Salamu – Dec, 2017

Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana . Ninakila sababu za kumshukuru Mungu aliyetupa mwezi huu wa kumi na mbili. Kumbuka ni mwezi wa mwisho katika miezi yooote katika mwaka. Ndiyo tuna maliza mwaka huu wa 2017. Ni Neema kubwa hii.

Mwezi ulipita tumekua na semina nyingi sana . Asanteni kwa maombi yenu. Ebu nikuletee salamu za mwezi huu wa kumi na mbili.

JIFUNZE KUTENGENEZA MAZINGIRA MAZURI YA KIUCHUMI ILI UWE NA UWANJA MPANA WA KUKUBARIKA

Kumbuka katika salamu za mwezi ulipita nilikuahidi kukuletea salamu  zitakazohusu habari za ili uweze kufanikiwa kwenye kona ya kuoa ni lazima ujue habari za uchumi au uhakikishe unamiliki mali.

Unaweza usinielewe haraka. Sikiliza. Mwanamke yoyote yule ambaye anatarajia kuolewa ndani yake huwa na mtazamo mkubwa wa kuona anaolewa na mwanamume ambaye atamtunza na kumpatia raha.

Kwa hiyo mwanaume yoyote ambaye anawito wa kuoa  ni lazima  alijue hili. Sikia nikwambie ili uwe na uwanja mpana wa KUKUBARIKA Ni lazima Uhakikishe unakua unafanya bidii katika eneo la uchumi wako.

Ngoja nikuonyeshe hii mistari naona ndiyo kijana utanielewa vizuri angalia maneno haya.

“Pia nimeona hekima chini ya jua, nayo ni kama hivi, tena kwangu mimi ilionekana kuwa ni neno kubwa.Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga. Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini. Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi. Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa, Zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu.Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.”(Mhubiri 9:13-18)

Ukiipitia hiyo mistari utagundua mambo mengi sana ya kujifunza. Mtu huyo alikua na hekima kabisaa,  lakini utaona  kwasababu tu alikua masikini hakukubarika. Siyo mimi nasema ila Biblia inasema hivyo. Na mimi naliamini neno la Mungu kabisa.

Naninajua kila neno lenye pumzi ya Mungu linafaa kwa mafundisho.  Mungu aliliachia neno hilo kwa makusudi kabisa ili atufundishe sisi  mfumo mzima wa nini tufanye ili tutengeneze wigo mpana wa kukubarika Iwe kwenye jamii taifa au katika hili la kuoa kwetu.

Mimi nakwambia ukweli hakuna kitu kibaya kama umasikini. Umasikini unamuondolea mtu alionao kibari.  Maandiko yanasema hivi.”Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi.”(Mithali 14:20)

Angalia  na hii  mistari mingine pia ” Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu. Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.” (Mithali 19:4-7).

Fikiria kidogo. Kama masikini hakubariki hata na ndugu zake tu, unafikiri atakubarika kwa msichana atokae kwa ndugu wa mbali naye kabisa?

Ili uoe lazima utengeneze ukaribu na huyo mwanamke, sasa sikia maandiko yanasema maskini hutengwa na marafiki hata awafuate kwa maneno wao huzidi kujitenga naye.

Na ili uoe lazima upeleke neno kwa huyo mwanamke, sasa angalia kitakachotokea kama wewe kijana ni masikini maneno yako hayasikilizwi na huyo mwanamke atajitenga na wewe tu.

Ndugu wa huyo mwanamke ndiyo hawatakukubali kabisaaa nakwambia!!!! Nimeona wazazi wengi wa wanawake huwakatalia vijana watakao kuwaoa watoto wao. Unajua sababu kubwa imebebwa na jambo gani? Ni kutokana na hili ninalo kuambia umaskini tu.

Ni familia chache duniani zinajua kuwa maisha ya mtu yanaweza badilika kabisa huko mbeleni, wengi huangalia muda huu huu, hawaelewi habari za kesho sijui anaweza kuwa na uchumi mkubwa.

Ni wasichana wachache sana wana imani hii ya kuwa Mungu anaweza kubadilisha uchumi wa huyu kijana ngoja niolewe naye tu. imani hii wengi hawana wanaangalia hali ya leo hii, wanafikiri hivi nikiolewa na huyu ndugu usalama wangu wa kimaisha utakuaje? Kweli nampenda lakini uchumi wake ulivyo hapana kwa kweli. Mwisho wa siku utaona ni kijana wa kiume kuumizwa tu.  Na kubaki na wimbo wa umasikini huu jamani!!

Biblia inasema hivi.”Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa!”(Wim7:6)

Ukiipitia mistari unaona wazi kuwa mapenzi huchochewa na vitu pia. Ili watu wawe na kitu anasa fahamu lazima na uchumi mzuri. Sasa sikia ili mwanaume uwe na mlango mpana wa kukubaliwa na mwanamke lazima ujue ni kitu gani ufanye ili huyo mwanamke avutiwe nawewe nacho kinaweza kabisa kikawa ni uchumi ulionao.

Utamu wa mapenzi au kupendwa mwanaume unaweza ukachochewa kabisa na mfumo wa uchumi wako. Watu wengi hufikiri eti kwakuwa hawa wanawake wameokoka basi wakifuatwa tu na wanaume waliookoka na kuwaomba waoane basi  kwa kuwa hao wanawake wameokoka watakubari tu. Hakuna mwanamke asiyetaka raha nakwambia

Sikia hao wanawake waliokoka ni watu kabisaa. Wanamambo wanayo yahitaji maishani mwao. Nimewasikia wanaume wengi wakiwalumu wanawake kisa eti wanawataka wanaume wenye uchumi mzuri tu. Bahati mbaya sana wanaume wengi hawaujui moyo wa mwanamke ulivyooumbwa.

Moyo wa mwanamke na moyo wa mwanaume upo tofauti sana. Kuna vitu wao wamevibeba moyoni ambavyo sisi wanaume hatunavyo kabisaa. Ngoja nikupe mfano huu.

Angalia. Hii mistari.”  Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;”(Waefeso 6:25) angalia na hii pia. “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza;…”(Yohana 17:12) .

Ukiipitia hiyo mistari utaona wazi kuwa Bwana Yesu Kristo analipenda kanisa na si kulipenda tu maandiko yanatufundisha analitunza.

Hata mwanaume ameambiwa awe hivyohivyo kwa mke wake. Ampende na amtunze. Sasa hapo kwenye kumtunza mke. Mwanamke moyoni mwake anauhitaji huo wa kutunzwa kabisaa. Wanaume wengi hujaribu kukwepa hapo.

Tunafikiri wao wako kama sisi. Lazima ujifunze kuwa mwanamke anamambo yake moja wapo ni kuona mwanaume akimtunza. Mwanamke anafurahi akiona mwanaume ampendaye anamletea nguo, kiatu, soda nk. Hata kama huyo mwanamke anauwezo kiuchumi kweli -kweli, lakini moyo wake ni mwanamke tu.  Anahitaji kutunzwa

Mwanamke anafurahi sana moyoni anapomuona mwanaume anaye mjali na ili uyatende hayo lazima uwe na uchumi mzurikijana.

Unajua wanaume wengi wanafikiri kwakuwa wanawake wanaokoka basi hawawezi kufikiria habari za maisha yao yatakuwaje. Sikia Mwanamke ni mwanamke tu.

kunavitu wanawaza kama wanawake wanavitazama kama wanawake si eti kwakuwa ameoka basi anabadilika katika mtazamo wake hapana wapendwa.

Usimtazame hivyo ni mwanamke anahitaji kupendwa na kutunzwa. Wanaume sikia maandiko yanasema tuwapende na ndani ya upendo unajua kuna mambo mengi sana.  Moja ya jambo lililo ndani ya upendo ni ufadhili.

Maandiko yanasema upendo hufadhili. Sasa ndani ya ufadhili kuna kuwezesha au kutunza nk. Kwahiyo unapotaka kuoa na ili uwe na urahisi katika kuoa kwako lazima ufahamu kuwa mwanamke atahitaji kuuona uwezo wako wa kumfadhili si kumpenda tuuuu!!!!

Naamini umenielewa. Lazima uhakikishe unajenga mfumo mzuri wa uchumi wako ili uwe na mlango mpana wa kukubalika.

Tuonane tena katika salamu za mwezi ujao. Barikiwa sana.

Wako Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila

Tunapoachana nataka nikupe taarifa hii  uunaweza kupata masomo yetu mengine kwenye maeneo yafuatayo.
1.Website yetu ya www.makatwila.org
2. Youtube- Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU
3.Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga
4.Dvds au Cd
5.Vitabu
6.Kwa njia ya Redio mbalimbali

Kwa mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi. 0754849924-0756715222
Mungu akubariki sana.
Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila