Bwana Yesu asifiwe sana sana!! Mimi na familia yangu ni wazima, tunawashukuru kwa Maombi yenu Mungu ametupa kuuona tena mwezi huu wa saba.
Mwezi uliopita tulikua na semina Vwawa, tukafanya semina Itili Moravian, tukafanya semina Uyole katika kanisa la Anglican, na tukawa na semina Arusha ya watumishi maaskofu na Wachungaji kutoka sehemu Mbalimbali nchini wa Madhehebu tofauti tofauti. Ilikua semina nzuri sana.  Tulimuona Mungu sana mwezi uliopita akiujenga ufalme wake. Usiache kutuombea.
Nikukaribishe tena katika salamu zetu za mwezi huu wa saba.
Nilikuahidi kuwa katika salamu za mwezi huu ntakuonyesha jambo lingine linaloweza kuwa chanzo cha kukuzuilia au kuwa mwiba kwako katika eneo la kuoa kwako au kuolewa kwako nikakuambia kiini hicho kinaweza kuwa laana. Ebu tujifunze hapo. Ni eneo muhimu sana lifuatilie kwa umakini na ulichukulie kwa taadhari kubwa mno.
Kikwazo kingine ni hiki ni kutokuwaheshimu wazazi wako tu. Sikiliza
WAHESHIMU WAZAZI WAKO ILI UPATE HERI KATIKA JAMBO HILI LA KUOA AU KUOLEWA
Jambo lingine muhimu ambalo unatakiwa ulifanye kabla ya kuoa au kuolewa kwako, ni hili la kuwaheshimu wazazi wako watu wengi wamekwama katika habari hii ya kuolewa kwao na kuoa kwako kisa ni hiki hawana heri. Hata ukiangalia leo hii ndoa nyingi sana zimekosa heri au baraka sababu mojawapo ili sababisha mabaya hayo ni hii ya kutokuwaheshimu wazazi kabla ya kuoa au kuolewa. Neno la Mungu linatupa agizo kuwa kama tunataka tuishi maisha marefu na tupate heri au baraka basi tunatakiwa tuwaheshimu sana wazazi wetu na kuwatii, kumbuka kinyume cha baraka ni laana.
Mungu ametupa agizo anasema “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” (WAEFESO 6:1-3) Neno la Mungu linatufundisha hapo kuwa ili leo hii upate heri au mafanikio na kama unataka uishi maisha marefu hapa duniani, basi ni lazima uhakikishe unawaheshimu na kuwatii baba na mama yako.
Ukizingalia ndoa nyingi sana leo hii zimekosa heri, ni ndoa zenye mafarakano sana, wanandoa wengi wanaishi kwa kugombana hawaheshimiani tena ingawa ni wakristo wengi wameachana kabisaa. Na kuna ndoa zingine hazina baraka ya kupata mali hata watoto, kisa ni hiki hiki cha kutowaheshimu wazazi wao kabla ya kuoa au kuolewa. Sikiliza iiwa leo hii wazazi wako umewapelekea hoja ya kuwa unataka kuolewa au kumuoa binti Fulani na wazazi wako wakakupinga, hapo unatakiwa uwe makini sana tena sana! Ukikosea tu fahamu mambo mawili haya yanaweza kukupata. Jambo la kwanza unaweza kufa mapema wewe au huyo mwenzio, ama mtakosa heri au amani katika ndoa yenu. Ndoa yenu inaweza kuwa na machafuko kila siku.
Vijana wengi sana wanapoonywa na wazazi wao juu ya mienendo yao ya kimahusiano na watu wajinsia tofauti huwa wanachukia sana, wengi huwavunjia heshima wazazi wao kwa kusema au hata kwa kutowatii. Matokeo yake wanajikuta wameangukia katika laana inayowapelekea kufa mapema au kukosa baraka maishani mwao.
Siku moja kuna kijana mmoja niliyekuwa namfahamu alifariki, nilikwenda mazishini nilipofika kule makaburini niligundua jambo ambalo lilinisikitisha sana, niliona makaburi mengi sana ni ya vijana, makaburi ya wazee niliyaona machache. Unaweza ukajiuliza swali uligunduaje Steven? Nilisoma vibao vinavyo onyesha miaka waliozaliwa hao ndugu na siku na mwaka waliofariki!
Hapo ndipo nilipogundua kuwa vijana wengi ndio wanaokufa sana kuliko wazee wetu. Unajua nili jiuliza sana ni kwanini? Jibu ni lilipata katika hiyo mistari ya Waefeso sura ya sita. Neno limesema wazi tena maneno hayo hata vijana wa agano la kale waliambiwa hivyo-hivyo na Mungu ebu sikiliza alivyowaagiza “Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako alivyo kuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako” (KUM 5:16)
Mungu aliwaamuru vijana wote wa agano la kale hata sisi wa agano jipya katuagiza pia kuwa kama tunataka mafanikio katika maisha yetu na kama tunataka tuishi maisha marefu basi ni lazima tuhakikishe tunawaheshimu sana wazazi wetu, haijarishi wana elimu kiasi gani au wana fedha kiasi gani ama wanaishi mjini au vijijini hilo halijarishi kinachotakiwa ni kuwaheshimu tu. Vijana wengi siku hizi shetani kawafunga fikira zao hawana ufahamu wala kumbukumbu ya maneno haya. Wengi hawawaheshimu wazazi wao, nisikilize Kijana na wewe binti, ikiwa wewe umeokoka baba yako au mama yako hawajaokoka unatakiwa uwaheshimu.
Mungu hajasema kuwa eti kwa sababu hawajaokoka basi husiwaheshimu, neno linasema waheshmu baba yako na mama yako katika Bwana. Mungu hakuwa ana maana kuwa baba yako au mama yako akitaka ufanye jambo ambalo lipo kinyume na maagizo ya Bwana basi uwatii kwa kulifanya hilo jambo. Sikiliza unatakiwa hapo usiwe mjinga, ila uwe mjaja kama nyoka mpole kama hua. Usikurpuke na kuanza kuongea nao jambo lolote bila adabu au hekima itokayo juu.
Zungumza nao kwa hekima sana. Kama umeokoka Roho Mtakatifu yuko ndani yako, anayo maneno mazuri sana ambayo ukitulia na kumsikiza atakupa wakati huo na utawajibu wazazi wako nao watakuelewa tu. Tatizo liko kwako unakuwa na jaziba na haujawa mtulivu ndio maana huelewani na wazi wako. ikiwa leo hii Mungu Kakuambia kuwa utaoa au utaolewa na Fulani na moyo wako umependa, na umewaendea wazazi wako nao wakamkataa kwa sababu zao wenyewe wala si za Mungu. Hapo unatakiwa uwe na hekima sana ya namna ya kuchukuliana nao na hata kutenda kwako. Usikurupuke tu kwa kuwaambia, BWANA ASEMA.
Sikiliza Bwana kasema na wewe wao hawajui kuwa kasema na wewe, unatakiwa uwe na busara sana wakati huo yaani utulie. Ludi kwa Mungu aliyesema na wewe mwombe sana aseme na hao wazazi wako mwamini Mungu. Mungu si mkolofi atasema nao kwa namna ya kipekee sana, na wata kukubaria tu kama jambo hilo limetoka kwake.
 Kinacho wasumbua vijana wengi na mabinti wengi ni hiki cha kutotulia wanapokataliwa na wazazi wao kuoa au kuolewa na wale wanaowapenda, sikiliza neno la Mungu linavyo sema “……Yeye aaminiye hatafanya haraka.” (Isaya 28:16B) Neno la Bwana linatufundisha kuwa mtu yeyeote yule anayeamini hafanyi haraka, kama Mungu kakupa huyo mwanaume au huyo mwanamke ili muishi pamoja kama mke na mume, na wazazi wenu wanawakatalia au kanisani nk, basi tulieni, si mnaamini kuwa Bwana ndiye mwanzilishi wa jambo hilo? Sasa mnaharaka ya nini tena.
Yeye atalimaliza jambo hilo kwa kuwa yeye ndiye mwanzilishi wake, vijana wengi hukurupuka na kuanza kukolofishana na wazazi wao na wazi kwa kukasirika wanaanza kusema maneno magumu sana ambayo yamebeba laana. Hata kama umeokoka na ni mtumishi wa Mungu mabaya hayo yatakukuta tu. vijana wengi wakikataliwa na wazazi wao kuoa au kuolewa wengi pasipo kuongozwa na Mungu wanakimbilia kwa ndugu jamaa na marafiki na hata kwa wachungaji kutafuta msaada ili waolewe au waoe, unajua hapo ndipo matatizo yanapoongezeka sana, kweli inawezekana hao ndugu zako na huyo mchungaji wako watatumia nguvu na hata mtaoana na huyo baba yako na mama yako watakuja hata arusini nk. Lakini kama walilazimishwa na watu wala si kulazimishwa na Mungu, nakuambia ukweli chamoto utakutana ncho tu huko mbeleni. Unielewe sana hapo
Wewe fuatilia leo chunguza utagundua hiki ninacho kuambia, umewahi kujiuliza swali ni kwanini vijana wengi wanaoa leo wanapata mtoto mmoja lakini hawakai siku nyingi mmoja wa hao wanandoa anakufa? Na watu wanasema amekufa mapema kweli sijui nani atakaye watunza hao watoto?
Unajua ukienda kwa Mungu atakuambia hili ninalokuonya leo kuwa hawaku waheshimu wazazi wao walipotaka kuoana. Uwe mwangalifu sana, usiruhusu maneno mbaya kutoka kwa wazazi wako. Wazazi wako wanaposema “shauri yako yatakayo kukuta huko utajijua mwenyewe” au tutaona kama mtaishi na huyo mwanamke nk, fahamu Maneno hayo yatatokea tu. Vijana wengi na kina dada wengi hawana adabu kabisa kwa wazi wao. Wazazi wao wanawawanenea maneno mabaya sana. Sikiliza wanachokunenea kibaya kinafungulia laana.
Ondoa kiburi hicho ulichonacho kwa wazi wako, hapo ndipo utapata heri. Kumbuka kuoa au kuolewa ni baraka. Kama hauwaheshimu ndipo pepo wanapata nafasi ya kukuzuilia usiolewe au kuoa. Kumubka mumeo yupo na mkeon yupo ila laana itakuzuilia usikutane naye.
 Neno la Bwana linasema hivi “Mimi nayaumba matunda ya midomo; ..” (ISAYA 57:19). Mungu anatabia ya kuyaumba matunda ya midomo ya wanadamu, sasa usije ukawapa nafasi hiyo wazazi wako waseme mabaya sana kuhusu maisha yako ya mbeleni na kuzilia kuoa au kuolewa kwako. Usiwape nafasi, kama unagundua hawataki jambo ulitakalo wewe jifunze kukaa kimya kwanza. Ingia kwenye maombi, na ukipata kibari cha kuzungumza nao ndipo ukasema nao. Ikiwa wazazi wako wanakutafutia mwanamke au mwanaume usiye mtaka fahamu umetegwa sana.
Uwe makini, kaana Mungu muombe akutegulie mtengo huo. Pia muombe akupe hekima ya kuongea na hao wazazi wako. Si ufanye kwa hasira, sikiliza neno la Bwana lina sema hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. Omba Mungu atakutoa katika huo mtengo mimi namuamini Mungu sana.
 Ni na imani umeelewa sana sehemu hii, basi hakikisha unawaheshimu wazazi wako, pia inawezekana kabisa wazazi wako wakawa na sababu za maana sana lakini wewe kwa sababu ya utoto huzioni, ebu watii usikurupuke kuolewa tu au kuoa eti kwa sababu wewe unampenda huyo umpendaye, wazazi wamejaariwa na Mungu kuona, kuelewa na kujua mapema kuliko watoto. Wao wanaweza kumuona huyo kijana au binti kuwa atakusumbua sana, kutokana na tabia yake, wanapokuambia mapema basi usiwachukie, i kiwa hawamtaki kwa sababu eti kijana huyo anamcha Yesu na wao hawawataki watu waliokoka basi fahamu hiyo si sababu ya msingi tulia. Mwombe Mungu atakufungulia mlango wa kukubarika kwa wazazi wako. Usilazimishe, umenielewa?
Tubu ulipokosea  na uwaombe msamaha wazazi wako. Mungu akubariki sana
Wako
Mr Steven& Mrs Beth Mwakatwila