Salamu – Septemba, 2010

Mpendwa katika Bwana, Steven na Beth, tunakusalimu katika jina la Bwana Yesu, Sisi ni wazima tunamshukuru Mungu kwa kutujaria tena uzima, Nimaombi yetu kwa Mungu akufanikishe sana katika mambo ya rohoni na ya kiuchumi, hizi ni Salamu zetu za mwezi huu wa tisa. Zinapatikana katika kitabu cha (MITHARI 24 :27) “Tengeneza kazi zako huko nje,jifanyie kazi yako tayari shambani, ukiisha, jenga nyumba yako”. Mungu akujarie kuyafanya haya katika maisha yako yote. Bwana Yesu akubariki.