Salamu – Aprili, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Naamini unandelea vema. Na ni imani yetu kuwa mwezi uliopita ulibarikiwa na salamu zetu za mwezi tulizo kutumia. Mungu akubariki pia kwa nafasi unayoitoa kwa kusoma na hata kwa kutuombea.

Nimekuletea salamu za mwezi wa nne, naomba zipokee! Kumbuka tuna salamu zenye kichwa “WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO”

Katika salamu zilizopita tuliangalia sababu ya pili inayoweza kuwa ndiyo kiini cha kuijeruhi nafsi yako. Nayo ilikua ni Dhambi.

Na tukajifunza dhambi ya uzinzi namna inavyoweza kuijeruhi nafsi au moyo wa mwanadamu.

Hebu tuangalie dhambi ya pili. Ambayo inaweza kuijeruhi nafsi ya mtu nayo ni: –

Biblia inasema hivi “Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu” (Mithali 26:28)

Ukiisoma mistari hiyo unaona uongo una mdhara mengi sana. Moja ya madhara ya uongo ni hii ya kumjeruhi mtu aliyesemewa uongo, na madhara mengine ya uongo ni kumtengenezea mtu huyo asemaye uongo chuki au uharibifu wa moyo wake.

Chuki hukaa moyoni; neno chuki maana yake hasa ni tendo la kutokuwa na upendo na mtu, watu, vitu nk. Kwa lugha nyingine chuki huitwa kijicho.

Mtu wa sifa hii mara nyingi hujikuta katika ugomvi na watu na uadui na watu. Mtu wa namna hii hawezi kuwa na amani na furaha moyoni hata siku moja.

Mtu yoyote amsemeaye mtu uongo; fahamu muda huo huo kinamchomtokea huko moyoni mwake ni jeraha la linalomuumiza moyoni mwake na kujikuta akianza kumchukia mtu huyo aliyesemewa uongo.

Ndani ya uongo kuna uzushi, masengenyo, shutuma za uongo nk. Wewe wafuatilie watu waongo. Utashsngaa ghafla wanapoteza marafiki, ndugu nk.

Sikia; ukiona mtu hakupendi na unatafuta sababu za yeye kukuchukia huzioni. Fahamu mtu huyo anajeraha moyoni mwake. Na jeraha hilo chanzo chake huenda ameambiwa maneno ya uongo dhidi yako au yeye mwenyewe amekusemea maneno ya uongo.

Mtu wa namna hiyo akikuona au kusikia jina lako hawezi kuwa na amani moyoni kabisa. Kadri siku zinavyozidi kwenda utaanza kuiona chuki yake wazi wazi.

Ukiona hivyo mtu wa namna hiyo anahitaji msaada, msaada mkubwa ni maombi, wala si kuzungumza naye tu.

Ni ngumu mno ukizungumza naye akuambie chanzo cha chuki yake kwako, hawezi sema alikusemea uongo mahali fulani. Wewe muombe toba na moyo wa toba, siku akitubu tu… utashangaa upendo unarudi.

Watu wengi hawajui kuwa unapomsemea uongo mkeo au mumeo, mkweo au shemeji kitakachotokea kwako ni tabia mbaya ya kumchukia.

Sasa sikia; ili uilinde nafsi yako jifunze kutokuwa muongo. Acha hiyo tabia, tubu, tengeneza… kama uliwaambia watu fulani habari za uongo kumhusu mtu furani, waambie ndugu zangu siku ile sikusema ukweli kumhusu mtu fulani.

Utashangaa utaanza kuiponya nafsi yako, jilinde na dhambi hii ya uongo. Tubu, iache, jifunze kupenda kusema ukweli usiupende uongo wala kuutenda.

Mungu akubariki sana. Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.