Salamu – Aprili, 2025

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Ni siku njema tumepewa na Mungu. Tumepewa tena mwezi huu wa nne. Mwezi uliopita tumekua na semina KKKT Uyole. Ilikua semina nzuri sana.

Ebu tuanze kuziangalia tena salamu za mwezi wa nne. Kumbuka tuna somo lenye kichwa…

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA

Hebu tuendelee mbele kidogo

2: NJIA YA PILI YA MUNGU ANAVYOWEZA KUTUPATIA UNABI NI KWA KUSEMA KWA SAUTI WAZIWAZI

Sikia Mungu anaweza kusema na mtu kwa kutumia sauti inayoweza kusikika na mtu au kundi.

Na unapoisikia sauti hiyo fahamu huo ni unabii. Maana neno hilo si la mtuni neno litokalo kinywa mwa Mungu moja kwa moja.

Sikia ni watu wachache ambao wanaisikia sauti ya namna hii moja kwa moja..kiukweli watu wengi wanamsikia Mungu kwa kutumia ndoto au maono watu wakiwa wamelala yani wapo rohoni.

Kuna watu si manabii ila wamepewa karama ya unabii.. Angalia mfano huu.. Mtume Paulo yeye si nabii, Neno la Mungu linasema hivi “7 Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.” (1Timotheo 2:7)

Kwa mujibu wa mistari hiyo Mtume Paulo anajitambulisha kuwa yeye ninani, hajajitambulisha kuwa ni nabii.

Sasa sikiliza huyu mtume Paulo alikutana na Mungu na aliona na alimsikia waziwazi akizungumza naye na kumpa maelekezo.

Sikia siku hiyo alipokutana na Bwana Yesu Kristo alikua na watuwengine wengi tu, watu hao waliisikia sauti ya Bwana Yesu Kabisa kutokea mbinguni.

Angalia mistari hii uone. “Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.” (Mdo 9:1-7).

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona wazi kuwa Mungu anaweza kusema na mtu kwa sauti wakati watu haosi manabii. Hao watu waliisikia sauti ila hawakuona kitu chochote, Mtume Paulo aliona ono na kusikia sauti moja kwa moja bila kulala usingizi, kama hao watu walisikia sauti ila hawakuwa wanaota ndoto usingizini.

Hiyo ni njia ya pili ambayo Mungu anaweza kuitumia kumpa mtu unabii.

Naamini umenielewa. Tuonane tenakatika kona hii ya salamu za mwezi

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.