Salamu – Januari, 2025

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Karibu sana katika eneo hili la salamu za mwezi, huu ni ni mwezi wa kwanza Tunamshukuru sana Mungu ametupa mwezi huu wa kwanza ukiwa ndio mwezi wa mwanzo wa mwaka huu wa 2025.

Tunamshukuru Mungu ametulinda mnoo katika mwaka uliopita…Tulikua na kambi la maombi zuri sana. Naamini kila aliyehudhuria maombi hayo kuna jambo kubwa Mungu amefanya naye.

Tunapo uanza mwaka mpya tutakua na salamu za mwanzo wa mwaka huu , salamu tutakazo kuwa nazo ni zile zile tuliloanza nazo mwaka jana.Tutaendelea na mfurulizo wa somo hili lenye kichwa

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA

Hebu tuendelee kujifunza.

ILI MACHO YAKO YA NDANI YAPATE KUWA VIZURI YAANI ILI MUNGU ASEME NA WEWE VEMA AU KATIKA HIZO NDOTO LAZIMA UWE MWAMINIFU.

Angalia mistari hii. “BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?” (Hesabu 12:5-8)

Sikia watu wengi wanaomba kwa Mungu awape karama hii ya unabii, na wengine zamani walipewa karama hii ya unabii na sasa imepotea na hawajui ni nini kimetokea.

Sikia moja ya sababu inayoweza kumfanya Mungu asikupe au akaiondoa karama hii kwako au usipate nafasi ya kuona maono waziwazi ukawa unaota ndoto tu tena za mafumbo mafumbo ni hili la kutokuwa mwaminifu.

Nini maana ya neno uaminifu? Uaminifu maana yake ni hii.

  1. KULIFANYIA KWA USAHIHI KILE ULICHOPEWA UKIFANYE 2. KUKISIMAMIA ULICHOPEWA UKITUNZE BILA KUKIIBA AU KUKITUMIA BILA RIDHAA. 3. KUTOKUFANYA KINYUME NA AGIZO ULILOPEWA

Sasa sikia, kwa mujibu wa mistari hiyo utaona wazi kuwa ili Zmungu azungumze na mtu waziwazi ni hili la kuwa mwaminifu.

Fikiria kidogo kuna ndoto au maono ambayo ndani yake ulipewa moja ulitunze jambo hilo kwa kutokumshirikisha kila mtu, pili uliweke kwenye matendo jambo hilo uliloonyeshwa katika ndoto.. Au kumshukuru Mungu hicho ulichokiona hata kama haujakielewa.

Sasa jiulize wewe umelitunza jambo hilo?kama haujayatendea kazi mambo kama hayo fahamu wewe si mwaminifu.

Sikia Mungu amekupa maagizo mengi sana je! Wewe unayafanyia kazi hayo uliyoagizwa? Ngoja nikupe mfano amekupa agizo la kutubu je! Wewe ni mtu wa toba?

Mbona unaficha dhambi ulizozifanya? Ukiwa ni mtu wa namna hiyo fahamu wewe si mwaminifu.. Ndiyo maana usishangae huoni maono ingawa zamani ulikua unaona sana.

Jifunze kuwa mwaminifu kwa Mungu na kwa watu wengine.

Mungu akubariki tuonane tena katika salamu za mwezi wa kwanza.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo.

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.