Salamu – Septemba, 2022

BWANA Yesu KRISTO asifiwe sana.. TUNAMSHUKURU Mungu sana ambaye ametupa mwezi Huu wa Tisa.

Mwezi  uliopita tumekua na semina Maalumu ya watumishi Jijini MBEYA ilikua semina nzuri sana. Mwakani tunatarajia mwezi tena wa nane kuandaa tena semina ya watumishi..tuombee.

Mwezi huu wa tisa tutakua na semina zipatazo tatu..tutakua Makete huko Njombe, Tukuyu mjini Wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya.. na Chunya Iliyo pia mkoa wa Mbeya.. semina hizo zote tutafunga hema..Usiache kutuombea.

Hebu pokea salamu za mwezi huu..kumbuka tuna salamu zenye kichwa 

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Ebu tusogee mbele kidogo.. tuangalie jambo hili muhimu..

MADHARA YA KUIHIFADHI UCHUNGU MOYONI AU DALILI ZA MTU MWENYE UCHUNGU

Sikia unapohifadhi huzuni au uchungu  moyoni mwako fahamu kuna madhara mengi tu utakutana nayo. Ebu tuangalie baadhi ya madhara ya kuhifadhi uchungu moyoni mwako.

1: MADHARA YA KWANZA   UCHUNGU UTAKUZUILIA WEWE KUSIKIA KILE CHEMA MUNGU AU WATU WAKUAMBIACHO

Watu wengi leo wanaonekana machoni pa watu kuwa wanakiburi.. yaani si watii wa kile wasikiacho au waambiwacho kutoka kwa Mungu au wanadamu. Kwa lugha nzuri wanaitwa wabishi.. na watu wa namna hiyo kwa kweli hujikuta wakikwama kwenye mambo mengi sana..

Wengi hupoteza ushirika na Mungu au watu.  Watu wa namna hiyo kiukweli hawakubariki machoni pa watu..wengi hujikuta wakipigwa na waume zao, na hata kuachwa, au wengine wanakimbiwa na wake zao nk. Kisa uhesabika ni watu wenye kiburi.

Sasa sikia, tabia hiyo inaweza kuwa na vyanzo vingi tu. Moja ya chanzo cha tabia hiyo ni uchungu uliohifadhiwa kwa muda mrefu moyoni mwa mtu huyo.

 Ngoja nikupe mfano huu.. Angalia mistari hii.“ Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.”(Kutoka 6:9).

Ukiipitia mistari hiyo utakiona hiki ninachokuambia mpendwa. Watu wenye majeraha moyoni yaliyopelekea wawe na uchungu, iwe kutokana na maisha magumu wanayokutana nayo, au walioumizwa na ndugu zao katika makuzi yao au waliojeruhiwa kutokana waalimu wao, au viongozi kazini nk.

Wengi ( si wote) Huwa na tabia kama hiyo ya kutokusikia…Kwa lugha nzuri hawashauriki na ni wabishi mtaani wanaitwa wagumu

Angalia mfano huo hapo juu, utaona hao ndugu hawakumsikiliza Musa..kumbuka Musa alitumwa na Mungu kwa watu hao..lakini watu hao hawakumsikiliza Musa, kwa maana nzuri hawakumsikiliza Mungu.

Nampenda Mungu sana..unajua neno lake hapo linatupa maarifa au kutujulisha 

chanzo cha kutokusikia kwao ni uchungu uliowajaa mioyoni mwao.

Ukiona watu hawawawasikii watumishi wa Mungu kwa kutii kile wawaambiacho fahamu huenda mioyo ya watu hao imejeruhiwa huenda na watumishi hao hao au watumishi wa Mungu waliopita.. Na kwa kweli watu hao wasipoondoa uchungu huo au kuponywa hizo jeraha ni ngumu kumsikiliza Mungu awatumae hao watumishi.

Ukiona mtu, hawasikilizi marafiki zake wanapompa ushauri, au hawasikii viongozi wake wawe wa kisiasa nk..ebu mchunguze mtu huyo..usishangae kuona hiki ninachokuambia..uchungu moyoni umemtengenezea tabia ya kutokusikiliza.. Huenda wanasiasa au hao marafiki zake ndiyo waliomjeruhi na akapata uchungu huo moyoni.

Watu wa namna hiyo wengi huwaita watu wa msimamo..sikia ni vizuri kuwa mtu wa msimamo..lakini mpendwa kuna misimamo inayoundwa kutokana tabia za majeraha ya moyo tu.

Wewe ebu mfuatilie mtu huyo,utaona mtu anaamua kuacha kazi..unamuuliza sasa ukiacha kazi unaenda wapi? Na ukiacha kazi hii utafanya kazi gani?

Ukiona anakupa jibu anakuambia anajua Mungu..wewe mfuatilie mtu huyo utaona amejeruhiwa huko kazini..anaacha kazi kisa kazi imemjeruhi..au watu waliopo hapo kazini.. 

Ndiyo maana anaiacha kazi bila maandalizi na hakuna atakae msikiliza akimpa ushauri wa kutulia hapo kazini. 

Umewahi kutana na mwanaume aliyejeruhiwa moyoni na mkewe au uchumi na hawaambii kuwa anajeraha moyoni? kisa ni mwanaume?

Utawaona wengi wanakimbilia kunywa pombe..sasa jipangeni mumwendee kumpa ushauri wa kuachana na pombe..Hata wasikiliza kabisaa..kisa uchungu tu uliomjaa moyoni mwake tu.

Umewahi kutana na mtu aliyejeruhiwa na mwanaume akiwa binti? Unajua wengi hujikuta hawaamini wanaume wengine kabisaaa..utasikia wanaume wooote waongo!!! Ukiona mtu wa namna hiyo fahamu kuna jeraha moyoni.. kama si yeye alijeruhiwa na mwanaume..basi rafiki yake au mama yake…si unajua ni rahisi shina la uchungu likachipuka na kuwanajisi na wengine?

Wanawake wengi huwa wanaambiana habari mbaya tuuuu za wanaume…tokea wakiwa mabinti..hata aje mwanaume mwema ni ngumu binti wa namna hiyo kumsikiliza..

Kutana na mwanaume aliyejeruhiwa na wanawake..wengi huchelewa kuoa..kisa jeraha..haamini mwanamke yoyote..hata akioa hiyo ndoa inashida mpaka huyo mwanaume apone huko nafsini…watu wa namna hiyo hawasikii ushauri wa mtu aitwaye mke nakwambia…

Wanaume wa namna hiyo hujihisi kusalitiwa tuuuu!!! Kudanganywa tuu, kupotezwa tuu na wanawake..

Hawawaamini wake zao..mwisho ndoa zao hubeba ugomvi tu..kaa na mwanaume wa namna hiyo kukusikiliza ni kazi sana..utasikia anakwambia wewe huwajui wanawake nakwambia!!

Ataanza kukuambia udhaifu wa wanawake utafikiri ni profesa furani wa  tabia mbaya tu za wanawake ..usipokua makini utashangaa ugonjwa huo kakuambukiza na wewe….Eheheheeee!! 

Kweli nakwambia..atakwambia habari Adamu kudanganywa na mwanamke yasni Hawa, atakwambia hari za  Ibrahimu kudanganywa na Sara mkewe kuzaa na mjakazi, atakwambia habari za Samsoni na Delila nk !!! 

Nafsi au moyo wake kwa kuwa ulijeruhiwa na mwanamke na anauchungu nao hao wanawake… hawezi ona jambo jema lolote kutoka kwa mwanamke..

Wewe kutana na mtu aliyejeruhiwa kiuchumi..usishangae akimkasilikia kila aliyefanikiwa..utasikia wezi tu hao……au utasikia akisema watu wa nchi hii wooote ni wezi tu……ukimpa ushauri wa masuala ya uchumi, hakusikilizi kisa anaona eti unamdharau, anaona kama unamsinga vile..usishangae ndiyo anakata mguu kwa kabisa…

Ukikutana na mtu wa namna hiyo angalia kwanza moyoni mwake kumejaa nini kama si uchungu…

Nimalizie kukutia moyo ndugu yangu.. usijiruhusu kuifadhi uchungu moyoni mwako kwa muda mrefu. Biblia inasema hivi “ Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;wala msimpe Ibilisi nafasi.”(Waefeso 4:26-27)

Ukiona mtu..hasikii, ebu msaidie..muombee kwa Mungu,shughulikia uchungu ulio moyoni mwake..mpe maneno ya faraja,mtie moyo,

Uchungu huo ukiondoka huyo mtu atakusikiliza..Sikia kunagharama ya kushughulikia uchungu ulio moyoni mwa mtu au kwako.. usichoke wala kukata tamaa msaidie.

Pia jifunze kukubaliana hali uliyokutana nayo..acha kuafikiria na kuyabeba mambo yaliyokuumiza ya zamani..

Tumalizie kwa mistari hii… “ Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.”(Isaya 43:18)

Bssi mpendwa yaachilie mambo yanayokuumiza ya zamani…KUNA JAMBO JIPYA MUNGU ANATAKA AKUTENDEE…

Ili akutendee utatakiwa umsikikizd, ili umsikilize lazima uondoe uchungu moyoni mwako..!!!

Hebu tubu kwa kuhifadhi uchungu kwa muda mrefu..mpende au wapende waliokujeruhi, wasamehe, UTAJIKUTA UNAANZA KUSIKILIZA.

Ndugu naamini umenielewa

Mungu akubariki sana.

Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
 9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.