Salamu – Februali, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ninakukaribisha sana katika kona hii ya salamu za mwezi. Huu ni mwezi wa pili, katika mwezi uliopita tumekua na semina nyingi ambazo kwa kweli tumemuona Mungu.

Ebu tuanze kuziangalia salamu za mwezi..kumbuka tuna salamu zenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Katika salamu zilizopita tuliona maeneo matatu ambayo yanaweza kuugua na yakahitaji kuponywa.

Nayo ni roho,nafsi na mwili. Na somo hili tunaangalia uponyaji wa nafsi au moyo

SHIDA IPO HAPA WATU WENGI HAWANA HAJA YA KUPONYWA NAFSINI AU MOYONI KWASABABU WANAJIONA NI WAZIMA KUMBE NI WAGONJWA NAFSINI

Biblia inasema hivi “ Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.(LUKA 9:11)

Ukiisoma mistari hiyo unaona kuwa Bwana Yesu Kristo huponya..lakini huwaponya wale wenye haja ya kuponywa. Sasa fikiri hujui kuwa nafsi yako inaweza kuugua utajikuta huwezi kuwa na haja ya kuponywa.

SABABU ZINAZO WEZA KUSABABISHA JERAHA NAFSINI

1: SABABU YA KWANZA NI MAUDHI

Watu wengi hawajui kuwa nafsi inaweza kujeruhiwa na kuwa dhaifu kwasababu ya maudhi ambayo mtu anakutana nayo kila siku.

Sikia maudhi hukaa moyoni au nafsini. Huko ndani ya nafsi kuna hisia..hisia ndiyo inatunza maudhi ,uchungu au huzuni.

Watu wengi hisia zao zimebeba uchungu, unajua ni kwanini? Ni kwasababu ya maudhi mbalimbali wanayokutana nayo tena tokea watoto wadogo.

Biblia inasema maudhi na huzuni vinakaa ndani ya nafsi, angalia mistari hii.

“Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. (Mwanzo 45:5)

Yusufu alijua kuwa ndani ya nafsi kuna kaa huzuni na maudhi, ndiyo maana akawaambia nduguze wasiwe moyoni na udhi wala huzuni.

Biblia inatufundisha kuwa moyo unaweza kuvunjika na kupata jeraha Angalia mistari hii. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;

Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;

Wala fedheha yake (Mithali 6:32-33).

Nataka nikuonyeshe hapo kuwa nafsi inaweza kupata jeraha..yaani kuumizwa. Na moja ya jambo linaloumiza au kujeruhi nafsi ni udhi au udhia furani ambao ndani yake hubeba uchungu na huzuni na kilio na kuomboleza na machozi

Angalia mistari hii uone “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu;

Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu. “(Ayubu 7:11 )

Ukiipitia mistari hiyo unaona ndani ya nafsi kunaweza kukaa uchungu. Sasa uchungu au huzuni ikikaa moyoni inatengeneza ugonjwa mkubwa kwenye moyo au nafsi ya mtu.

Kumbuka tuliko toka ndani ya nafsi kuna akili, hisia na utashi. Katika vitu hivyo vitatu fahamu ndiyo kumebebwa ufahamu,kujua,kufurahi,upendo,kukumbuka, kuelewa, kubuni,kunia,kukusudia,kuwaza,kudhamiria, kufikiri, kutafakali, nk.

Uchungu ukikaa moyoni nafsi ya huyo mtu itakutana na maradhi mengi mnoo.mfano mtu mwenye majonzi moyoni yatokanayo na uchungu, hawezi, kuwaza,kunia,kupanga vema, kukumbuka nk .

Mtu wa namna hiyo hawezi kujiamini na kutenda jambo lolote kisa akili utashi na hisia zake vimeugua kutokana na maudhi.

Mtu akitendewa jambo la kumuumiza ,usishangae hawezi,kula,kulala,kusoma,kusema nk huo ni ugonjwa. Wagonjwa wanao ugua magonjwa mengine wengi huwa na dalili. kama hizo.

Mtu ambaye hawezi kula,kulala,kusema,kuwaza vema huwa tunamwita mgonjwa… sasa angalia watu wengi mnoo wanadalili hizo zoote..wakienda kupimwa hispitali wataambiwa hawaumwi,lakini hawawezi kula,kulala,kuwaza,na utawaona wakikonda…lakini wameambiwa ni wazima

Ukikutana na hali hiyo ebu jiangalie huenda wewe ni mgonjwa hukoo nafsini, unahitaji uponyaji. Roho Mtakatifu yupo tayari kukuponya anakusubiri wewe ujitambue kuwa ni mgonjwa na unahitaji uponyaji.

Naamini umenielewa.. tuonane mwezi ujao katika kona hii mwezi ujao.

Barikiwa sana

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.