Salamu – Aug, 2017

Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana. Mimi na familia yangu ni wazima. Tunamshukuru Mungu sana ambaye ametupa nafasi hii ya kukuletea salamu za mwezi wa Nane. Mwezi wa saba tumekua na semina mbili kubwa.

Tulikua na semina ya watumishi wa Mungu maaskofu na wachungaji wainjilist mjini Arusha na tukawana semina ya siku nane Dar es Salaam Moraviani Kiwalani. Ilikua semina nzuri.

TULIFANIKIWA KUWA NA MASAA KAMA MANNE HIVI TUKAWA NA VIJANA ILIKUA YALIKUA MASAA MAZURI SANA.
Katika huduma yetu hii Tumekua na semina Dar es Salaamu kwa uchache sana. Naamini Mungu anatufungulia mlango taratibu katika jiji hilo.

Tulipomaliza ilitakiwa tuludi tena Arusha tarehe moja mwezi hu wa nane tulikua na kongamano kubwa la watumishi wa Mungu kutoka nchi mbalimbali. Ilikua nzuri sana tumemaliza tarehe tano ya mwezi huu.

Kutokana na namna ratiba yangu ilivyokua imenibana nilishindwa kukuletea salamu za mwezi wa nane mapema. Leo hii nimeipata hii nafasi nimeona nikuletee sala mu hizi.

kumbuka tunasalamu zenye kichwa

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA NA KUOLEWA

Katika salamu zilizopita tuliangalia eneo lile la jifunze kuwaheshimu wazazi wako. Ebu tupige hatua kidogo. Tuangalie jambo lingine muhimu nalo ni

USIMUWEKEE MUNGU MIPAKA KATIKA SUALA HILI LA KUOA AU KUOLEWA

Jambo lingine muhimu sana ambalo unatakiwa ulifanye ili uanikiwe katika suala hili la kuoa au kuolewa kwako ni hili la kutomuwekea Mungu mipaka. Watu wengi sana wamejikuta wame kwama katika mipango yao ya kuoa au kuolewa ni kwa sababu ya kumuwekea Mungu mipaka katika suala zima la kuoa au kuolewa.

Nakumbuka mimi kabla sijaoa nilijiwekea utaratibu ambao baadaye nilikuja kugundua kuwa nilimuwekea Mungu mpaka katika suala la kuoa kwangu, mimi nilijiwekea utaratibu huu, kwanza nilipanga kuwa sitaoa mpaka, moja, nipate kazi, mbili niwe na nyumba yangu, tatu,niwe na gari, jambo la pili,nilikuwa na muomba Mungu anipe mwanamke ambaye ni mwembamba, halafu mcheshi, sikutaka kabisa mwanamke mfupi, nilitaka mrefu,si unajua tena Mamiss…unajua nilikuwa naomba Mungu anipe mwenye miguu ya namna hii……!

Unajua nilikuwa na bidii sana ya kuomba mapema mwanamke mwenye umbile nilitakalo mimi na tabia niitakazo mimi. Sasa sikia siku moja ilikuwa usiku kama saa mbili hivi , naikumbuka sana hiyo siku, nilikutana na mtu mmoja, ambaye ameokoka, ndugu huyo alikuwa hajui kabisa maombi yangu na mipango yangu katika suala hili la kuoa, akaniambia hivi “Steven Unafahamu ni kwa nini watu wengi sana Mungu anashindwa kuwasaidia katika maisha yao?

Nikasema najua yapo mambo mengi wengine hawataki kumtii nk, yeye akaniambia jambo lingine ni hili WATU WENGI SANA HAWAFANIKIWI KWA SABABU WAMEMUWEKEA MUNGU MIPAKA” nikamuuliza kama mipaka ipi? Akaniambia watu wengi hawaolewi na hawaoi kwa sababu wamemuwekea Mungu mipaka, akasema wengine wametaka kuoa wakiwa na kazi au wengine wametaka kuoa wakiwa na magari au na umri fulani wengine wakiwa wamejenga nk,

Unajua alizungumza sana kwa namna ambayo siwezi kuielezea vizuri,sikumwambia kuwa hata mimi nimeweka mipaka ya siku ya kuoa kwangu, baada ya kuachana na huyo ndugu,nikaenda nyumbani kwangu,nikamwambia Mungu nimekosa nisamehe hata mimi nimekuwekea mipaka,ya kuoa kwangu,sasa naomba mapenzi yako yafanyike katika jambo hili.

Mimi nilimwambia Mungu anipe mke nitakapokua nakazi na nikiwa nimejenga nyumba yangu na nikiwa nimepata angalau gari la kutembelea .

Unafahamu, baada ya kuomba maombi hayo, bado niliendelea kumuomba Mungu anipe mwanamke mwenye sifa nizitakazo mimi, kimaumbile na hata kitabia.

Nakumbuka siku moja baada ya maombi ya namna hiyo,Mungu alisema nami,alisema nami kwa sauti,akaniambia,Steven,chukua kalamu na karatasi nikufundishe, nikatii, nikachukua kalamu na daftari akaanza kunifundisha.

Akaniambia, nisimuwekee mpaka katika jambo hili la kuoa kwangu, akaniambi ntakupa mke mwema, si kama vile wewe unavyotaka, akaniambi mkeo niliyekuandalia anaweza asiwe kama umtakavyo wewe, akasema usiniwekee mpaka, wewe omba nikupe mke mwema!

Fahamu si dhambi kuomba Mungu akupe mwanamke mwenye sifa uzitakazo wewe, lakini Mimi naludia tena mimi,niliambiwa niombe anipe mke mwema. Kweli Mungu Amenipa mke mwema,.

Mimi nilikua na maombi haya, nilitaka mwanamke mwembamba mrefu mweupe!!! Mtundu mtundu hiviii!!! Sikutaka mwanamke mkimyaaa mpole mpole hiiviiii!!! Nilitaka mwanamke msemaji hiviiii eheheeeeeee!!!!!!

Sasa Mungu aliponifundisha hivyo niliona wazi kuwa nilimuwekea mpaka. Siku ile aliniambia wazi kuwa, wewe unaniomba nikupe mke na unanipangia mke umtakaye wewe basi unaye, alinifundisha waziwazi kuwa mke wa kunifaa mimi yeye ndiye anayemjua na umbo lale na rangi yake yeye ndiye anaye mjua.

Niseme nisiseme!!!! Mungu alipokua ananisemesha kuhusu mke wangu Alinipa mwanamke ambaye ni mwembamba kabisaa tena mrefu kiasi, Ila si msemaji kabisaa, mtu wa kukaa kimya hasa anapokua na mimi. Akiwa na wenziwe huko atazungumza ila akiwa na mimi hasemi kabisaa. Mungu aliniambia kuwa mwanamke huyo wala si mwembamba ni mnene hasa.
Nilipomuoa akiwa mwembambaa nilimwambia wazi kuwa wewe ni mnene sana tu Mungu alinionyesha.

Unajua baada ya kupata mtoto wa kwanza akaanza kunenepa sana, ndipo nilipo kumbuka kuwa umbile hili Bwana alishaniambia siku nyingi,kuwa wewe omba mke mwema kwani anaweza akawa na umbile ambalo silihitaji, namshukuru Bwana kwa kuniambia mapema,

Unajua kwa sasa nalipenda umbile lake alilonalo sasa , kwani linanipa mimi heshima hata yeye kwa watu, unajua kila mtu anajua wazi kuwa nyumba ya Steven imebarikiwa kwa kumuona tu mke wangu! Unajua kila mtu anasema kweli unamtunza vizuri sana mkeo amenenepa hivi!

Hata wewe na kushauri usimwekee Mungu mipaka kwa mfumo kama huo wa kumchagulia au kumwambia unataka mwanamke au mwanaume wa aina gani. Ebu fikiria kidogo. Ikiwa wewe unachaguo lako wewe na Mungu anachaguo lake yeye la kukufaa siku atakapokuletea utakataa tu.

Ndiyo maana watu wengi mno wamekwama kisa ni hiki hiki wanamachaguo yao na Mungu anachaguo lake mpaka mtu ashuke na kupokea chaguo lililotoka kwa Mungu.

Maandiko yako wazi yanasema mke anatoka kwa Mungu, hatoki kwa mtu, sasa huyo mtu ili ampate mke kutoka kwa Mungu lazima kwanza ajiachie moyoni mwake kumpokea huyo mke kutoka kwa Mungu. Wewe leo hii unaweza fikiri kama wewe na ukataka kama wewe mke au mume mfupi au mrefu kumbe chaguo la Mungu ni tofauti sana na mtazamo wako.

Usitegemee Mungu atakupa mume au mke ikiwa wewe unamtazamo tofauti na yeye. Ninachotafuta hapa ni hiki nikukuonyesha mpaka mkubwa ambao watu wengi wameuweka na unawazuilia wasipewe wake zao au waume zao na Mungu.

Fikiria kidogo wewe humtaki mfupi na Mungu akakuletea huyoooo mfupi utampomea kweli? Kwanza akija tu huwezi hata kwenda kumuuliza Mungu si umeisha mkataa mapemaaaa?
Na Mungu pia anajua sana kuwa furani hataki mfupi na mbinguni wanajua wakwako ni mfupi hata kabla haujaletwa duniani unafikiri watakuletea huyo mfupi?

Hawakuletei kwasababu wanajua umewabana kwenye chaguo lako. Siku utakapo ondoa hilo chaguo lako na ukawa tayari kumpokea atokaye kwa Mungu na yeye akikuona moyoni mwako kuwa unataka kitu chema kutoka kwa Mungu nakuhakikishia watakuletea haraka katika kipindi kilichoamriwa mbinguni.

Unajua ni rahisi sana leo ukajikuta ukipishana na Mungu kwenye eneo hili kisa ni hiki hiki. Wewe unamtaka mweupe kumbe mbinguni hawajawahi kukuandalia mweupe ni mweusi. Sasa angalia huku chini umekazana kuomba na kumsubiria huyo mweupeeeee atokeee ghafra anatokea mweusi tena mweusi kwelil kweli Ahahaaa!!! Unafikiri utampoke? Si rahisi

Akitokea tuuuu laxima apigwe chini, kumbe ndiye wakwako. Nimewahi wasikia watu wengi sana wananiuliza mtumishi hivi wewe uwe na mtazamo wa kuoa mwanamke wa aina furani, na Mungu anakuletea wa aina nyingine je! Inawezekana kweli?

Mimi nakwambia inawezekana kabisaaaa!!! Unajua kwanini? Kwasababu Mungu ndiye anayemfahamu wa kukufaa wewe na ndiye aliumbwa kwa ajili yako. Wewe bahati mbaya kabla haujaanza kumuuliza Mungu ulijianzishia moyoni mwako yakwako kabisaaa nakuambia mtatofaitiana tu. Na nirahisi kufuatwa na mtu unaye mtaka wewe na ukafikiri Mungu kapenda kabisaa kumbe walaaa!!!!

Jifinze kumuomba yeye akutafutie wakukufaa wewe wala si wewe kumtafutia wa kukufaa ili akuletee. Unaweza kumpa taarifa kabisaa juu ya mtazamo wako. Usiogope kumwambia Aisee mimi Bwana Mkubwa napenda mwanamke mwenyeeeee miguu mikubwa au mwenye macho ya aina furani au mwenye makalio makubwa makubwa usisite kabisa kumwambia. LAKINI UWE TAYARI KUMSIKILIZA FUNDI STADI ALIYEKUUMBIA WAKWAKO KWASABABU YEYE ANAMFAHAMU. Ondoa mapenzi yako ruhusu mapenzi yake yafanyike.

Sasa ni rahisi kuomba mapenzi ya Mungu yafanyike, ila ni ngumu kuyapikea hayo mapenzi ya Mungu. Kwasababu mara nyingi tunakua na mapenzi yetu ndani ya mioyo yetu. Na tutataka kuona mapenzi yetu yakifanyika. Usifikiri ni rahisi kutembea ndani ya mapenzi ya mtu mwingine. Nikazi ngumu inayohitaji unyenyekevu mkubwa mno. Mimi naamini hivi. Watu wengi hawaolewi na kuoa kwasababu hii ninayokuambia ya kumuwekea Mungu mipaka.

Mungu ukimpenda na akajua kuwa umemuwekea mpaka katika habari hii, nakuhakikishia ATAKUZUILIA KUOA AU KUOLEWA MPAKA UTAKAPOUONDOA HUO MPAKA.

Basi usizidi kujichelewesha fanya bidii kumuomba Mungu akutafutie na usitafute wewe. Jifunze kumtafuta yeye akuhakikishiye wala si wewe ujihakikishie ntakufundisha vizuri huko mbele.

Mungu akubariki sana tuonane mwezi ujao katika kona hii ya salamu za mwezi.Amani ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila