Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ni mwezi mwingine Mungu ametupa. Mwezi uliopita tumekua na semina huko Makete.
Tulikua na semina ya wanawake. Kila mwaka huduma hii aliyotupa Mungu tunaandaa semina maalumu kwa sjili ya wanawake. Na tunakuwa na semina mikoa mbalimbali. Mwaka huu tukawa na semina mkoa wa Njombe huko Makete. Ilikua semina nzuri sana.
Pia tulikua na semina jijini Mbeya kwenye kanisa la Kkkt Forest. Ilikua semina nxuri sana.
Leo nimekuletea salamu za mwezi wa tano.
Naamini tunaendelea na salamu zenye kichwa
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)
Hebu tusogee mbele kidogo
KUNA UTOFAUTI WA NENO HUDUMA NA KARAMA ZA ROHO
Angalia mistari hii. Biblia inasema hivi “ Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.” (1Kor 12:4-7)
Moja ya jambo muhimu sana ambalo tunatakiwa tulijue ni hili la kujua kuhusu utofauti wa huduma na karama za roho. Usipo lijua jambo hili ni rahisi sana la kutokuona umuhimu wa wewe kuzitaka karama za roho. Na usipolijua jambo hili ni rahisi sana ukajianzishia huduma ambazo Mungu hajakutuma uzifanye.
Sikia, unaposikia kuhusu karama za roho fahamu karama za roho si huduma. ila karama za roho zinaweza kukuwezesha wewe katika huduma yako. Pia, lazima ufahamu kuwa unaweza usiwe na huduma yoyote lakini ukawa na karama za roho AINA ZA HUDUMA
Tunaposoma Biblia tunajifunza kuwa Mungu ameweka huduma au ofisi za kiutumishi zipo tano. Nazo ni hizi. “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”(Waefeso 4:11-13)
Ofisi za kihuduma zipo tano nazo ni mchungaji, mtume, mwalimu,nabii na mwinjilisti. Hizi ndiyo tunaita huduma. Kwa mujibu wa mistari hii utajifunza kuwa Mungu anaweza kumuita mtu akampa ofisi au huduma ya uchungaji nk na asimpe karama za roho. Na pia unaweza ukawa mtu haujaitwa kuwa mwalimu,au mchungaji,au nabii, au mtume au nabii lakini ukawa huna karama za roho.
Ngoja nikupe mfano. Mungu alimwita Samweli au Yohana Mbatizaji au Yeremia hawa ni manabii kabisa lakini hawakuwa na karama za roho kama matendo ya miujiza au karama za kuponya. Naamini sasa umeanza kuona umuhimu wa kuzijua habari za karama za kiroho na kuzitaka.
Sikia, mtumishi unaweza kabisa ukawa ni nabii au mchungaji nk ukawa huna kabisa karama za roho yoyote. Kama huna Mungu anakupa wewe mwenyewe nafasi ya kuzitaka karama za roho. Pia unaweza ukawa wewe huna huduma yoyote yaani wewe si mwinjilisti au ni mtume nk lakini ukawa na karama za roho. Naamini umenielewa..Tuonane katika eneo hili la salamu za kila mwezi Mungu akubariki sana.
Naamini umeelewa. Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi.
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.