Ninawasalimu katika jina la Bwana wetu mwema Yesu Kristo. Mimi na familia yangu ni wazima kabisaa tunamshukuru Mungu. Tumekua na mfululizo wa semina mbalimbali na tumemuona Mungu akitufundisha na kuwaleta watu kuja kujifunza. Tunawashukuru watu wote wanaotuombea na wanaotoa sadaka zao ili kuwezesha semina hizi. Mungu awabariki sana.

Hebu tuanze kuangalia salamu za mwezi huu wa sita..  Kumbuka tunasalamu zinakichwa hiki

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKAIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA AU KUOLEWA).

Katika salamu zilizopita tulijifunza eneo lile la tulia Mkeo au mumeo yupo. Leo nataka tusogee mbele kidogo.. Tuangalie eneo hili la

JIFUNZE KUKEMEA NGUVU ZA GIZA (MAPEPO MAHABA) 

Pia shetani anawafanya watu wengine wawe watu wa namna hiyo, yaani anawafanya watu hao kuwa watumwa wa mapepo ya uzinzi kwa kufanywa wake wa mapepo au kuwa waume wa mapepo hayo. Nimekutana na watu wa namna hiyo na nikawaombea wengi wamefunguliwa.

Unajua watu wa namna hiyo wanazuiwa na mapepo hayo kuoa au kuolewa, na ikitokea tu mwanaume akataka kumuoa binti wa namna hiyo mara nyingi utakuta mipango yao ya kuoana haifiki mbali. Na hata wakioana ndoa yao huwa na matatizo sana. Hawatakuwa na maelewano kabisa, hawatapata watoto, na hata uchumi wao unaweza kuvurugwa kabisa na pepo huyo mke au pepo mume. Wengine hufa mapema kisa ni hiki cha kuoa au kuolewa na mtu mwenye kumilikiwa na pepo. Mtu yeyote yule aliyeolewa na pepo wa mahaba, ni rahisi sana kumkuta mambo kama hayo.

Wanawake wengi sana wanatatizo hili pasipo wao kujijua. Tumekutana na wasichana wengi sana wenye tatizo hili katika huduma hii aliyotupa Mungu mimi na mke wangu ya kufundisha. Pia tumekutana na vijana lakini si wengi kama wasichana wenye mapepo ya namna hii. Inanisikitisha sana ninapowaona kinadada wazuri wa tabia uso na umbo, lakini hawaolewi, ukimuombea unashangaa pepo analipuka na kudai huyo dada ni mke wake.

Wengine wamekuwana mapepo hayo mpaka ndani ya ndoa, yanawafanya kina dada hao kuwa wakali wenye hasira sana na wagomvi kwa waume zao kisa ni ili waachane tu. Unaweza kujiuliza swali ntajuaje kuwa ninapepo la namna hii?

Yapo mambo mengi yanyoweza kujitokeza kwa mtu mwenye pepo la namna hiyo. Ebu tuyaangalie mambo machache. Jambo la kwanza anza kufuatilia ndoto zako unaota nini mara kwa mara. Ikiwa mara kwa mara unaota unazini ndotoni asilimia kubwa unalopepo linalozini na wewe. Na kadri siku zinavyozidi kwenda litakumiliki kabisa na kuwa mke wake au mume wako. Watu wengine wanatokewa kabisa na roho hizo waziwazi na kuzini na hizo roho. Lakini wanaogopa kusema wanaishi maisha magumu sana. Sikiliza tafuta mtumishi wa Mungu aliye mwaminifu mwambie habari hiyo, atakuombea na utafunguliwa kabisa. Jambo lingine ni kuota unazama chini ya maji ukiwa na mwanaume fulani mara kwa mara, hata kama huyo mwanaume unamfahamu ila hajakuambia wewe habari za kukuoa. Ukiona unaota ndoto za namna hiyo mara kwa mara fahamu kunaroho ya namna hiyo imekukalia.

Pia wengine hujikuta wamechafuliwa sehemu zao za siri mara kwa mara, yaani kwa siku hata mara mbili nk. Hasa wanawake. Ukiona hivyo fahamu inawezekana kunaroho ya namna hiyo imekumiliki pasipo wewe kujua. Wengine ni namna ya jinsi wanaume au wanawake wanavyowakimbia. Ukiona umeachwa na wanaume wengi au wanawake wengi amabo mlipatana kuoana fahamu inawezekana kuna roho inayozuilia jambo hilo.

Unaweza kujiuliza roho hizo zinatokana na nini? Yapo mambo mengi, lakini tuyaangalie machache. Jambo la kwanza ni kutokumuabudu Mungu na kumtii. Watu wengi sana leo hii hawajui kuwa Mungu anapotupa maagizo yeyote yale anakua anataka kutulinda na kutuokoa na mambo mabaya ambayo adui shetani amepania kututendea. Mfano wazazi wako au wewe mwenyewe mnapokwenda kwa waganga wa kienyeji au wachawi mnakua mnajikabidhi mmilikiwe na mapepo. Kwa kufanya hivyo inakua rahisi mapepo kuwafuatilia watoto wakike au wa kiume.

Fikiria mama yako alikupata wewe kwa mganga wa kienyeji unafikiri ni nani anauhalali wa kukumiliki wewe? Ni pepo, sitaki kukudanganya ikiwa wewe leo hii unakwenda kwa waganga na kuomba dawa za kupendwa nakuambia ukweli hupewi dawa unapewa pepo la mahaba! Jiulize mwenyewe kunaushirika gani kati ya mti au maji uliyopewa wewe uyaoge unywe na kupendwa?

Fahamu kuna nguvu unapewa za kiroho za kukuwezesha wewe kupendwa, na nguvu hizo ni mapepo. Ngoja nikuulize swali hili umewahi kwenda kwa waganga wa kienyeji? Na wakakuchanja chale mwilini? Fahamu asilimia kubwa wamekupandikizia mapepo. Hiyo ni njia moja wapo ambayo watu wanafungulia mlango wa kumilikiwa na mapepo. Njia nyingine ni dhambi. Mungu anapokuambia usizini anajua kinachotokea kwa watu wanaofanya uzinzi yaani tendo la ndoa kabla ya majira na wakati. Sikiliza unapofanya uzinzi unapokea vitu furani kutoka kwa huyo uliyezini naye.

Ntakufundisha vizuri huko mbele. Angalia maneno haya ya Bwana yasemavyo. “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, wale wawili watakuwa mwili mmoja.” (1KOR 6:16).

Ili adui apandikize mapepokwa watu wengi humtafuta mtu mmoja, na kumwekea jeshi la mapepo ya mahaba, na huyo mtu anweza kuwa wakike au wa kiume, mtu wa namna hiyo mimi namwita “wakala” wakala huyo kazi yake kubwa ni kusambaza mapepo yaliyo ndani yake kwa kutumia njia ya uzinzi. Fahamu mtu wa namna hiyo anachofanya ni kuwafuata mabinti au kina kaka na kuakikisha wanazini ili augane naye. Neno kahaba kila mtu anajua kazi yake nini, umewahi fikiri kumbe unapokwenda kuzini tu unakwenda kuchukua tabia, magonjwa, roho nyingine kutoka kwa huyo uliyezini naye? Nakuahakikishia watu wengi walivamiwa na mapepo mahaba sikuile walipozini tu.

Wanatafuta nini kinachowazuilia kuolewa au kuoa kumbe ni pepo walilolipata siku ile walipozini. Sikia vijana wengi wanapokea roho hizo za kumilikiwa na mapepo kwakutumia njia ya kufanya punyeto! Wanawake pia pale wanapo sagana au wanapojisaga. Mtu ambaye anafanya punyeto anafungulia mlango wa pepo kutawala akili zake, Biblia inasema wazi kuwa wanazini na vinyago vyao, kumbuka neno vinyago ni mawazo mabaya. Sasa mtu aliyebobea kwenye kufanya punyeto hutuzini mawazoni au vinyago. Anpofanya hivyo ni rajisi pepo kumuingia, na matokeo yake pepo huyo atazini na huyo kijana kila mara kwa kutumia mawzo hayo.

Mungu anasema tumpende kwa akilizetu zote, fikili wewe ndani ya akilizako nani kazitawala pepo au Mungu? Fanya hivi tubu leo, nakuambia ukweli ukiendelea na kufanya hayo hautaolewa au kuoa, na ukioa ndoa yako itapatashida sana kwani pepo atakua tayari amekubana katika mawazo yako hutamfikilia mumeo au mkeo utamfikilia pepo ajaye mawazoni mwako kwa kukuleta sura za wanawake fulani au wanaume fulani.

Jambo lingine linalo weza kupelekea pepo kukuzuilia kuoa kwako au kuolewa kwako ni laana. Laana ina njia zake, lakini ngoja tuone laana inayotokana na kutowaheshimu wazazi wako. Ohoooo!!! NTAKUONYESHA LAANA HII KATIKA SALAMU ZA MWEZI UJAO.

Mungu akubariki sana na tuonane tena katika kona hii mwezi ujao. Barikiwa sana

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila
0754849924