Salamu – Octoba, 2025

BWANA YESU KRISTO ASIFIWE SANA
Pole na kazi zote, tunamshukuru Mungu ametupa mwezi huu wa kumi.
Hebu tuanze kupokea salama za mwezi wa kumi.


JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)

JIFUNZE KUOMBA KINABII

Angalia mistari hii:
“5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa. … 13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.” (1 Kor 14:5 na 13)

Kwa mujibu wa mistari hii inasema tunatakiwa tuombe kwa roho, kwa kunena kwa lugha. Kuomba kwa kunena maana yake ni kunena kwa lugha.
Sasa sikia, mtu anaponena kwa lugha maana yake anazungumza na Mungu kwenye ulimwengu wa roho.


UKIOMBA KWA ROHO UKIONGEZA KUFASIRI SAWA SAWA UNABII

Ili ulimwengu wa roho umjulishe huyo aliyeomba kwa kunena kwa lugha anatakiwa aombe kufasiriwa.
Ukifasiliwa maana yake umepewa neno la Mungu la kukupatia jibu; neno hilo tunaita unabii.

Sasa sikia, mtu anayeomba kwa kunena kwa lugha ukaongeza kufasiriwa sawasawa unabii.

Watu wengi wanaomba kwa kunena kwa lugha, hawaludi kumuomba Mungu awafasiriwa kile walichokua wamekiomba.

Sasa sikia, ukiomba kufasiriwa tenga kufuatilia ndoto au maono au kukisikia Mungu anakisema wakati ukiomba au baada ya kuomba.
Watu wengi wakiota ndoto au maono hawajui kuwa huenda ndiyo majibu ya maombi yao waliyoomba kwa kunena kwa lugha.


Angalia mfano huu

“Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.” (Habakuki 2:1–3)

Habakuki aliomba. Mungu akamwambia ili apokee jibu la maombi yake afuatilie ndoto atakayoiota.
Sikia, ndoto hiyo ilibeba maelekezo kutokea mbinguni tunaita unabii.

Sasa leo hii unaweza ukaomba kwa akili au kwa kunena kwa lugha jifunze kuupokea unabii ambao ndani yake umebeba maombi yako.


MWISHO

Katika salamu za mwezi ujao tutaanza kuzitazama salamu mpya kwenye eneo hili.
Niombee ili Mungu atupe salamu kwa majira hii kutoka kwa Mungu.

Na amini umebarikiwa katika hili somo.
Tuonane katika salamu za mwezi ujao. Mungu akubariki sana.


UKIHITAJI MASOMO YETU, UNAWEZA KUYAPATA KWA NJIA HIZI ZIFUATAZO:

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” – utaipata Play Store, ambapo kuna masomo mengi sana hapo.

  2. Tovuti yetu: www.mwakatwila.org

  3. YouTube: Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU)

  4. Facebook: Ingia katika tovuti yetu uone alama ya Facebook (f), “like” na utapata maelezo ya kujiunga; au andika “SOMA NENO LA MUNGU” moja kwa moja kwenye Facebook.

  5. Instagram: Tafuta “Steven Mwakatwila”.

  6. DVDs au CDs

  7. Vitabu – Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata vitabu, DVD na CD.

  8. Kwa njia ya Redio – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:
    • Rungwe FM 102.5 – Kila Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku
    • Baraka FM 107.7 – Kila Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku
    • Bomba FM 104.1 – Kila Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku
    Unaweza pia kutusikiliza kwenye Online Radio yetu: radio.mwakatwila.org

Kwa mawasiliano zaidi:
+255 754 849 924
+255 756 715 222


Wako:
Mwl. Mr & Mrs Steven Mwakatwila