Salamu – Agosti, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ni siku njema tena nimekuletea salamu za mwezi huu wa nane..

Naamini Umekua na mwezi wa saba mzuri sana, naamini mwezi huu wa nane Mungu atakupa mwezi mzuri. Pia..

Mwezi wa saba ksetu ulikua mzuri sana..Tulikua na semina nzuri sana huko wilaya ya Mbarali eneo la Chimala..Tulikua na semina ndani ya hema..Tulimuona Mungu akituhudumia kwa namna ya ajabu…

Na mwezi huo tulikua na semina maalumu ya watumishi wa Mungu wa shirika la Here’s Life Africa. Watumishi kutoka Dunia nzima wao na wake zao..Ilikua semina nzuri sana

Ebu pokea salamu za mwezi huu wa nane…nazo ziko hivi..

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Katika salamu zilizopita tulianza kuangalia jambo la linaloweza kupelekea jeraha moyoni mwako nalo lilikua ni Kupokea jeraha kutokana na kutarajia kitu kisichokuwa.

Katika salamu za mwezi huu nataka tusogee mbele kidogo tuangalie jambo la tano nalo ni hili

4: KUKAA NA MTU MBAYA

Ukiishi na mtu mwenye tabia mbaya yaani mtu mkali , jeuli asiye na huruma au rehema fahamu mtu huyo ataijeruhi nafsi yako na usishangae na wewe utajikuta unatabia kama ya kwake kabisaa….

Watu wengi leo ukiwaangalia nje walivyo..yaani sura zao utawaona ni watu wapole nk..lakini wakifumbua vinywa vyao utashangaa maneno yao na sura zao ni tofauti kabisaaa…hata kwa matendo yao ni tofauti na walivyo kabisaa

Utashangaa ni mtu anayekaripia tuu..hawezi kutia moyo mtu,anakua ni mtu aliye na huruma kabisaa..na usishangae mtu huyo anaomba sana na anashinda kanisani na kutumika..

Ukiishi na mtu mbaya mkali nk fahamu ataijeruhi nafsi yako tu, na usishangae utajikuta unatabia kama ya kwaketu…. Yaani utakua mkali na mkolofi kama yeye.

Angalia mistari hii.”Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema.”(Mithali 16:29).

Mtu mkali humtengenezea mwenzake tabia mbaya.. ukiipitia mistari hiyo utajifunza mambo mengi tu..moja ya jambo nililojifunza ni hili mtu mkali anawatengenezea wenzake tabia hiyo ya ukali.

Mfano Mara nyingi mtu anayefokewa mara kwa mara iwe na wazazi au kiongozi wake, hujikuta akibeba jeraha moyoni..

Maneno anayoambiwa huenda ndani ya moyo wa huyo mtu na kumkata na kumtengenezea uchungu

Angalia mistafi hii..(Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.”(Zaburi 57:4).

Maneno yanaweza kuwa upanga wenye kujeruhi kabisa…sasa sikia watu wengi wanapokutana na watu wabaya wanaowafokea na kuwajeruhi kwa maneno makali..fahamu hata wao inakua rahisi kujikuta wakiwa na tabia ileile ya kuwajeruhi wengine ..

Mtu wa uchungu moyoni ni rahisi kuwaambukiza watu wengine uchungu huo alionao moyoni.. Biblia inasema hivi “ mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”(Waebrania 12:15).

Biblia inasema wazi kuwa uchungu unaweza kutoka kwa mtu mmoja na ukawanajisi watu wengi mnoo..

Sasa sikia, unapoambatana na mtu mkali au hasira nyingi fahamu ni rahisi kujikuta unakuwa na tabia ileile aliyonayo yaani nafsi yako inakua imejeruhika

Sikia wewe hukua na tabia hiyo…umeipata tabia hiyo kutoka kwa mtu mbaya ambaye amekujeruhi hiyo nafsi yako.

Watu wengi wanameziharibu nafsi za watu wengi kwa kuwatengenezea tabia mbaya sana.. wewe fuatilia watu walioisi na watu wabaya utashangaa na wao huwa vilevile, ni wachache wanaopona.

Biblia inasema hivi …“Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;“(Mithali 22:24).

Kwanini Biblia inatuonya hivyo? Kuna weza kuwa na sababu nyingi sana. Moja ya sababu ni hii…mtu huyo atakujeruhi na usishangae jeraha hilo litakujengea tabia hiyo hiyo..

Ngoja nikupe mfano huu..watu wengi ambao wanaua watu bila kujali, ukiwasikiliza utagundua tabia yao hiyo ya kuuwa watu, ilitokana na jeraha walilojeruhiwa huko moyo mwao kwa kutokana na mfumo wa maisha ya kikatili waliolelewa na watu wakatili.

Sikiliza unaweza usijue kuwa unawaangamiza watu wengi kwasababu ya tabia yako ya kikatili uliyonayo.

Jifunze kuwatia watu wengine moyo…wafariji,uwe na rehema na huruma kwao…utakua mjenzi mzuri wa nafsi za watu..

Ukiona unatabia mbaya …ebu jichunguze umeipata wapi? Angalia makuzi yako…nani ulienda naye aliyekua anaambatana na wewe? nk.

Ukiona kuna mtu uliyeambatana naye na alikua hivyo fahamu alikujeruhi na ukajeruhika na ukajikuta ukiwa na tabia hiyo..

Hebu tubu, msamehe huyo aliyekujeruhi au kukutengenezea mfumo wa tabia hiyo mbaya… anza kuikataa hiyo tabia… ikatae kwa maombi na kwa kusema…kuwa hii si tabia yangu…nataka tabia yangu njema… Mungu atakupa.

Mungu akubariki sana.

Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222