Bwana Yesu Kristo asifiwe.. Tunamshukuru Mungu ametupa mwezi huu wa Tano. Katika mwezi huu wa tano tumekua na semina nzuri ya Wanawake na tumeifanya Sumbawanga mjini.
Tulikua na semina nzuri sana, Tunamshukuru sana Roho Mtakatifu kwa kazi hiyo nzuri… Mwezi huu pia tunatarajia kuwa na semina jijini Mbeya kwenye viwanja vya Otu( SIDO) tarehe 27-31/5/2026 kuanzia saa tisa jioni.. Tunaomba maombi yako kwa semina hii pia wape na watu wengine taarifa hii..Karibuni sana
Hebu tuanze kuzipokea salamu za mwezi huu.. Kumbuka tuna salamu zenye kichwa
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA MIUJIZA NA UPONYAJI ( SEHEMU YA PILI)
3: MUNGU HUTUMIA MIUJIZA ILI KULIDHIBITISHA NENO LA MUNGU LILILOLETWA NA WATUMISHI WAKE.
Mungu anapotaka kuridhibitisha neno lake lililoletwa na watumishi wake anaweza kutumia miujiza ili watu wajue kuwa neno hilo limetoka kwa Mungu.
“19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.“ (MARKO 16:19-20)
Kwa mujibu wa mistari hiyo utajifunza kuwa Mungu hutumia miujiza au ishara ili kuridhibitisha neno la Mungu.
Sikia unapoona miujiza ikitokea mahali moja ya sababu ni hii, Unajua watu wengi wanaposikiliza neno la Mungu kwa kutumia vinywa vya watumishi hujikuta wakiwa na mashaka sana ya maneno hayo.
Sasa sikia ili Mungu apate kurithibitisha neno lake hutumia miujiza.
Angalia mistari hii “6 Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya.” (Mdo 8:6).
Mungu alitumia miujiza ili kuwafanya watu hao wasikie neno la Mungu lililoletwa na kinywa cha Filipo.
Sikia usisite mtumishi kumpa Mungu nafasi ya adhibitishe neno lake, usitafute wewe kulidhibitisha neno la Mungu, Mwachie Bwana Yesu Kristo alidhibitishe hilo neno..Ukisukumwa kuwaombea wagonjwa wewe waombee, au kukemea nk.
Sikia ukifanya hivyo tu, usishangae kuanza kuona miujiza ambayo Mungu anaitumia ili kuridhibitishia neno lake Mungu.
Basi sikia taka Mungu akupe karama hii miujiza ili neno la Mungu liwe na uthibitisho
Naamini umenielewa. Mungu akitujalia tuonane tena katika salamu za mwezi ujazo..
Mungu akubariki sana.
Ukihitaji masomo yetu, unaweza kuyapata kwa njia zifuatazo:
1. App yetu ya huduma yenye jina “HUSONEMU (MWAKATWILA)” — inapatikana Play Store, ambapo kuna masomo mengi sana.
2. Tovuti yetu: www.mwakatwila.org
3. YouTube: HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU
4. Facebook: ingia kwenye tovuti yetu uone alama ya Facebook (f), kisha “like” ili upate maelezo ya kujiunga, au tafuta “SOMA NENO LA MUNGU”
5. Instagram: tafuta “Huduma ya Soma Neno la Mungu”
6. DVDs 📀 au CDs 💿
7. Vitabu
NB: Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733 ili kupata vitabu, DVD na CD.
8. Kwa njia ya redio:
- Rungwe FM 102.5 MHz — Jumapili saa 3:00 hadi 4:00 usiku
- Baraka FM 107.7 MHz — Jumanne saa 12:00 jioni hadi 1:00 usiku
- Bomba FM 104.1 MHz — Ijumaa saa 3:00 hadi 4:00 usiku
9. Online Radio: radio.mwakatwila.org
Ratiba ya vipindi:
- Saa 12:00 asubuhi
- Saa 07:00 mchana
- Saa 12:00 jioni
- Saa 03:00 usiku
10. Ingia MWAKATWILA YouTube Online
Kwa mawasiliano zaidi:
+255 754 849 924
+255 756 715 222
Wako,
Mwl. Steven Mwakatwila & Beth Mwakatwila