Salamu – Novemba, 2024

BwanaYesu Kristo asifiwe. Karibu sana katika eneo hili la salamu za mwezi. Tunamshukuru sana Mungu ametupa mwezi huu wa kumi na moja.

Kabla hatujaendelea Mbele nataka nikupe tasrifa hii. tarehe 28-31/12/2025 Tutakua na kambi ya maombi.Tutafanyia jijini Mbeya kwenye shule ya St Marys Kadege.Tunaanza saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni.

Namna ya kuja ni nauli yako ya kwenda na kuludi,malazi na chakula tutakupa.Karibuni sana mpe taarifa hii na mtu mwingine.

Mwezi huu nimekuletea salamu hizi.

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)

NAMNA YA KUPOKEA UNABII

Kwa ufupi tuone namna ya kupokea unabii au ni njia zipi Mungu anaweza kusema na mwanadamu.

Ukisoma Biblia utaona Mungu ana njia nyingi sana anazoweza kuzitumia kuzungumza na mtu au mwanadamu.

Hebu tuanze kuona njia ya kwanza. 1. NDOTO.

Moja ya njia ambayo Mungu anaweza kuzungumza na mtu ni ndoto au maono. unaweza ukawa unataka kujua maana ya neno ndoto au maono ni nini?

MAANA YA NENO NDOTO AU MAONO.NI MAELEKEZO AU NI WAZO LA MUNGU KUTOKA ULIMWENGU WA ROHO UJUMBE UNAOKUJA KAMA PICHA UNAWEZA BEBA HATA SAUTI.

Sikia maelekezo hayo yanakuja kwa mtu kwa kutumia USINGIZI AU WAZIWAZI.Kwalugha nzuri niseme kuwa ndoto au maono ndiyo mlango ambao Mungu huutumia kuzungumza na watu.

Angalia mistari hii uone. “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,” (Ayubu 33:14-16).

Ukiisoma mistari hiyo unajifunzakuwa Mungu anasema.na anaitumia hiyo njia ya ndoto na maono ili azungumzie na mwanadamu .

Unapomuomba mungu akupe karama ya unabii fahamu Mungu atakupatia wewe nafasi ya kuota ndoto na kukuonyesha mambo ili akupe wewe huo unabii yaani neno lililotoka kwenye ulimwengu wa roho.

MANABII WANAPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA MUNGU KWA KUTUMIA NDOTO AU MAONO YAANI MANABII HUPOKEA UNABII KWA KUTUMIA NDOTO AU MAONO.

Bahati mbaya watu wengi wanapowasikia manabii.Wanafikiri kuwa wao wanaona waziwazi tu.au wanasikia sauti ya Mungu tu.Sikia manabii huota ndoto au maono.maana yake wanalala usingizi na Mungu huwapa ndoto.

Biblia inasema hivi “BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?” (Hesabu 12:5-8)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona kuwa manabii ili wapokee unabii wanaota ndoto.Sikia hata kwako wewe uliyepewa karama ya unabii fahamu ili Mungu akupe unabii ataitumia njia hiyo hiyo ya ndoto na maono.

Biblia inasema hivi. “Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.”(Zaburi 89:19-20)

Fahamu kuwa watakatifu wa Mungu ili wazungumze na Mungu njia mojawapo ambayo Mungu anaitumia ni hii ya ndoto au maono.

Hata unaposikia Mungu alizungumza na Ibrahimu fahamu njia aliyoitumia Mungu kuzungumza naye alitumia ndoto.

“Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.4 Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.” (Mwanzo 15:1-4)

Ibrahimu alikuwa nabii alipokea unabii kwa kutumia ndoto.na maono. Biblia inasema hivi “Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse. Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.Abimeleki akaamka asubuhi na mapema, akawaita watumwa wake wote, akawaambia maneno hayo yote masikioni mwao, nao watu hao wakaogopa sana.Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.“(Mwanzo 20:6-9).

Angalia mfano Mungu alizungumza na Yusufu kwa kutumia ndoto.Mungu alimtaarifu Yusufu na ndugu zake kuhusu maisha yajayo.

Biblia inasema hivi “Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota.Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.”( Mwanzo 37:5-11).

Mungu alitumia ndoto ili kumtafsiria na kumtaarifu Daniel kuhusu ndoto ya mfalme . “Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni.” (Daniel 2:16-19)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unajifunza kuwa Mungu alimjulisha Daniel siri hiyo iliyokua imefichika mnoo.Wewe kasusome mlango huo wote utajua kuhusu habari hizo. Danieli aliomba kwa Mungu, akapewa jibu kwa ndoto .lile jibu ndiyo unabii. kwa hiyo ndoto ndiyo mlango wa mazungumzo kati yako na Mungu.

Ngoja nikupe Mfano mwingine. Paulo alikua anaenda mahali kwenye huduma.Ili Mungu ampe maelekezo au muongozo, aliutumia mlango huo huo wa ndoto na maono. Angalia mistari hii ”Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,wakapita Misia wakatelemkia Troa.Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.“ (Mdo 16:6-10).

Ukiisoma mistari hiyo unaona wazi kuwa Roho Mtakatifu alimuongoza Paulo aende wapi.na njia ya kumuongoza Roho Mtakatifu alitumia maono usiku kitandani. Akaona picha ambayo ilimpatia maarifa ya nini afanye.Sikia Mtume Paulo alipoona hilo ono alijua kabisa kuwa Mungu anamwambia nini, hakupata shida akakifanya kile alichoambiwa.

Bahati mbaya watu wengi wakiota ndoto huwa wanazidharau sana.kumbe wanapishana na maelekezo kutoka kwa Mungu. Usizidharau hizo ndoto.zitafakari, na usiste kuziombea na kuziweka kwenye matendo.

Naamini umenielewa. Tuonane katika eneo katika salamu zijazo.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.