Bwana Yesu Kristo asifiwe.
Ninakukaribisha kwenye eneo hili la Salamu za Mwezi wa Pili. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa mwezi huu wa pili katika mwaka huu.
Karibu uzipokee salamu hizi. Kumbuka tuna salamu zenye kichwa:
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA MIUJIZA NA UPONYAJI (SEHEMU YA PILI)
Ebu tuendelee tukiangalia eneo lifuatalo:
KARAMA YA MIUJIZA INA KIPIMO
Angalia mistari hii:
“12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;”
(Mdo 8:12–14)
Ukiisoma mistari hiyo utaona kuwa kulikuwa na miujiza mikubwa. Biblia haiwezi kusema miujiza ni “mikubwa” kama hakuna miujiza mingine ambayo si mikubwa. Hii inaonyesha wazi kuwa miujiza ina vipimo.
Angalia mfano huu:
“10 Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;
12 hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.”
(Matendo 19:10–12)
Hapa tunaona “miujiza ya kupita kawaida.” Kwa hiyo ipo miujiza ya ukubwa, na ipo miujiza ambayo ni ya kawaida zaidi. Unapotaka karama ya miujiza, ni muhimu ufahamu kuwa miujiza hiyo ina kipimo.
ILI MTU APOKEE MUUJIZA AU ATENDE MUUJIZA, ANAWEZA PEWA MAELEKEZO YA NINI AFANYE
Angalia mistari hii:
“6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho,
7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.”
(Yohana 9:6–7)
Mtu huyu ili apokee muujiza ilibidi apokee maelekezo na kuyafuata. Kama asingeyafuata, asingepokea muujiza wake.
Angalia mfano mwingine:
“Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.”
(Yohana 5:6–9)
Fikiria kidogo: kama asingejitwika godoro na kuanza kutembea, angepokea muujiza wake?
Bwana Yesu Kristo alipokuwa anataka kutenda muujiza, mara nyingi aliwapa watu maelekezo ya kufanya.
Angalia mfano huu:
“12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
18 Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
19 Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.”
(Luka 17:12–19)
Kama wangekataa kufuata maelekezo hayo, wasingekutana na muujiza wao.
Pia wakati Mungu alipotaka kuwaokoa wana wa Israeli, aliwapa maelekezo ya kutumia damu katika milango:
“12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.”
(Kutoka 12:12–13)
Kwa hiyo, ili Mungu afanye muujiza kupitia maisha yako, anaweza kukupa maelekezo. Na hata unapohitaji kupokea muujiza, unaweza kupewa utaratibu au maelekezo ya kufuata.
Angalia mfano wa Naamani:
“10 Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.
11 Lakini Naamani akakasirika…
13 Watumishi wake wakamkaribia…
14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.”
(2Wafalme 5:10–14)
Kama Naamani angekataa kufuata maelekezo, asingepokea muujiza wake.
MUNGU PIA HUWAPA WATUMISHI MAELEKEZO ILI WAFANYE MUUJIZA
Mungu alimpa Musa na Haruni maelekezo ili wafanye miujiza:
“19 BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Shika fimbo yako, kaunyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri… ili yageuke kuwa damu…
20 Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA alivyowaambia…”
(Kutoka 7:19–20)
Na hapa tena:
“16 BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Nyosha fimbo yako, ukayapige mavumbi ya nchi, ili kwamba yawe chawa…”
(Kutoka 8:16–19)
Na pia:
“8 BWANA akanena na Musa na Haruni…
9 Farao atakaponena nanyi… Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka.”
(Kutoka 7:8–9)
Pia:
“1 Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini…
2 BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo.
3 Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka…
4 BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia…”
(Kutoka 4:1–4)
Ukiangalia mistari hii, utaona kuwa Mungu huwapa watumishi wake maelekezo ili miujiza itokee na watu waone maajabu.
HITIMISHO
Ebu tuishie hapa. Tuonane katika eneo hili la salamu za mwezi wa tatu.
BARIKIWA.
JINSI YA KUPATA MASOMO YETU
1. App: HUSONEMU (MWAKATWILA) – Play Store
2. Tovuti: www.mwakatwila.org
3. YouTube: HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU
4. Facebook: SOMA NENO LA MUNGU
5. Instagram: Huduma ya Soma Neno la Mungu
6. DVDs 📀 au CDs 💿
7. Vitabu
NB: Wasiliana na mhudumu ofisini: +255 763 109 733 (Vitabu, DVD & CD)
KWA NJIA YA REDIO
➖ Rungwe FM 102.5 MHz – Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku
➖ Baraka FM 107.7 MHz – Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku
➖ Bomba FM 104.1 MHz – Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku
ONLINE RADIO
radio.mwakatwila.org
Ratiba ya Vipindi vya Redio
Saa 12:00 – Asubuhi
Saa 07:00 – Mchana
Saa 12:00 – Jioni
Saa 03:00 – Usiku
10: INGIA MWAKATWILA YOUTUBE ONLINE
MAWASILIANO
+255 754 849 924
Au
+255 756 715 222
Wako,
Mwl Steven Mwakatwila & Beth Mwakatwila
