Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Nimekuletea salamu ya mwezi wa tisa. katika mwezi huu tunamshukuru Mungu sana kwakutulinda nakutupigania
Mwezi uliopita tulikua na semina kubwa ya watumishi yaani maaskofu na wachungaji. Ilikuas emina nzuri sana.
Hebu tuanze kuzipokea salamu za Mwezi huu wa tisa. Kumbuka tuna salamu zenye kichwa
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)
AINA MBILI YA NENO LA MUNGU
Mungu ana sema na watu. shida kubwa hatujui njia ambazo Mungu anaweza kuzitumia kusema na watu. Hebu tuzitazame hizo njia mbili
1. Neno lililooandikwa (Biblia). Biblia ni neno la Mungu, humo ndani kuna maagizo ambayo Mungu ametupatia tukiwa hapa duniani.Hili ni neno ambalo kila mtu kapewa.ukilisoma hilo neno humo ndani ndiyo utamkuta Bwana Yesu Kristo na ukafanywa uwe Mkristo.
Kwa lugha nzuri ni hivi Kitabu hiki Mungu amekileta kwa watu wote.ni maamuzi ya mtu kukisoma na kukiamini na kukiweka kwenye matendo.neno hili lipo hai kabisaa na limepimwa mara saba kwa moto. “Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.”(Zaburi 12:6)
2. Neno la kutoka kwa Mungu moja kwa moja kwenye ulimwengu wa roho.(unabii)
Sikia Mungu yupo hai.hafi. alikuwepi yupo atakuwepo. Sikia Mungu alisema anasema na atasema.
Mungu anaishi milele kama alitupa maneno yake yaliyoandikwa fahamu hata leo hii anaweza kusema neno
Angalia mfano huu. msikilize asemavyo. “BWANA, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni. (Isaya 45:11).
Kwa mujibu wa mistari hii Mungu anatupa ufahamu kuwa anaweza kukupasha habari ya mambo mbalimbali kwa ajili ya sasa kesho nk.
Usifikiri atakacho kukupasha habari mengine yapo ndani ya Biblia.mfano unatafuta kwa Mungu maagizo au maelekezo au ushauri wa je? Uende shule ukasome huko au usiende kusoma. Mungu atakupa neno hilo mojakwa moja kutokea katika ulimwengu wa roho.
MUNGU ANAWEZA KUSEMA NA MTU MOJA KWA MOJA HATA KAMA HAMJUI MUNGU
Sikia Mungu anaweza kusema na mtu yoyote yule. Unaweza ukawa umemwamini na ukamjuaau haujamjua na humwamini.
Mfano Mungu alizungumza na Farao “Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.” ( Mwanzo 41:25)
Mfalme Farao alikua hamjui hamwamini Mungu.
Farao alikuaa ana abudu miungu mingine. Mungu hakulijari jambo hilo wala halikumzuia alienda na kusema naye moja kwa moja kutokea kwenye ulimwengu wa roho.
Kwa lugha nzuri Farao alipewa unabii.
Bahati nzuri alikuwepo Yusufu anaye mjua Mungu aketiye mbinguni juu sana. Yusufu alijua kuwa Mungu ndiye aliyesema naye na alikua anampa maelekezo yanayohusu miaka kumi na nnekwa ajili ya nchi yake.
Nilichotaka nikutie nguvu ni hiki. Mungu anaweza kusema nawewe kabisaa.Akakupa maelekezo yanayohusu maisha yako au maisha ya watu wengine nk.
Bahati mbaya watu wengi hawajui kuwa Mungu anaweza kusema nao na kuwapa taarifa nyibgi tu zinazowahusu wao wenyewe au watu wengine au kwa ajili ya kanisa au huduma au kwa ajili ya nchi au dunia.
Mungu yupo tayari kukupasha wewe habari ya mambo yatakayokuja nk. kiukweli Mungu anapokupa karamaya unabii fahamu Mungu atakupa taarifa nyingi tu.
Ili ujue namna ya wewe au nduguyo nk wafanye ninj au kama ni jambo gumu ili kumwomba Mungu aliondoe hilo jambo baya nk.
Naamini umeelewa.Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.