Salamu – Julai, 2024

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.Ninamshukuru Mungu ambaye ametupa mwezi huu wa saba.

Mwezi huu tumekua na semina tatu, tumekua na semina Chunya,Chimala na Ubaruku.

Semina hizi zilikua nzuri sana.Ndani ya mwezi huu wa saba tunatarajia kuwa na mkutano mkubwa wa semina ya watumishi kutokea nchi mbalimbali.Tutafanyia huko Arusha tuombee.

Nimekuletea salamu za mwezi. Hebu tusogee mbele kumbuka tuna salamu zenye kichwa:

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)

Hebu tusogee mbele

USIUZE KARAMA ZA ROHO

Moja ya jambo unalotakiwa ujilinde nalo sana ukiwa umepewa karama za roho ni hili hakikisha hauiuzi karama hiyo aliyokupa Mungu.

Sikia neno karama za roho maana yake ni zawadi. Neno zawadi tunapewa bure. Zawadi hainunuliwi, ila unaweza kuomba upewe zawadi na huyo atoae zawadi hufanya maamuzi ampe au asimpe.

Sasa sikia, unapopewa karama za roho Mungu ametupa sisi maagizo tusiziuze hizo karama.Angalia mistari hii “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.“ (Mathayo 10:8).

Ukiisoma mistari hiyo tunajifunza kuwa tunapopewa karama za roho za kuponya,kufanya matendo ya miujiza nk tunatakiwa tusitozi kitu chochote. Sikia unajua leo hii ni rahisi mnoo ukapewa karama za roho na ukaanza kuzitumia hizo karama za roho kibiashara.

Haujawahi kuona au kusikia ili upewe huduma ya kuponywa au kupokea unabii utoe kitu fulani?

Sasa sikia kwa habari za karama za roho tusikose kujua. Moja jambo la kujua ni hili hakikisha hauuzi karama hizo za roho.

Mungu ameagiza kututunza. Mungu yeye akuinulie watu wa kukutunza, si wewe ujipangie leo kiwango cha karama za roho. Sikia, ukianza kufanya hivyo, utapewa fedha au mali au magari mengi tu.

Lakini si siku nyingi utapoteza karama hiyo na huko mbele utakutana na hukumu mbaya sana. Hukumu mbaya ni hii ya Bwana Yesu Kristo akwambie hakujui. Unafikiri Mungu akisema sikujui atakupeleka wapi kama si jehanamu?

KUNA MADHARA MAKUBWA UNAWEZA KUKUTANA NAYO UKITAFUTA KUUZA HUDUMA

Unaposoma Biblia unaona kuwa Gehazi ni mmoja wa watumishi wa Mungu akimtumikia Mungu kama msaidizi wa mtumishi Elisha.

Gehazi alikutana na mabaya alipotafuta fedha baada ya huduma kutendeka. Angalia mistari hii. “Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama BWANA aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake. Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake. Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi? Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji. Ukiona kuna mahali umekosea nakushauri tubu. Geuka acha kufanya dhambi hiyo. Jipange vema ndipo Mungu atakuoenda na kukulinda wewe na huduma na hiyo karama za roho alizokupa.” (2Wafalme 5:20-27)

Ukiisoma mistari hii utajifunza kuhusu madhara ya kuuza huduma au karama. Elisha aligundua kuwa Naamani analengo la kuiuza huduma ambayo Mungu amefanya kwa kutumia Elisha.  Elisha hakuwa tayari kuchukua kitu chochote kwa sababu huo haukuwa muda wa kuchukua hivyo vitu.

Gehazi yeye alikua tayari kupokea hiyo zawadi ambayo ndani yake ilikua inauza huduma. Gehazi alikuwa tayari kuchukua kitu kwasababu ya huduma iliyofanywa na Elisha.

Kilichomtokea ni kupokea ukoma. Sikia, ukifanya huduma yoyote ya Mungu ambayo imebeba karama za roho usitumie karama hizo za rohoni kuuza hiyo huduma. Sikia Mungu anaweza kukutunza kwanjia nyingi,lakini si kwa mtindo huu wa kuuza huduma,yaani kutumika karama za roho kujipatia fedha au utukufu nk.

Ukiona kuna mahali umekosea katika jambo hili fanya toba. tubu. geuka uache tabia hii.

Naamini umeelewa. Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.