Nina wasalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo. Ninamshukuru Mungu ambaye anatutunza na kutupa uzima kila siku. Ninaamini hata wewe Mungu kakupatia uzima na kukutunza. Tumekua na semina nyingi mwezi uliopita wa nne.

Kwakweli tumemuona Mungu akiwafungua watu wengi na kuwafundisha. Mwezi huu tunaendelea na mfululizo wa salamu zetu zilizobebwa na  kichwa

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKAIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA AU KUOLEWA).

Ebu tusonge  mbele tuangalie jambo lingine muhimu sana nalo ni hili usiogope mkeo au mumeo yupo!

MUMEO AU MKEO YUPO USIOGOPE

Jambo lingine kubwa sana muhimu unalotakiwa ndugu yangu ulifahamu ni hili,fahamu kabisa mkeo au mumeo yupo, kina chotakiwa utulie tu, wala jambo hili lisikupe hofu kabisaa, ikiwa ndani yako una wito wa kuoa au kuolewa, fahamu mkeo au mumeo yupo, nasema kuwa ikiwa ndani mwako kama kuna wito wa kuoa au kuolewa ni kwa sababu kuoa au kuolewa ni wito.Wapo watu ambao hawana wito huo au niseme hawana upako huo wa kuoa au kuolewa kabisaa! Siku moja Bwana Yesu aliwaambia Wanafunzi wake kuhusu jambo hili,alisema hivi “Maana wako matowashi waliozaliwa hali hivyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi;tena wako matowashi waliojifanya  kuwa matowashi kwa ajiri ya ufalme wa mbinguni.awezaye kulipokea neno hili,na alipokee” {MATHAYO 19:12}

Ukiyasoma maneno hayo utagundua kuwa wapo watu ambao Mungu hajawapa upako wa kuoa tokea matumboni mwa mama zao. Watu hao wanaitwa matowashi, neno towashi kwa maana nyingine anaitwa “hasai”, mtu huyo hana wito wa kuoa au wa kuwa na watoto na amini umenielewa hapo!  Kuna tonatofuti ya neno hasai na tasa.  Hasai hana uwezo wowote wa nguvu za kiume au za kike. Mtu anaweza kuwa tasa lakini akawana nguvu za kuime kabisa. Pia wapo wanawake ambao ndani yao hawana wito wa kuolewa kabisaa! Bwana Yesu anasema wapo watu waliofanywa na Mungu kuwa na hali kama hiyo, pia wapo watu walifanywa na watu kuwa katika hali hii, pia wapo watu waliojifanya kuwa katika hali hii.

Wapo watu leo hii ambao hawapendi mtu fulani aoe au aolewe,na kwa kutumia nguvu za giza watu hao wanawafanya watu hao wasioe au wasiolewe kabisa, pia shetani anawafanya watu wengine wawe watu namna hiyo,yaani anawafanya watu hao kuwa watumwa wa mapepo ya uzinzi kwa kufanywa wake wa mapepo au kuwa waume wa mapepo hayo, nimewahi kutana na watu wa namna hiyo wengi sana,na nikawaombea wengi walifunguliwa, unajua watu wa namna hiyo wanazuiwa na mapepo hayo kuoa au kuolewa, na ikitokea tu mwanaume akataka kumchumbia binti wa namna hiyo,ikiwa kijana huyo hajawa na Yesu ni rahisi sana moja kujikuta mipango yao kuvulugika, au kijana huyo kufa, pia kwa mabinti ndio hivyo hivyo,wakitaka kuolewa na mwanaume aliyeolewa na pepo wa mahaba, ni rahisi sana kumkuta mambo kama hayo. Ikiwa hata wewe ndugu msomaji wa kitabu hiki unamatatizo ya kujikuta unazini na mapepo,unatakiwa umpe Yesu maisha yako kwani yeye pekee ndiye msaada, pia unatakiwa uombewe ili upate kuondolewa ushirika wako na hiyo roho mbaya.

Sasa ikiwa wewe ndani yako una wito huo fahamu mkeo au mumeo yupo.  Usihofu kabisa, neno la Mungu linatufundisha wazi kuwa,Mungu alipokuwa ana muumba mtu kwa mfano wake aliwaumba siku moja mwanamke na mwanaume, neno la Bwana linasema hivi “ Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu;wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani,na wanyama na nchi yote pia,na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia Mungu akawaambia,zaeni  mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha;……” {MWANZO 1:26-28}, Ukiyasoma maneno hayo ya Bwana utagundua jambo ninalo kuambia kuwa, siku Mungu alipokuwa anamuumba mtu kwa mfano wake, alimuumba siku moja mwanaume na mwanamke, fahamu kwa mfano wa Mungu, Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke siku moja wala hawakuumbwa kwa siku tofauti tofauti, unaweza kujiuliza mbona Adamu ndiye aliyetangulia? Adamu alitangulia kuja duniani kaba ya mkewe Hawa katika mwili huu wa damu na nyama. Lakini kwa mfano wa mwili wa Mungu waliumbwa  wote wa wili kwa wakati mmoja, neno la Mungu linasema kuwa Mungu ni Roho “ Mungu ni Roho….” {YOHANA 4:24}

Ikiwa Mungu ni Roho basi hao ndugu pia waliumbwa kwa mfano wa Mungu ambao ni roho, na Mungu ana kaa mbinguni, siku ile alipokuwa anaziumba hizo roho mbili kwa mfano wake yaani mwanaume na mwanamke alikuwa katika ulimwengu wa roho au mbinguni anakokaa. Siku ile Mungu alipokuwa anawaumba hao watu aliwapa siku ileile agizo la kuzaana, yaani kwa maana nzuri siku ile aliwafungisha ndoa hukohuko mbinguni. Tena neno la Mungu linatufundisha kuwa hao ndugu walikuwa wa moja kweli hata jina lao lilikuwa moja, wote waliitwa Adamu  sikiliza maneno haya ya Bwana Ysemavyo“ Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu.Siku ile Mungu alipoumba mtu kwa sura ya Mungu alimfanya;mwanaume na mwanamke aliwaumba,akawabarikia akawaita jina lao Adamu,siku ile walipoumbwa.” {MWANZO 5:1-2}

Umeyasikia maneno hayo ya Bwana jinsi ya semavyo? Ukiyaelewa maneno hayo utagundua kuwa kumbe kila mwanamume aliyepo duniani anaye mke wake tayari hata kabla hajazaliwa katika tumbo la mama yake, watu wengi sana hawajui kuwa kabla hajazaliwa na kuanza kuishi hapa duniani walikuwepo sehemu fulani, nayo ni mbinguni, ebu yasikilize maneno haya ya Bwana yasemavyo “Neno la Bwana lilinijia kusema, kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,kabla hujatoka tumboni,nalikutakasa;nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” { YEREMIA 1:4-5} Umeyasikia maneno hayo ya Bwana yasemavyo mpendwa? Mungu alimjua Yeremia kabla hajaumbwa katika tumbo la mama yake, unafikiria alimjulia wapi? Alimjulia katika ulimwengu wa roho, yaani mbinguni ana kokaa Mungu, Kila mtu alitoka huko na ataludi huko neno la Mungu linasema hivi “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” { MUHUBIRI 12:7}

Kila roho ya mwanadamu lazima ijue kuwa ilikuweko kwa Mungu na italudi siku moja kwa huyo Mungu aliyeiumba, na roho ina ludi kwa Mungu baada ya mwili kufa, sasa kumbe hata wewe ulikuwepo huko mbinguni na siku ulipokuwa unaumbwa haukuumbwa peke yako, kama wewe ni mwanaume fahamu ulipokuwa unaumbwa siku ile ile unaumbwa kwa mfano wa Mungu uliumbwa na mkeo!  Pia hata wewe dada fahamu kuwa siku ile ile ulipokuwa unaumbwa kwa mfano wa Mungu au roho, uliumbwa pamoja na mumeo siku ileile. Na Mungu akawabarikia pamoja na kuwapa maagizo mengi tu, kama Yeremia aliumbwa kwa kusudi la kuwa Nabii wa mataifa kabla mimba haijatungwa katika tumbo la mama yake,  fahamu hata wewe na huyo mwanaume au mwanamke Mungu aliwaumba kwa kusudi maalumu kabisa, na aliwaleta hapa duniani kwa kusudi hilo. Ndio maana na kuambia suala la ndoa si la kukulupuka na kujiolea kila mwanamke unayemtaka wewe, umewahi kujiuliza kwa nini Mungu anakukataza usizini?

Ebu fikiri kuwa kumbe kila mtu aliyepo hapa duniani  Mungu alimuumba siku moja na mkewe au na mumewe, sasa ikiwa utafanya naye tendo la ndoa mwanamke yeyeote yule bila utalatibu alio uweka Mungu, fahamu unakuwa unamualibia mwenzio mke wake! Ngoja nikuulize swali,je! utajisikiaje siku unapoambiwa Haloo,mkeo leo kazini na fulani? Ikiwa utajisikia vibaya utakapo sikia mumeo kazini na fulani, basi hata wewe unatakiwa uhakikishe haufanyi tendo la ndoa na mwanamke yeyote yule. Inakupbidi umsubilie Mungu akupe wa kwako. Leo nataka  umwone kila dada au binti awe mkubwa au mdogo kuwa ni mke wa mtu! Pia mwone kila mwanaume awe mdogo au mkubwa  kuwa ni mume wa mtu. Umeelewa hapo?

Ndio maana na kuambi unatakiwa utulie sana usije ukavamia waume za watu au wake za watu kisa eti mnasoma naye, sikia huyo ni mke au mume wa mtu katika ulimwengu wa roho.  Sasa ili Mungu akupe yule aliye wako ambaye muli umbwa siku moja, ambaye atakuwa ni nyama katika nyama yako na mfupa katika mfupa wako,  Unatakiwa usijikurupukia tu na kutamani umenielewa mpendwa? usiwe na hofu yupo aliyewako,  hakikisha hauchokozi wakina kaka kwa kutaka mapenzi fahamu huyo siyo mumeo ni mume wa mtu ingawa hajaoa au hajaolewa tulia mwombe Mungu siku ikifika ya wewe kupewa wako atakupa usiwachezee wake za wenzio au waume wa wenzio umenisikia!

Mungu hapendi kabisa tabia hiyo ya uzinzi moja ya sababu ni hii ya kuwa halibia wenzio wake zao au waume zao, achana na tabia hiyo tubu Mungu atakusamehe tulia, subiri yuko wako mlioitwa kwa jina moja mimi naitwa Steven, Mungu pia alimwita mke wangu jina hilo hilo la Steven! Wewe unaitwa nani? Basi hata huyo wako anaitwa jina hilohilo, subiri,usije ukajichukulia ambaye si wajina lako! Utapata shida sana maishani mwako.  .

Ebu tuishie hapo. Fuatana nasi katika salamu za mwezi ujao. Mungu akubariki sana.

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila