Salamu – Octoba, 2010

Bwana asifiwe sana tunakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo aliye hai. Tuna kila sababu za kumuinulia Mungu wetu shukrani nyingi kwa wema wake aliotutendea katika mwezi uliopita, kwa kweli mwezi huo uliopita tumekuwa na Muda mrefu wa kuwa na Bwana katika maombi, na pia tumekutana na watu wengi ambao walikuwa na mahitaji mbalimbali,kama magonjwa, kufunguliwa katika vifungo mbalimbali kwa njia ya maombi, tumemuona Bwana akiwafungua watu wengi sana, Bwana Yesu asifiwe sana! Mungu ametupa kuona tena mwezi huu wa kumi katika mwaka huu wa 2010. Ni neema kuona mwezi mpya, nina amini hata wewe Mungu amekuvusha salama na kakupa mwezi huu wa kumi, inawezekana umekuwa katika wakati mgumu sana katia mwezi huo uliopita, na taka nikutie moyo mpendwa, sahau yote mabaya uliokutana nayo, nina imani kuwa mwezi huu kuna baraka na neema nyingi kutoka kwa Bwana ambazo amekuandalia ebu jipange kupokea sema, Amen.

MUOMBE MUNGU AKUGEUZE NIA AU FIKIRA ZAKO 

Mwezi huu ni nazo salamu maalumu kwako, nazo ni hizi, unatakiwa Uanze kufanya maombi maalumu. Ni maombi gani hayo? Ni haya MUOMBE MUNGU AKUGEUZE NIA YAKO! Na pia uwaombee na wengine Mungu awageuze nia zao.   Sikia maneno haya yasemavyo. ” …..bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema,ya kumpendeza, na ukamilifu.” {Rum 12:2b} Unaweza kuwa na swali hili, neno nia maana yake nini? Nilipokuwa naliangalia neno hilo nia nikagundua kuwa nia ni dhamili, ni fikira au ni ufahamu ama ni akili! Au kukusudia, au kudhamilia, ukisoma maneno hayo kwenye Biblia ya kiingeleza utaona limeandikwa hivi “… but be transformed by the renewing of your mind”  angalia tena maneno haya ”  Ambao  ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini….” {1KOR 4:4}. Pia ukiyaangalia maneno hayo kwa lugha ya kiingeleza, neno fikira imeliita Minds ona.”The god of this age has blinded the minds of unbelievers….” . Ndio maana na sema anaposema tugeuzwe nia zetu, kwa ujumla wake alikuwa anataka kutuambia tunatakiwa tugeuzwe katika mfumo mzima wa fikira,mawazo au akili zetu. Au makusudio yetu tuliyo ya kusudia au mambo yale tuliyo ya dhamilia.

Umewahi jiuliza swali kwa nini watu wanafanya uovu? Au kwa nini watu wanadanganywa, halafu hawaoni  kama wanadanganywa, wapo kwenye hatari harafu hawaoni kuwa wako kwenye hatari nk. ukiona watu wapo kwenye mfumo kama huo fahamu kuna tatizo kwenye nia zao au akili zao . kwa ujumla ukiwaangalia watu wengi utagundua hiki ninacho kuambia, Shetani yeye anachokifanya ni kuziteka nyara fikira za watu au kwa lugha nzuri huziloga fahamu za wanadamu, Ikiwa fikira zako {akili} zimetekwa na adui fahamu hutaweza kugundua kuwa unadanganywa,unaibiwa, unatawaliwa, unanyanyaswa, upo hatalini, unafanya huduma ya watu wala si ya Mungu, unaweza kuniuliza kivipi? Ngoja nikuambie unaweza kufanya kazi ya watu ukafikiri unamtumikia Mungu kisa ni fikira zako zimetekwa tu, .Angalia maneno haya ya Bwana yasemavyo. “ Si kila mtu aniambiaye Bwana Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe;….” {MT 7;21-23}

Hao ndugu walikuwa wanafanya huduma kabisa, lakini Yesu anasema hawajui. Kwa nini aseme hawajui watu waliofanya huduma tena kwa jina lake? Sikia hawakufanya huduma hizo kwa mapenzi ya Mungu au kwa lugha nzuri kama Mungu atakavyo! Walijifanyia kama watu Fulani watakavyo au kama wao watakavyo au kwa makusudio yao wenyewe. Ikiwa leo hii fikira zako zimeharibika na kuambia ukweli huwezi kufanya jambo jema lolote lile kumbuka katika RUM 12: 2B Neno la Bwana linatuambia hivi ” …..bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema,ya kumpendeza, na ukamilifu.” {Rum 12:2b}. Utaona hapo kuwa ili ufanye yaliyo mapenzi ya Mungu lazima nia yako ikaye sawasawa! Kumbuka shetani anacho kifanya ili kukualibia wewe usiyafanye yaliyo mapenzi ya Mungu atatafuta kuziteka nyara fikira zako hizo, na akifanikiwa kuziteka nyara tu basi, hutaweza kuwa kama Mungu anavyokuwazia,au kama alivyokukusudia, hutafanya kazi ile Mungu atakayo uifanye, unajua hutaziona njia za baraka maishani mwako, kwa sababu fikira zako zimegeuzwa na adui,adui hataki upate mema wala uyafanye mema. Unajua Huwezi jua haki zako ni zipi alizokupa Mungu katika maisha yako yote. Neno la Mungu linasema wazi kuwa twende kwake Mungu tukahojiane naye kuhusu habari za haki zetu ambazo ni halali yetu kupewa,”Unikumbushe ; na tuojiane;eleza mambo yako,upate kupewa haki yako” {ISAYA 43: 26}  

Hebu wewe mwenyewe jiulize swali hili, kwa nini leo hii nchi za Kiafrika nyingi ni masikini kweli wakati Mungu amezipa kila aina ya utajiri, ukiangalia aridhi aliyotupa Mungu imejaa utajiri mkubwa, angalia anga alilotupa Mungu linadodosha mvua kwa majira yake, angalia jinsi Waafrika tulivyo utaona wazi kuwa tokea kale ni watu ambao Mungu ametujaria nguvu, wewe angali leo hii Afrika kuna wasomi wengi tu, lakini ni masikini! Nini sababu inayopelekea tuwe masikini wakati utajiri tunao? Ebu ona Mtanzania mwenzangu jinsi tulivyo, je! Kuna sababu yoyote ile ya maana inayotufanya sisi tuwe masikini kama si hii nina yokuambia ya tatizo kwenye mfumo mzima wa akili zetu? Ebu jiulize swali kwa nini leo hii watoto wa Mungu yaani watu waliokoka, kwa lugha nzuri Wakristo ni masikini kweli, wakati Bwana Yesu Kristo alipokuja hapa Dunianii moja ya kazi aliyoifanya ni kuwatoa watu wote wa mwaminio kwenye umasikini, sikiliza maandiko yanavyo sema “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajiri yenu,ingawa alikuwa tajiri,ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umasikini wake” {2 KOR 8:9}. 

Neno la Mungu hapo linatufundisha wazi kuwa Bwana Yesu aliamua kufanyika masikini ili apate kutufanya sisi tuliokuwa masikini tupate utajiri, sasa angalia watoto wake tulivyo utaona wazi tupo tofauti kabisa na hilo andiko. Wewe tembea uone watu waliokoka wanavyo kula, wanavyo vaa, wanapolala yaani nyumba zao, utaona wazi ni wahitaji sana. Ona watoto wetu wanapo soma, kama wamefaulu basi ndio wanakwenda kwenye shule za kata, na sisi tunashangilia kweli na kusema Mungu ametenda muujiza mtoto amefaulu ameenda shule ya kata! Nenda kaone hizo shule za kata zilivyo, hakuna waalimu na kuna matatizo mengi kweli, Swali kwa nini tuwe hivyo wakati Yesu amekuja kututoa kwenye umasikini na kazi hiyo njema tayari ameisha ifanya miaka takribani elfu mbili iliyopita? 

Ukiliwaza kwa kutulia jambo hili na kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu utagundua kuwa tatizo liko kwenye mfumo mzima wa kuwaza kwetu,kufikiri,kwetu au niseme hivi nia yetu imeharibiwa ingawa tumeokoka, na kwa kuwa nia au akili zimeharibiwa ndio maana tuko hivi tulivyo, ili tutoke hapa tulipo tunahitaji msaada kutoka kwa Mungu wa kugeuzwa nia zetu. Sikia neno la Mungu linasema wazi kuwa mtu yeyote yule akiwa mrithi hapewi mali mpaka akili zake ziwe zimekaa sawa! Ona maneno haya yasemavyo . “Lakini nasema ya kuwa mrithi,wakati wote awapo mtoto,hana tofauti na mtumwa,angawa ni Bwana wa yote;……kadharika na sisi tulikuwa watoto,tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.” {GAL 4:1-3}. Ukiyaangalia maneno hayo ya Mungu utagundua hiki ndicho ninacho kuambia kuwa umasikini uliolibana kanisa tatizo lake au chanzo chake kipo kwenye akili zilizo halibiwa. Ona anasema mrithi yeyote yule akiwa mtoto hapewi urithi au hapewi mali mpaka atakapo pata akili ,kwa lugha nzuri mpaka nia yake iwe imekaa sawa, kumbuka tulikotoka nia ni fikira ni dhamini, ni mfumo mzima wa mawazo ya mtu na makusudio yake, sasa ona mtoto mdogo anachotofautiana na mtu mzima ni katika mfumo mzima wa kufikiri, kuamua,na kutenda, ambako ndani yake kunakujua au kufahamu mambo yaliyo mema au yaliyo mabay, mtoto hawezi kupambanua mambo, hayajui mema wala mabaya anachanganya yote, ona Biblia inavyosema “ Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima,ambao akili zao, kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua mema na mabaya” { EBR 5:13} Mtoto tofauti yake na mtu mzima ipo hapo kwa mujibu wa Biblia, mtoto hajui sana neno la haki, hajui kipi chema na kipi kibaya, mara nyingi makusudio yake ni ya hatari sana kwake na wazi wake, unanielewa mpendwa?  

Kwa nini warithi wawe masikini wakati wao ndio wenye uhalali wote wa kumiliki mali ya Baba yao? Jibu ni rahisi baada ya kuona sifa za mtoto, mtoto uwezo wa akili yake ni mdogo, kwa kuwa ni mdogo hapewi mali ya baba yake, mpaka akili zake zitakapo kaa sawasawa. Kanisa leo hii ni masikini ni kwa sababu hiyo ya mfumo wa akili umehalibiwa, kumbuka mtoto hajui mali za baba yake,kila gari likipita barabarani akiliona atasema la babaaaa! Wakati si la baba yake, wewe kutana leo hii na watoto wa Mungu harafu waulize swali hili, mali za Mungu ni zipi na mali za shetani ni zipi? Utasikia majibu yake ambayo yanaweza kukufanya ulie au masikio yako yawashe! Sijawahi kuona katika maandiko kitu chochote cha shetani. iIa Biblia yangu inasema vitu vyote ni mali ya Bwana haleluyaa! Kwa nini tuko masikini kanisa? Sikia jibu ni hili lazima tubadilike ndani yetu, au fikira zetu zigeuzwe. ukiangalia jinsi watu wengi walivyo utagundua hiki ninachokuambia. wewe fikiri mtu anaona kabisa anakosa haki zake za kimsingi kama huduma za afya, au huduma za malazi nk, na utakuta mtu huyo analalamika kabisaa kuwa yupo shidani, lakini cha ajabu utaona hatafuti nja ya kutoka kwenye hiyo shida yake, mtu anaona kabisa hapo alipo iwe kanisani au sehemu yoyote ile anadanganywa au anaibiwa, unaweza kujiuliza inawezekanaje mtu aibiwe kanisani? Ona maneno haya utajua unaweza ukawa kanisani na ukageuzwa punda wa mtu “Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu,kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo,wataoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza,wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa;…” { 2PETRO 2: 2-3A}  

MUNGU TU NDIYE MWENYE UWEZO WA KUTUGEUZA NIA AU FIKIRA ZETU 

Ukiyaangalia maneno hayo utaona wazi neno la Mungu linatuonya kuwa kuna watu ambao watatokea kama watumishi lakini wala si watumishi wa Mungu, ni watu wajitafutiao faida kutoka kwa watu wanao mwamini Yesu, sasa mtu ambaye fikira zake zimetekwa na adaui hawezi kupima au kuaangalia, hachanganui mambo yupo yupo tu. unajua ni kwa nini? kumbuka tatizo liko kwenye nia yakei! fikira zake zimealibiwa hajitambui, mtu wa namna hiyo anaitaji msaada. na msaada ni Mungu tu. Ni kuomba Mungu aingilie kati na kuzigeuza fikira za mtu huyo. Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kukugeuza wewe hiyo nia yako, nakuambia ukweli wewe huwezi kujigeuza, ona hayo maneno ya Bwana ya semvyo ‘ Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu” Anapo sema mgeuzwe, kwa kufanywa upya nia zenu ana maana yupo atakaye kugeza na kukufanya upya! Kama uwezo wakugeuka na kufanywa upya nia yako ungekuwa mikonono mwako, angesema, ugeuze na ifanye upya nia yako. Lakini anaposema mgeuzwe na kufanywa upya, anataka kutuambia yupo awezaye kukugeuza na kukufanya upya katika hiyo nia yako , ni nani huyo? Ni Bwana Yesu peke yake 

Nia za watu wengi zina hitaji kugeuzwa. Maombi na Neno la Mungu tu, ndivyo vinavyo weza kukugeuza hiyo nia yako, ukianza kuomba Mungu akugeuze hiyo nia yako, Mungu ndipo atakapo kugeuza hiyo nia yako au kwa lugha nzuri ataanza kuiweka sawa, na ndipo utakapo anza kuona ni wapi ulipo na unatakiwa ufanye nini ili utoke hapo ulipo. Ona mfano huu, wana wa Israeli walikaa jangwani miaka alobaini, bila kuiona njia ya kuwatoa jangwani, tena naamini wengine walikuwa hawoni umuhimu wa kuitafuta njia ya kutokea jangwani, miaka alobaini hao watu hatusikii kama walifanya maombi maalumu ya kumuomba Mungu ili awatoe hapo walipokwama, unajua kwa nini walikuwa hawaioni njia? Ni kwa sabau fikira zao zili kwama,zilifungwa, fahamu fikira zako zikifungwa hata macho yako hayataona njia, wale ndugu hawakuiona njia ya kutokea kwenye jangwa mpaka Bwana alipo waambia Geukeni, unajua alifanya nini? Alitengeneza ufahamu wao, hapo ndipo walipogeuka. ” Ikawa mwaka wa arobaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi,Musa akawaambia wana wa Israeli kama yote aliyopewa na Bwana ya kuwaamuru; alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori aliyekuwa akikaa Heshboni,na Ogu mfalme wa Bashani,alikuwa akikaa Moabu,alipoanza Musa kufunua torati hii, akisema,Bwana,Mungu wetu, alituambia huko Horebu,akasema,mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori……..“ {KUM 1:3-7}. Ndugu zetu hawa walikaa hapo miaka alobaini ebu fikiri miaka alobaini ni mingi sana, hawaioni njia ya kutokea hapo jangwani, mpaka Mungu alipowaambia wageuke,ndipo walipogeuka,na walipogeuka tu, njia wakaiona ya kutokea kwenye hiyo shida yao. Inawezekana hata wewe ndugu yangu una miaka mingi hapo ulipo umekwama kitakacho kutoa hapo ni hiki. Utakapo badirika fikira zako! 

Neno nia ni fikira, nataka ni kuulize swali hili, je! Unafikiri nini juu ya utumishi aliokupa Bwana? Unafikiri nini juu ya habari za kusoma kwako? Unafikiri nini juu ya habari ya kiuchumi? Unafikiri nini juu ya kutoka kwenye hiyo shida uliyo nayo, najua unapita jangwani,inawezekana jangwa lako ni ndoa, ni uchumi mbovu,ni ugonjwa, ni kukataliwa, ni hili huna mtoto, inawezekana jangwa lako ni dhambi Fulani imekutawala, kweli unatafuta namna ya kuishinda unashindwa mpaka umekata tamaa, inawezekana unamiaka mingi umezunguka kwenye hilo jangwa, huoni njia ya kutokea, sikiliza huoni njia ya kutokea kwa sabau mfumo wa fikira zako umeharibiwa.  

Watumishi wengi wa Mungu leo hii ukiangalia huduma zao utangundua hiki ni nacho kuambia, ziko pale pale, hazikui, kisa nini unajua? Fikira zao! Huwezi kupiga hatua ya pili kihuduma mpaka umebadilika ndani yako au katika fikira zako!. Wewe fikiria tokea umeanza kuchunga ona maendeleo ya uchungaji wako kama unakua, ona hao watu unaowachunga kama wanabadilika iwe kiroho au kiuchumi, kama hawakui, tatizo liko kwako mtumishi, unatakiwa ubadilike nia yako, ugeuzwe kutoka nia yako hiyo ya kizamani uipate nia mpya kutoka kwa Bwana ambayo itakufanya ufanye huduma katika mapenzi ya Mungu na kwa kiwango alichokupangia uwe kwa wakati huu, ukifanya huduma katika mapenzi ya Mungu huduma hiyo ndani yake kuna mafanikio. Wewe angalia watumishi wengi wanavyoishi maisha ya kimaskini kama watoto yatima wakati wanaye Baba yao aitwaye Yesu Kristo, na hawaoni njia ya kutoka kwenye huo umasikini ambao unawapelekea watumishi wengi wawe watumwa wa watu Fulani. Na wao hawaoni kuwa ni watumwa kwa sababu mfumo wa fikira umeharibika. Ngoja nikupe mfano huu labda utaelewa. Watumishi wengi leo hii hawawezi kuikemea dhambi kwa watu Fulani kisa ni kwa sababu hao watu ndio wanao watunza! Angalia leo hii kanisa la kiafrika lilivyo utaona wazi kuwa akili za watumishi wengi ziko ulaya badala ya mbinguni aliko Bwana wao aliyewaajiri. Wanajikuta wakitumikishwa na watu, kisa eti wanawapa msaada. Fikiri uone utaona huifanyi kazi ile aitakayo Bwana Yesu bali unaifanya kazi ile aitakayo mtu Fulani aitwaye mfadhili! 

Siku utakapo badilika katika fikira zako na kuambia ukweli ndipo utakapo iona njia ya kutokea, wewe anza kuomba maombi maalumu ya kubadilishwa hizo fikira zako utaona nakuambia, utashangaa, ndipo utaona wazi kuwa Mungu anavyoitazama huduma yako anaitazama tofauti na wewe na watu wanavyoitazama, wewe unaweza ukaona imekuwa sanaa, kumbe Mungu anakuona umedumaa kabisaa na unamuudhi, ndipo utakapo anza kuona kuwa ulianzisha kanisa nakujiita mchungaji wakati wewe ni mwinjilisti tena wa kimataifa,ndipo utatambua kuwa umepoteza muda kwenye huduma ambayo mungu hakukuitia. Hapo ndipo utakapoanza kujua kuwa huduma uliyo nayo unatumia nguvu zako tu, wala si nguvu za Mungu, unaweza kujiuliza swali je! Na weza kumtumikia Mungu kwa nguvu zangu? Sikiliza maneno haya ya Bwana yasemavyo, “Lakini nikasema , nimejitaabisha bure,nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana,na thawabu yangu ina Mungu wangu na sas Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake,ili nimletee Yakobo tena,na Israeli wakusanyike mbele zake tena;{ maana mimi nimepata heshima mbele za macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu}; naama asema hivi, ni neno dogo wewe kuwa mtumishi wangu ili kziiinua kabila za Yakobo,na kuwa rejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa;” {ISAYA 49:4-6A}. 

Fikiri mtumishi Isaya alianza kufanya huduma kabisaa, lakini alikuwa hajui kuwa anafanya huduma kwa kutumia nguvu zake, na kwa kuwa alikuwa akitumika kwa kutumia nguvu zake kazi ile ilikosa matunda, yaani ilikuwa ni kazi isiyo na faida. Kumbuka alikuwa anatumika na watu wakimwita Mtumishii! Ila mbinguni Mungu alipokuwa anamwangalia aligundua kuwa huyo jamaa alikuwa anatumika tofauti na Mungu alivyotaka atumike. Siku Nabii Isaya anapata akili mpya ndipo alipogundua kuwa amepoteza muda na nguvu zake bure kwa huduma ambayo ilikuwa haina faida. Ngoja nizungumze hili uone leo hii watumishi wengi wanafanya huduma ambayo nakuambia ukweli haina faida mbinguni kabisaa, ona leo hii mtumishi ana andaa mkutano wa injili, lakini baada ya mkutano kwisha shetani halii, ila wachungaji waliomznguka huyo mtumishi ndio wanaolia, kisa, kawachukua watu waliokuwa wakristo tena wameokoka kabisaa, na yeye utasikia anasema OOO Kazi ya Bwana inasonga mbele! Wewe angalia hapo kanisani kwako ulipo una watu wangapi ambao uliwakuta wapagani na una watu wangapi ambao uliwakuta ni Wakristo tena waliookoka kabisaa. Siku utakapo anza kuomba Mungu akugeuze nia yako, ndipo utakapo gundua miaka mingi umefanya kazi isiyo na faida kwa Mungu. Mungu anafaidika nini wakati mkristo Fulani anapohamia sehemu fulani? Mungu anafaidika pale tu watu wasiomjua Yesu yaani Wapagani wanapoamua kutubu na kumpokea Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wao, hapo ndipo kuna kuwa na furaha Mbinguni. Siku moja nilikwenda kwenye mji Fulani, nilikuta makanisa yapo mengi sanaa, nikafikiri eneo hilo wapagani ni wachache. Nilipofanya utafiti, niligundua kitu hiki ninacho kuambia kuwa tunahitaji kugeuzwa nia zetu kama kweli tunataka tutende yale ya mpendezayo Mungu katika utumishi wetu. 

Niligundua eneo hilo wapagani ni wengi sana, kwa nini pawe na wapagani wengi sana wakati makanisa hapo yapo mengi kwelikweli? Nikagundua jambo hili kila mtumishi aliyekuja kuanzisha kanisa hapo hakuwatafuta wapagani, aliwatafuta Wakristo waliokoka walioko katika madhehebu mbalimbali. wao wakaona kazi ya Mungu inaenda kwa mfumo huo, wakati haiendi,na hawaoni kama haiendi, kazi kubwa wanayo ifanya ni kuchukuliana waamio, huyu mwaka huu akiandaa mkutano au semina nzuri basi ana uhakika wa kuwachukua wakristo walioko nje ya dhehebu lake, na huyo aliyechukuliwa waamini, naye anaenda kutafuta mtumishi mhubili mkubwa, ili naye awakombe wakristo wote walio nje ya dhehebu lake, Swali langu ni hili hao watu wanafanya huduma yenye faida au hasara? Jibu unalo wewe mwenyewe, swali la pili ni nini tatizo? Jibu ni hili tatizo lao lipo kwenye fikira zao au nia yao kumbuka nia ni dhamiri au makusudio, sasa ukikaa na kuangalia utaona watumishiwa namna hiyo wanahitaji kugeuzwa nia zao, au mtazamo walio nao. Sikia Sikufikira zao zitakapo badilika ndipo watagundua kuwa kazi wanayoifanya haina faida, hawawezi kutoka kwenye tabia hiyo isyo njema mpaka wameanza kuomba au kuombewa kwa Mungu ili awabadilishe mfumo mzima wa kufikiri kwao. Sikia mtumishi leo unahitaji kugeuzwa hiyo nia yako., hapo ndipo utakapo iona hiyo njia ya kutokea.  

Sikiliza Mtanzania na Wewe Mwafrika mwenzangu, ili leo hii tutoke kwenye jangwa la utumwa tulionao unao tokana na umasikini uliokidhili lazima tuanze kumuomba Mungu atugeuze nia zetu hizi tulizo nazo, ambazo zimeharibiwa na mwovu, wewe fikiria maisha tuliyonayo,ona, tazama, chunguza, utaona wazi kuwa si mpango wa Mungu au si mapenzi ya Mungu tuishi maisha ya namna hii Watanzania na Waafrika,  kama si mapenzi yake tuishi maisha haya, kwa nini tunaishi hivi? Sikiliza jibu Mungu anasema. “…..bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema,ya kumpendeza, na ukamilifu.” {Rum 12:2b}.

Nina imani kwa sehemu umeelewa na umegundua chanzo cha kukwama kwako, au kwa watu wengine katika mambo yao mengi, tatizo lipo kwenye mfumo wa fikira au nia zao, Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kukugeuza wewe hiyo nia yako, nakuambia ukweli wewe huwezi kujigeuza, ona hayo maneno ya Bwana ya semavyo ‘ Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu” Anapo sema mgeuzwe, kwa kufanywa upya” anamaana yupo atakaye kugeza na kukufanya upya! Kama uwezo wakugeuka na kufanywa upya nia yako ungekuwa mikonono mwako, angesema, ugeuze na fanya upya nia yako. Lakini anaposema mgeuzwe na kufanywa upya, anataka kutuambia yupo awezaye kukugeuza na kukufanya upya, ni nani huyo? Ni Bwana Yesu peke yake. Nenda kwake muombe anao uwezo wa kukugeuza,au kuwageuza nia zao watu wote wamuendeao ili awageuze, Hebu kwa mwezi huu tuishiye hapo. Tuombeane heri ili Mungu atuvushe tena mwezi ujao ili tuendelee kupokea salamu hizi kwa upana zaidi. 

 

Mungu akubariki na kukugeuza kabisa fikira zako ziwe kama Mungu atakavyo. Asante sana  

 

WAKO 

 

MR STEVEN & MRS BETH MWAKATWILA