Karibu Huduma ya Soma Neno la Mungu. Katika tovuti hii Watumishi wa Mungu Mwl. Bwana na Bibi Steven Mwakatwila tunafanya bidii kusoma na kukuonya na kukufundisha juu ya Mungu Yesu Kristo ili upate kuponywa na kuurithi ufalme wa Mbinguni. Ungana nasi katika masomo, vipindi vya redio, makala, katika CD, DVD, VHS na matamasha mbalimbali yanayofanyika kote Tanzania. Fuatilia ratiba ya matamasha na semina ili kujua lini unaweza kuhudhuria upate Neno la Mungu.

Wanafamilia

Hii ni familia inayokua kila siku ya Huduma ya Soma Neno la Mungu, karibu uwe mmoja wetu! Jiunge leo. Kama ilivyo familia ya duniani, kuwa mwana familia wa familia ya Mungu (Familia ya Soma Neno la Mungu) ni upendeleo na uwajibikaji pia.

Ni furaha iliyoje kujua kwamba tunaweza kutegemea hii familia yetu mpya kwa ajili ya upendo, msaada na kuhudumiana! Biblia huita “kujumuika pamoja,” na kwa kawaida maana yake ni kushiriki pamoja na waumini wenzetu furaha na huzuni zetu. Pamoja na kwamba Wakristo wanapaswa kuhudumia wanadamu wote, Biblia husema wazi kwamba lazima tutoe kipaumbele maalum kwa waumini wenzetu: “Kwa hivyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.” (Wagalatia 6:10).

Je, katika uzoefu wako kama mwana familia wa duniani, matumaini yako yamepungua kwa namna ye yote ile? Familia ya kanisa yaweza kuleta uponyaji wa nguvu kadiri mnavyoshiriki kwa uwazi na kuonyeshana upendo usio na masharti ninyi kwa ninyi. Ni muhimu kukumbuka kwamba familia ya kanisani inatokana na watu kama sisi wenyewe, wanadamu wanaokua na wasio wakamilifu. Nyakati fulani familia za aina zote hizo zaweza kutukatisha tamaa. Ndiyo maana lazima siku zote tuelekeze macho yetu kwa Yesu ambaye ndiye tu Mfano wetu halisi.

Familia ya Soma Neno la Mungu inakuhitaji. Fanya sehemu yako katika kushiriki upendo wako, muda wako, talanta zako, na vyanzo vyako vya kifedha pamoja na ndugu na jamaa zako katika Kristo.

Salamu za Mwezi

Kila mwezi Watumishi wa Mungu Mwl. Bwana na Bibi Steven Mwakatwila tunakuletea salamu kwako wewe msomaji ili kukupa ujumbe maalumu katika mtiririko mzuri juu ya mambo muhimu ambayo unapaswa huyafahamu. Kila mwezi unapata mfululizo wa mada maalumu iliyochaguliwa ambayo itajibu maswali mengi ambayo huenda umekuwa ukijiuliza kwa muda mrefu ama unaweza kupata maarifa zaidi kwa kujifunza mengi yaliyomo katika salamu hizo.

Ungana nasi sasa kwa kufuatilia salamu hizi kila mwanzo wa mwezi ili kupata maarifa zaidi. Unaweza pia kutupa mtazamo wako juu ya salamu hizo na nini ungependa kifundishwe kwenye mada ya salamu za mwezi itakayofuatia. Karibu sana na Mungu akubariki! Tembelea ukurasa wa Salamu za Mwezi kusoma!

Ilikuwaje hata kumtumikia Mungu?

Baada ya kumpokea Bwana Yesu Kristo, Mungu aliweka ndani yangu wito wa kumtumikia, na ninamshukuru kwa kunipa ofisi ya Ualimu ndani yangu, na kuniambia wazi kuwa anataka nifundishe watoto wake na watu wake, utumishi ulioanza rasmi mwaka 2006 baada ya kupitishwa na Bwana katika maandalio mbalimbali, ya kiutumishi. Mwaka huo nikiwa Lilongwe Malawi kikazi, ndipo Bwana aliposema nami kuwa “Sasa rudi Tanzania kwa kazi ninayotaka uifanye……”

Soma zaidi...

Jiunge nasi leo

Pata habari kutuhusu

Error: Contact form not found.