Salamu – Octoba, 2024

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Karibu tena kwenye kona hii ya salamu za mwezi. Tunamshukjru Mungu. ametupa mwezi wa kumi.

Karibu ili tupokee salamu za mwezi wa kumi.

Kumbuka tuna salamu zenye kichwa.

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)

ROHO MTAKATIFU ANASEMA WAZIWAZI.

Ninapokukuambia kuwa Mungu anaweza kusema na wewe waziwazi fahamu namzungumzia Roho Mtakatifu. Fahamu Mungu ndiye huyo huyo anayeitwa Roho Mtakatifu.

Angalia mistari hii “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” ( Yohana 24:23-24)

Mungu ndiye huyo huyo aitwae Roho Mtakatifu. Sasa sikia Roho Mtakatifu anaweza kusema na mtu au watu kutokea kwenye ulimwengu waroho.

Yaani iko hivi, wewe umepewa roho.kwa kuwa unayo roho fahamu Mungu ambaye ndiye Roho Mtakatifu anaweza kusema wewe.

Mungu anapokupa karama za rohoni maana yake anakupa zawadi rohoni.moja ya zawadi hiyo ni hii ya unabii yaani Roho Mtakatifu kusema waziwazi au muda huu akizungumza na mtu kutoka katika ulimwengu wa roho

Angalia mfano huu. Biblia inasema hivi “12 Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.” ( 1Kor 1:12)

Neno ufunuo maana yake ni MAELEKEZO YA KUTOKA KWA MUNGU KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Mtume Paulo anasema wazi kuwa mafundisho yake hakuyapojea kutoka kwa mwanadamu.Alifundishwa na Roho Mtakatifu

Angalia mfano mwingine Biblia inasema “Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma. Petro akawashukia wale watu, akanena, Mimi ndiye mnayemtafuta. Mmekuja kwa sababu gani?(Mdo 10:19-21)

Kwa mujibu wa mistari hii unajifunza kuwa Roho Mtakatifu alizungumza na Petro moja kwa moja au wazi wazi kutokea kutoka kwenye ulimwengu wa roho.

Angalia mfano mwingine.Biblia inasema hivi “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.4 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.“( MDO 13:1-3)

Kwa mujibu wa mistari hii utajifunza wazi kuwa Roho Mtakatifu anasema au akampa mtu maelekezo moja kwa moja kutokea kwenye ulimwengu wa roho.

Hawa ndugu hawakusonpma kitabu furani.Mungu alisema moja kwa moja muda huo huo na hawa ndugu wakasikia na kuelewa cha nini chakufanya.

Jifunze kujua kuwa Roho Mtakatifu anaweza kusema na mtu.kumbuka Roho Mtakatifu anaweza kukaa ndani yako. Yupo tayari akupe wewe karama za rohoni mija wapo ni hii karama ya unabii.

Anza kuomba kwa Mungu ili uanze kumsikia na kuyaona yale anayoweza kukuonyesha na uka pewa maelekezo.

Sikia usifikiri kwakua una masikio basi wewe unasikia,au kwa kuwa unamacho basi wewe unaona.

Biblia inasema hivi “Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA?Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii.” ( Isaya 42:19-20)

Sikia anza kuomba Mungu akufumbulie macho yako uone na ayazibue masikio yako yasikie na Usikie na uyatii hayo uliyoyasikia

Kwa leo tuishie hapa kwa salamu za mwezi huu wa kumi. Mungu akubariki sana

Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.