Bwana Yesu Kristo asifiwe, tunamshukuru Mungu ametupa mwezi huu wa tatu.
Hebu tuanze kuangalia salamu ya mwezi wa tatu.
Kumbuka tunaendelea na salamu zenye kichwa.
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA
Hebu tuendelee mbele kidogo.
3: ILI UONE MAONO NA NDOTO JIFUNZE KUTOA SADAKA VEMA.
Angalia mistari hii “BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea.” (Mwanzo12:7).
Kwa mujibu wa mistari hii unajifunza kuwa Ibrahimu aliona maono..alitokewa na Mungu, na Mungu alimwambia kuhusu maisha yake yajayo. Ibrahimu aliloona hilo ono alitengeneza madhabahu. Sikia kazi ya madhabahu moja wapo ni kupokea sadaka.
Kwa maana nzuri Ibrahimu alipoona hayo maono alimtolea Mungu sadaka. Angalia na mistari hii “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.” (Mdo 10:1-4)
Kwa mujibu wa mistari hiyo tunaona wazi kuwa sababu yaKornelio kuletewa ono waziwazi la kukutana na malaika chanzo chake ni utoaji wa sadaka. Kwa hiyo ili leo hii upewe karama hii ya unabii yaani kupokea maelekezo moja kwa moja kutoka ulimwengu wa roho unatakiwa ujifunze uwe na tabia ya utoaji wa sadaka mbalimbali kwa Mungu. Utoaji wako unakufungulia wewe mlango wa kupokea sauti au maelekezo kutoka kwa Mungu..
4: JIFUNZE KUOMBA ILI
a) Mungu akutie nguvu ili uone au upokee maelekezo.
Angalia mistari hii”siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;” (Waefeso 1:16-19)
Ili leo hii upewe roho ya ufunuo na macho ya ndani yaone fahamu unatakiwa uombe.. Mtume Paulo aliomba ili watu hao wapewe mambo hayo. Sikia kinacho sababisha hawa watu wapewe macho yanayo ona na kupewa mafunuo ni nguvu za Mungu. Tumezoea kuita upako. Sikia, ili Mungu aseme na watu kinacho msaidia huyo mtu aone au asikie kutoka katika ulimwengu wa roho ni upako au nguvu za Mungu.
Biblia inasema hivi “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:13)
Sikia; kwa mujibu wa mistari hiyo ili ufanye jambo lolote fahamu ni nguvu za Mungu zinazokukuwezesha ili ukifanye hicho. Kwa hiyo hata kusikia mambo ya rohoni kinachoweza kukuwezesha ni nguvu za Mungu. Ukiona mtu zamani alikua anaona au anaota ndoto zilizonyooka na ghafra zimepotea ebu angalia nguvu za Mungu ndani yako zimekaakaaje.
Jifunze kuomba Mungu akujaze nguvu za kukuwezesha kusikia maelekezo kutoka kwa Mungu
b) Ombea masikio yako na macho ya ndani yapate kuona na masikio yapate kuzibuka.
Angalia “Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” (Ufu 3:18)
Jifunze kumuomba Bwana Yesu Kristo ashughulike na macho yako yapate kuona. Sikia unaweza kufikiri unaona..kumbe bado huoni kabisaa..yaani macho yako ynatakiwa yafumbuliwe. Bwana Yesu Kristo anao uwezo wa kuyafumbua macho yako uone
Naamini umenielewa
Mungu akipenda Tuonane tena mwezi ujao katika kona hii ya salamu za mwezi.
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.