezi kukupa umuoe kabisaa.Ndio maana amesema yeye ampendezaye Mungu atamponyoka mwanamke wa namna hiyo. Ikiwa ndugu yangu hutatulia na kutulia ndio kumpendeza Mungu nakuahakikishia utaoa mwanamke wa namna hiyo upende usipende!

Ndio maana nakuambia usijianzishie mapenzi mapema mpendwa kwa kuwaiga watu walio na ma“GIRL FRIEND” nakuambia ukweli ukiwa ni mtu wa namna hiyo utajikuta tu umenaswa na huyo mwanamke hata kama hutaki kumuoa utamuoa tu! Hata wewe dada ikiwa leo hii hutampendeza Mungu kwa kutulia kwako na kuyachochea mapenzi kabla ya wakati wake nakuambia ukweli utajikuta umeangukia kwa mwanaume ambaye utajuta sana baadaye. Ili umpate mwanamke au mwanaume atokaye katika moyo wa Mungu kweli ni lazima umpendeze Mungu, unaweza kujiuliza swali nitampendezaje Mungu? Sikia, ni kwa kufanya haya mambo mawili makubwa. Moja ni lazima umwamini na la pili ni lazima uyafanye mapenzi yake. Ukisoma maneno ya Mungu yanasema hivi “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao” (EBR 11:6).

Neno la Mungu linatufundisha kuwa ili leo hii mimi na wewe tupate kumpendeza Mungu ni lazima tuhakikishe tunamwamini. Neno imani maana yake ni hii “Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (EBR 11:1). Imani maana yake ni hiyo, yaani ni ule uhakika ulionao kuwa Mungu atakupa mwanamke au mwanaume mwema kabisa iwapo tu utamshirikisha kwa kumwendea kwa njia ya maombi. Uhakika huo ukiwa nao hiyo ndio imani, kama huna uhakika basi huna imani kabisaa! Ikiwa unaimani kwa Mungu kuwa atakupa mwanaume au mwanamke mwema basi huta fanya haraka wala huta babaika bali utatulia tuli! unajua ni kwanini unahangaika sana na una hofu sana katika suala la kuolewa kwako dada? Jibu ni rahisi sana, ni hili huna imani kwa Mungu wako. Neno la Mungu linasema aliye na imani hana hofu “Kwamaana andiko lanena kila amwaminiye hatatahayarika” (RUM10:11).

Ukimwamini Mungu utamsubiri. Ukimuomba Mungu akupe nakuambia ukweli atakupa katika majira yake. Kwa nini leo hii watu wengi wanajianzishia jambo hili ovyo-ovyo jibu ni kwa sababu hawamwamini Mungu. Wanawake wasio na imani wanaona kama wanaume ni wachache kuliko wanawake, basi wengi huingiwa na hofu, nakuanza kujitafutia wanaume wa kuwaoa kwa kujipendekeza kwa hao wanaume na kujirahisisha sana. Matokeo yake kweli wataolewa lakini cha moto watakiona huko mbeleni! Pia wanaume nao ni hivyohivyo kwa sababu hawana imani kwa Mungu kuwa atawapa wanawake wazuri kwa sababu ya wanawake ni wengi basi wanashindwa kutulia wanaanza kulukaluka na hao mabinti, mara leo huyu hooo! Kesho huyu matokeo yake ni kujikuta wakinaswa na wanamke ambao ni tanzi na kwa kweli ni kifungo kabisaa.

Ebu anza kumpendeza Mungu kwa kumuamini, kuwa atakupa aliye wako, pia tulia ondoa hivyo vinyago ulivyojiwekea moyoni mwako yaani picha za wanaume uliojiwekea moyoni au wanaume uliojiwekea moyoni. Wewe mwenyewe fikiria unawanaume watatu wote hao umewakubaria kukuoa, naunajidanganya kuwa utamchagua mmoja fikiriawote hao wakikung’ang’ania utafanya nini? Pia ondoa tabia hiyo ya kukata tamaa uliyonayo kwa kuwaza kuwa umechelewa, na unaona kama huwezi kuolewa na ukaanzisha juhudi yako binafsi ya kuolewa kwa kuanza kutafuta wanaume wakukuoa achana na tabia hiyo. Tulia mwamini Mungu kuwa atakupa aliye wako, ebu ondoa kuchoka kwako jipe moyo mkuu sasa mwendee Mungu atupaye haja zetu mwambie haja yako ya kuolewa, atakupa mumeo. Mungu anasikitika anapokuona dada aliyekuumba kwa mfano wake ukishindwa kumuamini katika jambo dogo kama hili na kuanza kutafuta wanaume wa wenzio na kuolewa mitala, mwamini Mungu atakupa mume hujachelewa ebu mwamini leo.

Jambo lingine unalotakiwa ulifanye ili upate kumpendeza Mungu na kwa kumpendeza huko Mungu atakupa mwanamke mwema na kukuokoa na mwanamke huyo mbaya ni hili. Lazima uhakikishe unayatenda mapenzi ya Mungu. Unaweza kujiuliza nini yaliyo mapenzi ya Mungu? watu wengi sana wanaijua sana sala kuu ya Bwana, ambayo ndani yake kuna ombi hili “mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni” kila siku unaisema sala hiyo lakini inawezekana kabisa huyajua hayo mapenzi ya Mungu unayo yaomba yatizwe hapa dunia kama huko mbinguni, ngoja nikuambie mojawapo ya mapenzi ya Mungu ambayo anataka yatimizwe hapa duniani, nayo ni haya “Hili nizuri nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli, kwa sababu Mungu ni mmoja na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1TIMOTHEO 2:3-5)

Fahamu ndugu yangu kuwa jambo zuri ambalo Mungu analitaka na amelikubali yaani ndilo analotaka litimizwe hapa duniani ni hili la kila mtu apate kuokolewa. Mungu hilo ndilo penzi lake na amelikubali mbinguni na anatakalitimizwe hapa duniani, sijui wewe ndugu yangu umeokolewa? Au je! Yesu amekupatanisha na Mungu? Fahamu ikiwa wewe hujapatana na Mungu kwa kupitia wokovu mkuu aliotenda Bwana Yesu pale msalabani na kuambia ukweli humpendezi Mungu! na itakuwa shida sana kumwepuka mwanamke au mwanaume aliye mtego na tanzi. Nafahamu ninacho kisema mpendwa. Unaweza leo hii ukafikiria jambo la kuokoka ni la dhehebu fulani au ni la watu wa umri fulani, vijana wengi shetani anawadanganya kuwa waokoke wakati tayari wameoa, nakumbuka mimi niliwahi wekwa kikao na mtu fulani ambaye alikuwa ni baba mwenye nyumba niliyopanga, yule baba aliambia kwanini nimeokoka wakati bado ni kijana ndogo? Pia aliniambia sasa ukiwaumeokoka leo unafikiri suala la kuoa utaoaje? Unajua aliniambia mambo mengi sana ya kunifanya nimuache Yesu ili nitafute mwanamke kwanza wa kumuoa ndio niokoke!

Sijui wewe unamawazo gani moyoni mwako? Na amini inawezekana unamawazo kuwa ukiokoka sasa ndio jamaa huyo unayefikiria atakuoa ndio hata kuoa tena. Unasubiri akuoe kwanza ndio uokoke. Ikiwa unamawazo hayo nakuambia ukweli unakuwa umekosea sana. Kwani huwezi kumponyoka huyo mwanamume jeuri mpaka umpendeze kwanza Mungu. Yaani ni lazima uamue kumpa Yesu maisha yako ndio atakupatia mwanaume mwema au mwanamke mwema. Nakuambia ukweli ndugu yangu nakumbuka mimi kabla sijampa Yesu maisha yangu nilikuwa na mawazo ya kuwaoa mabinti fulani. Unajua nilikuwa nafikiri kuwa mabinti hao nawapenda, na nilikuwa na mfikria mmoja na mwingine. Ila namshukuru sana Mungu aliniokoa na tendo la uzinzi, sikuwahi kufanya nao zinaa. Ngoja nikuambie, sikuwahi kufanya nao uzinzi, nilijua habari za tendo la ndoa ni baada ya kuoa. Kwa hilo namshukuru sana Mungu aliniwezesha kulikimbia. Nakumbuka vijana wenzangu walikuwa wananicheka pale ninapo babaika niwaonapo wasichana wazuri wakijileta sana kwangu, unajua walikuwa wananiambia Steven mbona unawakawiza! Usiwe mshamba wewe.

Ngoja nikuchekeshe kidogo, nakumbuka siku moja nilimchukua binti fulani alikuwa anakila sifa za uzuri wa sura mpaka umbo. Rafiki yangu mmoja alinipa chumba chake nikitumie kwa kukutana na huyo dada. Nikakaa naye chumbani, nikamtoa nguo zote akawa uchi kabisa. Nilipotaka kulala naye nilipata hofu ya ajabu sana, nikamwambia nakuja, nikaenda chooni nikakaa huko nikifikiria kuwa nifanye naye uziznzi au nimuache? Unajua nilipotoka chooni nikamwambia avae nguo tuondoke. Alikataa kabisa na alikuwa ni mwanafunzi wa sekondali. Ilitakiwa aludi shuleni kwao nikamwambia basi mimi naondoka naenda kufunga duka langu jioni imefika, nikamuacha pale kitandani mimi nikaondoka, kesho yake aliniandikia barua ndefu sana ya kunilaumu eti aliona mimi nimemdharau sana. Unajua mimi pia nilijilaumu sana kwa kumuacha! Kipindi kile nilifiiria hao wasichana ni na wapenda na nilimwambia ntakuoa ngoja kwanza nitafute pesa unajua siku ninaokoka siku ileile Mungu alinibadilisha kabisa. Unajua ndipo nilipoona hatari sana kwa huyo msichana na hata hao wengine.

Ndipo ufahamu uliponijia kuwa hao wasichana hawakunifaa kabisa katika suala la kuwaoa. Hakuwepo hata mmoja aliyonekana moyoni mwangu anafaa, unajua ni kwanini ilinitokea hivyo? Ni kwa sababu Bwana aliniwezesha kuwaponyoka, asifiwe Bwana kwa kuniokoa! Ngoja nizungumze na wewe kijana mwenzangu hao wasichana unaowaona wewe kuwa wanafaa uwaoe ni hatari hao kuliko akili zako zinavyowaza. Leo hii huwezi ona siku utakapompa Yesu Maisha yako ndipo akili zako zinapowekwa sawa na kuanza kuona hatari ambazo wewe sasa hivi huwezi ona.

Hata kwako dada, siku ukimpa Yesu maisha yako tu, ndipo nuru au wokovu wa kukuokoa na hao kina kaka waongo na wazinzi wanao jua sana kudanganya kwa maneno matamu ya kusema silali usingizi nakuwaza wewe dear! , umewahi kujiuliza kama hawalali na hawali chakula mbona hawakondi na kufa? Bila Yesu kuwa ndani yako nakuambia ukweli utanaswa nao tu. Siku hizi mabinti wengi ndio wamekuwa mitengo kwelikweli. Wewe waangalie kutembea kwao na hata kuvaa kwao, unafikiria ni nani anayetegwa hapo kamasio wewe ndugu? Nakumbuka siku moja nilikuwa nyumbani kwangu nikisikiliza redio nikakutana na tangazo moja linahusu habari ya sherehe ya kumaliza kidato cha sita. Waliweka tangazo lao katika redio moj katika mji ninao ishi, walikuwa wanawahamasisha walengwa wote waende kwenye ukumbi kwa wingi na waliwaambia kuwa kutakuwa na disko kabambe. Unajua yule dada mtangazaji aliwataka mabinti wote wanaokwenda kwenye hilo disko wahakikishe wanamavaa yeye alisema vijivazi! ambavyo yeye aliviita vijivazi vya “mtego-mtego”. Baada ya hilo tangazo nikajiuliza maswali mengi sana siku hiyo, nipata majibu na nikawaza mengi nikajiuliza hivi vijana wengi watapona kweli?

Ikiwa kwa makusudi kabisa mabinti wameamua kuvaa kimtego mtego, Je! Hapo vijana watafanikiwa kumuepuka huyo mwanamke ambaye Mungu anasema wazi kuwa mikono yake ni vifungo na moyo wake ni mtego na tanzi? Sikiliza huwezi kumponyoka ikiwa Yesu hayumo ndani yako. Kwanini nasema hivyo? Ni kwasababu Yesu akiwa ndani yako hutaenda naye disko kwenye vijivazi vya mitego mitego. Unajua kama kweli umeamua kumpa Yesu maisha yako nakuambia ukweli Mungu ni mwema atakupa hekima itokayo juu. Inayojua usemenini na ukae wapi kwa na kwa wakati gani. Utajua ni wapi kunahatari na wapi kuna usalama, utajua ni binti gani anajileta leta au ni mwanaume gani anajigonga gonga kwako na utajua tu kuwa huyu nia yake ni kunidanganya tu au huyu anataka fedha zangu wala hanipendi kabisaa. Utajua namna ya kukaa na kila mtu wa jinsia tofauti na wewe, utajua hata namna ya kumsaidia ili usimchomekee kinyago moyoni mwake nk.

Na amini katika Sehemu hiyo umenielewa mpendwa, ikiwa Yesu hayumo moyoni mwako yaani hujaokoka bado nakupa nafasi hii mpe Yesu maisha yako leo kwa faida yako na faida ya Mungu pia. Kwani Mungu hataki upotee, ikiwa unataka kumpa Yesu maisha yako ebu sema sala hii. “Sema Bwana Yesu, nakuomba unisamhe dhambi zangu zote, futa jina langu kwenye kitabu cha mauti, andika jina langu kwenye kitabu cha uzima, naomba leo ingia ndani yangu, nakukabidhi maisha yangu yote, uyatawale kabisa, na uniokoe na kila jambo baya siku zote za maisha yangu, unikumbuuke siku utakayokuja, nisaidie ee Bwana, asante Mungu kwa kunisikia naomba yote haya kwa jina la Yesu Kristo Ameni” Ikiwa umeisema sala hii toka moyoni mwako amini Yesu ameingia ndani yako sasa, yumo ndani yako, na atayabadilisha maisha yako kabisa mtii kwa kufuata maagizo yake yote yaliyomo ndani ya neno lake, anza kusoma Biblia na kuomba kila siku, pia nenda kanisani, usisite kuwaambia wenzeko au ndugu na jamaa kuwa umeokoka leo.

Ebu achana na huyo mwanaume au huyo binti ambaye ulijenga uhusiano mbaya naye, usiludie tena kutenda dhambi naye, ebu mwambie wazi kuwa humuhitaji tena kwa uhusiano ule wa mwanzo anza upya kuishi maisha matakatifu pia mwombe Mungu kila siku akuokoe na mwanaume au mwanamke aliye mtego yaani asiye mwema. Na amini ukifanya hivyo Mungu atakupa siku moja mke mwema na mume mwema.

Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila