Salamu – Aprili, 2021

Bwana Yesu Kristo asifiwesana. Naamini Mungu ameendelea kukutunza na kukupigania. Nikukaribishe tena ndugu yetu katika kona hii ya salamu za mwezi.

Hizi ni salamu za mwezi wa nne, kumbuka tuna salamu zenye kichwa

VIPAO MBELE VYA MAOMBI YAKO WEKA BIDII YA KUOMBEA MASIKIO YAKO.

Hebu tusogee mbele katika kujifunza somo hili

MADHARA YA KUTOKUSIKIA MATESO MENGINE TUNAKUTANA NAYO KWASABABU KUTOKUMSIKILIZA MUNGU ASEMAVYO.

Ili uone umuhimuwa somo hili ebu tuyaangalie kwa sehemu madhara ya kutokusikia.

1. MADHARA YA KWANZA KUJIKUTA WEWE NA JAMAA ZAKO KATIKA MAISHA MAGUMU

Angalia mistari hii uone “Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.” (Yeremia 22:21-22)

Ukiipitia hiyo mistari utaona huyu ndugu alikutana na magumu kisa ni kutokusikia tu. WATU WENGI WALIOFANIKIWA AU KUINULIWA WAKO KWENYE HATARI SANA KISA NI RAHISI KUMDHARAU MTU NA UKAKATAA KUMSIKIA….

2: MFANO WA PILI: UNAPOTEZA NAFASI AMBAYO MUNGU ALIKUPA

Angalia mistari hii isemavyo “Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme. Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA. Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.” (1Samweli 15:22-26).

Unapoisoma mistari hiyo unaona kitendo cha Sauli kutokusikia kilipelekea apoteze nafasi aliyopewa ya kuwa mfalme. Licha ya kupoteza kazi ndani ya mistari hiyo unaona madhara mengi tu aliyokutana nayo Sauli

Kuna mambo kama manne hivi alikutana nayo

1: Sauli alifutwa kazi.

2: Aliingizwa kwenye kundi la wachawi au walogaji
Sikia Mungu akisema na wewe na wewe usisikie fahamu unaonekana kama mchawi

3: Aliingizwa katika kundi la waabuduo sanamu au makafiri watu wasio na Mungu…

4: Sadaka yake ilikataliwa

Angalia mistari hii isemavyo “Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme. Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA. Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.” (1Samweli 15:22-26).

Biblia inatuonya sana kuhusu utoaji wetu wa sadaka.. Mungu anataka tusikie ndipo tutoe sadaka mahali tuliposikia tutoe. Angalia mistari hii “Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo.“ (Kum12:13-14)

Ngoja nikupe mfano huu. Nakumbuka nilikua na sadaka ya zaka. Na ninakumbuka nilitaka kumsikia Mungu akinipa maelekezo ya kuitoa hiyo sadaka.

Mungu alinipa maelekezo yaliyonistaajabisha na kunifundisha kitu, aliniambie niipeleke sadaka hiyo kwa viongozi wa kwaya fulani.

Kwaya hiyo haikuwa kanisani kwetu, ni kanisa tofauti sana na lile la kwetu.. nili tii nikaenda kuwapa, nilipofika pale kanisani niliwakuta wakiwa nje wanafanya mazoezi. Akaja kiongozi wao yaani katibu na mweka hazina nikawapa.

Baada ya siku nyingi kidogo kupita wale ndugu walikuja nyumbani kwangu, wakaniambia kuwa sikuile nilipowapelekea sadaka ile ni kweli Mungu alinituma, wakaniambia walikua wanaondoka kesho yake kwenda Dar es Salaamu kurekodi nyimbo zao.

Sasa walikwama nauli ya watu wawili, na waliwachagua vijana wawili waondoke na loli badara ya kuondoka na basi..yaani baada ya zoezi lao la mwisho siku hiyo vijana hao walitakiwa waende Uyole jijini Mbeya kutafuta malori yanayojwenda Dar Es Salaamu ili wawaombe madereva na walipe kidogo…hata fedha ya kujikimu kwa vijana hao wawili ilikua hakuna.

Waliniambia kuwa ulipotupa ile sadaka ilitoshereza nauli ya watu hao wawili kwenda na kukudi na pia kuwakimu katika mahitaji yao yoote. Nikajifunza kumtolea Mungu kwa kumsikia…leo hii watu wengi hutoa kimapokeo na hawaoni baraka

Mfano mwingine ni huu. Nakumbuka nilikua nataka kutoa sadaka furani kwa ajili ya semina ya neno la Mungu,kulikua na semina katika mji wetu. Mungu alinikataza nisitoe ile sadaka.. na nilipewa maelekezo nii toe moja kwa moja kwa mtumishi wa Mungu. Mimi nilikua mwanakamati niliona nivema nitoe kwenye kamati kuliko kumpa mtumishi moja kwa moja…Kweli niliitoa kwenye kamati..nilipotoa tu..nikajikuta sina amani kabisaaa… niligundua nimekosea nilitubu sana sana..

Baada ya semina nikasikia kuwa kiongozi mmoja kwenye kamati ile alichukua sadaka hizo na kufanyia mambo yake. Ndipo nilipofahamu ni kwanini Mungu alinikataza nisitoe pale na siku msikiliza..

KUNATOLEO UNAWEZA KUSIKIA KABISA MUNGU AKIKWAMBIA TOA KITU FURANI. AU USITOE KITU FULANI

Angalia mifano hii “Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng’ombe wa baba yako, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng’ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.” (Waamuzi 6:25-27)

Mungu alimpa Gideoni maelekezo ya nini atoe na atoeje, kama Mungu alisema na Gideoni kwa ajili ya utoaji fahamu hata sisi leo Mungu anaweza kusema kabisaa kwa ajili ya utoaji shida hatusikii na madhara yake ni kukosa baraka

Mfano wa pili angalia Mungu alimpa maelekezo ya utoajiIbrahimu “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” (Mwanzo 22:1-2)

Mungu alimpa Ibrahimu maelekezo ya utoaji wa sadaka hiyo na alimwelekeza mahali pa kuitolea..Ibrahimu alisikia na alipoitoa hiyo sadaka alibarikiwa sana yeye na uzao wake.

Yapo madhara mengi tu ya kutokusikia.nimekuonyesha mifano hiyo michache ili uchukue taadhari katika jambo hili. Weka bidii ya kuomba Mungu akupe sikio la kumsikiliza.

Naamini umeelewa tuonae tena katika kona hii mwezi ujao
Barikiwa

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222