Salamu – Agosti, 2021

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.. ni imani yangu wewe ni mzima…nikupe pole na magumu yoote uliyokutana nayo naamini Mungu atakupigania na kukuvusha salama katika pito unalopitia   Nikukaribishe kwenye kona hii ya salamu za mwezi, naamini umekua ukilifuatilia somo vizuri.

Kumbuka tunasomo lenye kichwa

VIPAO MBELE VYA MAOMBI YAKO WEKA BIDII YA KUOMBEA MASIKIO YAKO.

Katika salamu zilizopita tulijifunza eneo la maana mbili za kusikia na tuliishia katika kile kipengere cha MFANO WA ISHARA NI SAUTI YA MUNGU UKIWA NA SIKIO LA KUSIKIA UTAISIKIA

Hebu tusogee mbele kidogo hapo.  

MAOMBI YA ELIYA KUTAKA ISHARA ALITAKA WATU WAISIKIE SAUTI YA MUNGU

Unaposoma maandiko unaona nabii Eliya alitaka ishara kwa Mungu ili wana wa Israeli wamsikie Mungu.  

Angalia mistari hii. ”Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu.“ (1Wafalme 18:36-39).

Mungu alijithibitisha kuwa yeye ndiye BWANA na kumdhibitisha Eliya kuwa ni mtumishi wake kwa kutumia ishara hiyo. Ishara hiyo ilibeba sauti ya Mungu kwa wana wa Israeli kabisaa.

Na waliisikia kwa kuanguka kifudifudi na wakasema wazi kuwa BWANA NDIYE MUNGU.  

ISHARA NI SEHEMU YA SAUTI YA MUNGU UKIWA NA SIKIO YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU UTAISIKIA SAUTI YAKE KWA UPITIA ISHARA.E: ISHARA YA MOYO KUWAKA AU MOTO MOYONI

Moja ya ishara ambayo imebeba sauti ya Mungu na ukiwa na sikio la kusikia utaisikia sauti hiyo ni hii ya moyo kuwaka unaposikia neno,wazo nk.   Mungu anaweza kusema na wewe kwa kutumia sauti hiyo ya moyo kuwa..yasni unajisikia huko ndani kama moto hivi.

Angalia mistari hii uone hiki ninachokuambia. “Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? Wakaondoka saa ile ile, wakarejea Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa pamoja nao, wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni.” (Luka 24:30-34)

Hao ndugu walisikia sauti ikisema nao na walijikuta waisikiapo hiyo sauti mioyo yao ikiwakandani yao, hawakujua kuwa kuwaka kwa mioyo yao ilikua ni ishara kuwa huyo asemaye maneno hayo ni Bwana Yesu Kristo.   Wao hawakumtambua, kisa hawakuijua ishara hiyo kuwa ni kuwapa taarifa kuwa Mungu alikua anasema nao..wao walijikaza kimyaaa mpaka Bwana Yesu Kristo alipoondoka mbele yao kiajabu ndiyo wakagundua kuwa aliyekua anasema nao ni Bwana Yesu Kristo.

Cha kufurahisha ni kuwa kumbe katika kusikia kwao kuliambatana na mioyo ya watu hao kuwaka. Sikia unapopokea wazo,au neno na ukajikuta moyo wako unawaka ebu tulia lisikilize vema hilo wazo inawezekana kabisa ni Mungu anasema na wewe ili uchukue hatua maalumu.

Unapomsikia mtu akisema na wewe neno la masna na ukajikuta unaona moyo wako unawaka fahamu hiyo sauti si ya mtu huyo tu. Mungu ndiye asemaye na wewe kwa kumtumia mtu huyo.

Angalia mfano wa mistari hii “Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.” (Yeremia 20:9).

Hiyo ni ishara ya kuwa kunajambo ambalo Mungu anataka ulifanye na hujamsikia na hufanyi atakacho.

E: KUKOSA AMANI NA FURAHA MOYONI

Ishara hiyo ya kukosa anani na furaha ni sauti inayokupelekea wewe kwenye nini Mungu anasema na wewe ukifanye   Sauti hiyo ya Mungu itakukosesha amani mpaka ukifanye hicho atakacho Mungu… sehemu nyingine Biblia inasema ni amani ya Mungu ikusaidio mwanadamu kuisikia sauti ya Mungu yaani kukifanya kile Mungu anataka.

Angalia mistari hii. “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.” (Wakolosai 3:15)

Ukienda kwa Mungu na ukatafuta mwongozo ambao wewe unatakiwa ufanye maamuzi fahamu amani hiyo ndiyo itakua sauti ya Mungu kukuongoza kuwa uamuzi uliouchukua ni mzuri, utajikuta una amani, ikiwa ni uamuzi mbaya fahamu utakosa amani. Usijilazimishe kukifanya kitu ambacho huna amani kukifanya.

Sikia ukipanga kufanya jambo na ukamuomba Mungu akuongoze fahamu kama si mapenzi yake atakuletea huo moto unaokosesha amani moyoni.

Ishara hiyo inabeba sauti ya Mungu ya mwongozo, ukiona tu amani imetoweka baada ya kufanya maamuzi yako fahamu Mungu anakua na neno na wewe isikie hiyo sauti usifanye au fanya kile unachoongozwa na ishara hiyo.

Angalia mistari hii. “Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi. ”(Isaya 55:12)

Amani na furaha moyoni ndiyo ishara kuu ya muongozo wa sauti ya Mungu kwa wanadamu.

Na amini umenielewa.

Mungu akubariki sana. Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.