Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. ni siku nyingine tumepewa katika mwezi huu wa nane, Tunamshukuru Mungu kutupa mwezi huu. Mwezi uliopita tulikua na semina tatu mfululizo.
Tulikua na semina Chunya mjini tulipomaliza tukaenda Chimala na tukaenda Ubaruku. Tulikua na semina nzuri sana.
Hebu tusongee mbele. kumbuka tunasalamu zenye kichwa.
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)
Mwezi huu tuna salamu hizi
UTOFAUTI WA NENO NABII NA NENO UNABII.
Watu wengi sana hawajui kuwa kuna utofauti wa neno Nabii na neno unabii. watu wengi wanaposikia neno unabii wanachanganya na neno nabii
Angalia mistari hii uone “Na manabii wote wakasema hivyo kwa unabii, wakisema, Kwea Ramoth-Gileadi, ukafanikiwe; kwa kuwa BWANA atautia mkononi mwa mfalme.” (1 Wafalme 22:12)
Ukiisoma mistari hiyo unajifunza hapo kuna utofauti wa nabii na unabii.kwa mujibu wa mistari hii unaona Nabii alisema unabii. Maana yake nabii anweza kupokea unabii na akausema
MAANA YA NENO UNABII.
Sikiliza unaposikia neno unabii maana yake nineno lisemwalo kutoka kwenye ulimwengu wa roho au ni neno ambalo linatoka kutoka kwa Mungu moja kwa moja au wazi wazi.
Mungu anaweza kumpatia mtu yoyote neno au maelekezo wakati mtu huyo si nabii. Mtu huyo anapopewa neno, neno hilo ndiyo linaitwa unabii. Unapolipokea neno hilo wakati wewe si nabii ndiyo tunaita karama ya unabii
NABII NI OFISI. ANAPOKEA NENO MOJA KWA MOJA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
Ukisikia neno nabii maana yake ni mtu maalumu aliyeumbwa na Mungu ili apokee neno litokalo kwa Mungu. Mtu wa namna hii yeye yupo tofauti na mtu ambaye si nabii ila anaweza kupokea neno kutoka kwa Mungu.
KUNA KARAMA YA UNABII YAANI SI NABII HUPOKEA NENO MOJA KWA MOJA KUTOKA MUNGU
ANGALIA MFANO “Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena. Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini.Mtu mmoja kijana akapiga mbio, akaenda akamwambia Musa, akasema, Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini.Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee bwana wangu Musa, uwakataze.Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA angewatia roho yake.” (HESABU 11 :25-29).
Hawa watu hawakua manabii.ila walipokea unabii na waliutoa.
UTOFAUTI NABII NI MUDA WOTE ANAPOKEA NENO KILA WAKATI
Nabii yeye kaumbwa hivyo,yeye macho yake yanaona pande zote mbili yaani ulimwengu wa roho na ulimwengu huu tulionao.
Zamani walikuwa wanaitwa waonaji “kwa hiyo lazima tujue kuwa kupewa unabii si tiketi kuwa wewe ni nabii.”
AGANO JIPYA KILA AAMINIYE MUNGU ANATAKA AMPE ROHO YA UNABII
Sikia Mungu anaposema taka karama zilizokuu fahamu anataka kuona watu wasio manabii wakitaka wapewe zawadi ya namna hii ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mungu moja kwa moja
“Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” (1Kor 12:8-11)
Angalia na hii mistari.“Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.” ( Ufu 19:9-10).
Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona wazi kuwa unaweza kuwa si nabii Mungu akakupa Roho ya unabii yaani ukapewa maelekezo au maagizo moja kwa moja kutoka kwa Mungu.
Naamini umeelewa.Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.