Salamu – Novemba, 2010

ILIUPATE KUFANIKIWA KATIKA ENEO LA KUIGEUZA FIKRA YAKO LAZIMA UYAJUE MAMBO YANAYO WEZA KUHALIBU FIKRA ZAKO 

Sikia ili leo hii upate kufanikiwa sana katika suala hili la kugeuza fikra zako au akili,ama ufahamu wako, unatakiwa ujue ni mambo gani yanayoweza kuwa ndiyo kisababisho cha uhalibifu wa fikra zako. Yapo mambo mengi sana yanayoweza kuwa ndiyo chanzo cha uharibifu wa mfumo mzima wa fikra zako, hebu tuanze kuyaangalia mambo yanayoweza kuharibu fikra zako au pia za watu wengine. 

JAMBO LA KWANZA NI DHAMBI 

Adui wa Mungu na wanadamu shetani, alijua kuwa ili leo hii alihalibu kusudi la Mungu ambalo alilikusudia kuliona likitendeka kwa Mwanadamu, aliona kinachoweza kuhalihalibu hilo kusudi la Mungu alilokusudia kwa mwanadamu ni kumchomekea mwanadamu dhambi. Dhambi ndiyo kiini cha uharibifu wa fikra za mwanadamu, Neno la Mungu linasema hivi. “ Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao…..” (1KOR 4: 4) Ukiyaangalia maneno hayo utaona kuwa neno mungu lililotumika hapo limeandikwa kwa helufi ndogo, maana yake si Mungu mkuu, bali ni adui shetani ajifanyaye mungu, sasa sikiliza, neno la Mungu hapo linatupa akili kuwa shetani ndiye anaye ziharibu fikira au nia ama akili za watu, na njia mojawapo anayoitumia kuziharibu hizo fikira za watu zisiwe kama Mungu alivyozikusudia ziwe, anatumia (kirusi) kiitwacho dhambi.  

Wewe ona mifano hii michache ndiyo utaelewa kitu hiki ninacho kuambia, sikia neno hili la Bwana lisemavyo. “Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu” (HOSEA 4:11). Ukiyaangalia maneno hayo utagundua wazi kuwa moja ya jambo linaloweza kuondoa ufahamu au fikira za mwanadamu ni dhambi, neno huondoa maana yake ni kutoa, au kuharibu au kupunguza kiwango cha ubora wa fikira alizo kupa Mungu. Fahamu ili leo hii adui aipunguze fikira yako atakachokifanya ni kukusakizia dhambi ya ulevi au uzinzi nk, Unapoifanya hiyo dhambi tu, adui ndipo anapopata mlango wa kuigeuza hiyo nia yako itoke katika njia yake ambayo Mungu alitakaipite, kwa lugha nzuri ndipo anapoiteka hiyo fikira yako, akiisha kuiteka tu, hutawaza vile Mungu alitakauwaze, hutafikiri kwa kiwango kile Mungu alikuumbia ufikili, kile kiwango cha ufahamu wako kinapunguzwa au kuondolewa kabisa.  

Angalia maneno haya ya Bwana yasemavyo “Lakini hawa nao wamekosa kwa divai,wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai,wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono,hujikwaa katika hukumu” (ISAYA 28: 7) Ukiyaangalia maneno hayo utaona wazi kuwa dhambi ya ulevi inaondoa akili au inaharibu mfumo mzima wa nia ya mtu, hao ndugu walijikuta hawawezi kuhukumu vema kisa, ni kileo, walijikuta hawana maono sahihi au fikira au mawazo sahihi kwa sababu ya kileo, neno maono ni neno pana sana, na maono hayo yanatengenezwa ndani ya akili za mtu kwenye mawazo yake. Adui anajua kuwa ili leo hii akuharibie mipang yako yote ya mbeleni (maono) atakacho fanya ni kukutengenezea kirusi kiitwacho dhambi ili kiharibu mfumo mzima wa fikira zako, na ana aina nyingi ya virusi vya dhambi, kama ulevi uzinzi, uchawi nk, Ukiwaangali watu wengi walivyo utaona jinsi wasivyo na maono au mtazamo au mipango mizuri ya maisha yao, yawe ya kiuchumi, kifamilia, au kiroho. Unaijua sababu? Ni kwa sababu mfumo mzima wa fikila zao umehalibiwa na adui, adui ameuharibu mfumo huo wa fikira za watu hao kwa kutumia kileo, Mungu anapozungumzia kuhusu mabaya yaliyo ndani ya kileo anasema “ Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. Tena msilewe kwa mvinyo,ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;” (WAEFESO 5:17-18). 

Mungu anataka usiwe mjinga, bali uwe ni mtu mwenye fikira au akili tena akili nzuri,    ukisoma hapo utaona Mungu anakupa maarifa ya kuukimbia ujinga, anasema usilewe kwa mvinyo! Kwa maana nyingine Mungu anajua kabisa kuwa ikiwa wewe utakuwa ni mtu utumiaye kileo unakuwa unaukalibisha ujinga, Sikia anasema ndani ya kileo huko kuna ufisadi. Sikia kama leo hii utalifahamu kwa upana neno ufisadi, ndiyo utaelewa ni kwanini Mungu alikukataza usimwe pombe. Pombe inaondoa ufahamu mpendwa, inaharibu mfumo wa kufikiri kwako ingawa unajidanganya kuwa ukinywa ndio unakuwa na uwezo wa kufikiri, sikia, jinsi unavyokunywa ndivyo unavyo ondoa uwezo wa kufikiri, kupanga mambo, au kuwaza kwako yaliyo mema. Ona maneno haya ya semavyo , “ Ni nini mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu! Tena ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme. Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; wala haifai wakuu waseme, kiwapi kileo? Wasije wakanywa na kuisahau sheria, na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. Mpe kileo yeye aliye na karibu ya kupotea; kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Anywe akausahau umasikini wake asiikumbuke tena taabu yake.” ( MITHALI 31:2-7) 

Ukiyasoma maneno hayo utaona wazi kuwa Mungu anakuonya wewe ndugu yangu kuwa inatakiwa uhakikishe hauwapi moyo wako watu wale wawezao kuuhalibu moyo wako. Kumbuka ndani ya moyo huko kuna hisia,utashi, na akili. Fahamu kuna watu au vitu ambavyo vinaweza kuuharibu moyo wako, au niseme kuhalibu mfumo mzima wa kufikiri kwako au kufahamu kwako . Vitu vinavyoweza kuharibu huo moyo wako kimojawapo ni pombe, sikia anasema wazi kuwa kileo hakiwafai wakuu, sikiliza hata wewe ni mkuu, kumbuka Mungu alikuumba wewe utawale, wewe ni mkuu sana ila hujajitambua tu. Neno linasema usinywe kileo na neno lina toa sababu za wewe kutokunywa kileo, neno linasema, kileo kinaharibu fahamu za wakuu, kumbuka wewe uliumbwa utawale na umiliki, inawezekana familia yako,aridhi, ofisi, fedha, gari nk.  

Fahamu unapokunywa pombe unapoteza uwezo wa kutawala kwako au kuhukumu kwako, kwa kuwapa kila mtu haki yake ipitayo mkononi mwako, ona mfano huu jinsi kileo kinavyowapoteza watu wengi kwenye kutoa hukumu ya haki, utaona mtu ni baba wa familia ana mke na watoto, lakini hawapi haki yao kisa ni kileo, ona leo hii huwezi kuwasomesha watoto wako, kisa ni pombe, huwezi kuwatunza watoto wako kama ipasavyo kisa ni pombe, huwezi kujenga kisa ni pombe, umezaa watoto wengi kweli na leo hii wanaishi maisha magumu kisa ni uzinzi, ona jinsi uwezo wako kazini ulivyopungua kila siku kisa ni pombe, unapoteza fedha nyingi sana kwenye pombe na uzinzi. 

Neno linasema mpe kileo aliye karibu na kupotea, je! Wewe ni mmoja wapo wa wawaliopotea? Kama ulipotea nakushauri uludi ugeuke leo, geuza fikira zako kwa kutokubali kunywa kileo, hapo ndipo utakapo igeuza hiyo fikira yako,utapata ufahamu kuwa unasomesha watoto wa wenzio wakwako umewaacha na mama yao wanaishi maisha magumu sana, neno linasema mpe kileo masikini ili ausahau umasikini wake, hasemi atoke kwenye huo umasikini! Maana yake nini? watu wengi wanazidi kuwa masikini kwa sababu ya kileo, wakinywa wanasahau shida zao kwa kitambo tu, yaani akili zao zinaharibiwa kwa kuusahau umasikini wao, kumbuka mtu huo bado ni masikini tu, ila kausahau kwa muda. Watu wengi wako hivyo. 

Kama watapata akili hawatatafuta kusahau bali kutoka kwenye umasikini, huwezi kutoka kwenye umasikini kama unakunywa kileo, kileo kinaharibu mfumo wa ufahamu wako, unaweza ukawa msomi na unasema nimesoma, lakini nakuambia kwa sababu ya tatizo la kunywa pombe ulilo nalo leo hii umepunguziwa vitu vingi sana ambavyo Mungu alitaka uwe navyo. usijidanganye kwa hivyo vichache unavyojifariji kuwa unavyo, jiulize swali kwa nini wewe unapata mshahara mkubwa kuliko huyo mwenzio, ona maendeleo ya huyo mwenzio yalivyo, utaona ana maendeleo mazuri kuliko wewe, ingawa wewe unamshahara mkubwa kuliko huyo mwenzio. Ina wezekana mfumo wa fikira zako tayari umeharibiwa na ulevi na uzinzi. Nataka leo hii utubu na kumuomba Mungu akugeuze hiyo nia yako. Sikia ndugu yangu leo hii wewe ni kijana na unakunywa pombe, nataka upate ufahamu kuwa uzee unakuja ndipo utakapo fahamu kuwa kileo ni kibaya, kwani utakapozeeka uwezo wa kufikiri kwako utakuwa mbaya kuliko mzee ambaye hakuwahi kugusa kileo. 

Hebu tuone madhara ya dhambi ya uzinzi, neno la Mungu linasema kuwa uzinzi unaondoa fahamu za wanadamu ““Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.” (HOSEA 4:11). Watu wengi leo hii hawajui kuwa uzinzi unaondoa ufahamu wa wanadamu, umewahi kujiuliza kwa nini watu wengi wana maamuzi ambayo kila mtu mwenye akili timamu anayashangaa, wawe ni viongozi wa selekali au dini au wa kifamilia. Neno la Mungu linasema kuwa mtu aziniye ana haribu nafsi yake, na ndani ya nafsi huko ndiko kuna akili ona neno la Mungu lisemavyo.“…Na kahaba humwinda mtu ainase nafis yake iliyo ya thamani. Je! Mtu aweza kutia moto kifuani pake na nguo zake zisiteketezwe? Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto na nyayo zake zisiungue? Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia. ….Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; wala fedheha yake haitafutika.” (MITHALI 6: 26B-28 NA MSTARI WA 32-33) .  

Unapofanya uzinzi fahamu unaharibu mfumo mzima wa fikira zako, au niseme akili yako yote inageuzwa, neno linasema aziniye na mwana mke hana akili kabisa, ikiwa wewe unafanya uzinzi Mungu anakuona huna akili, kumbuka Mungu alipokuumba alikuumba vema kabisa, alikupa akili, kinacho ondoa akili ni uzinzi, mtu yeyote yule ambaye ni mzinzi ukimwangalia utaona wazi neno hili ninalo kuambia kuwa anaondolewa ufahamu wake. Fuatilia mtu ambaye ni mzinzi jinsi mfumo wake wa kuwaza ulivyo, utaona wazi kuwa mfumo mzima wa fikira zake au makusudio yake hayawi mazuri, kama ni bosi kazini utaona kazi haziendi hapo kazini, kana ni baba ni rahisi kutelekeza familia yake yote. 

Wanaume wengi sana walio na tabia ya uzinzi utawaona kabisa fikira zao zimeharibiwa katika kuwaza kwao utaona hawawazi kitu kingine zaidi ya hao wanawake walionao, sikia neno la Mungu lisemavyo “ Maana kwa Malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande ca mkate, kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya dhamani” (MITHALI 26) Ukiyasoma maneno hayo utaona wazi kuwa mtu yeyote yule ambaye ni mzinzi neno linasema fikira zake zinaharibiwa kwa kumuhitaji huyo Malaya kama vile mtu mwenye njaa ya kuhitaji angalau kipande cha mkate. fikiri mtu mwenye njaa anaweza kufikiri vema? Kama hawezi kufikiri vema ndivyo hivyohivyo mtu mzinzi asivyoweza kufikiri vema. Wewe mwenyewe jiangaliye ulivyo kama unatabia hiyo, ukiwa umekaa na umetulia wakati huo unapotakiwa uanze kufikiri mambo ya maana  naya muhimu, utaona hapo ndipo huyo mwanamke au hao wanawake wanachukua nafasi akili mwako, utaona asilimia themanini unawafikiria hao au huyo mwanamke na hizo ishirini zilizo bakia ndizo unazo waza mambo ya maana, wewe mwenyewe jipime uone, umejiona ulivyo?  

Mungu anataka ugeuze nia yako au kwa lugha ya kueleweka akili zako, nimeona watu wengi leo hii wakipoteza fedha zao nyingi kwa kutofikiri kwao vema kwa kuwapa Malaya, na hata wakiwafumania hao wanawake na wanaume wengine wanadanganywa kama watu wasiowahi hata kwenda shule, kisa uzinzi umeloga fikira zao. Wewe fuatilia viongozi wazinzi, utaona wazi hili ninalo kuambia, mfumo mzima wa maamuzi yao mara nyingi hauwi mzuri, nilikuwa najiuliza swali hili miaka mingi sana, ni kwanini maamuzi, mipango, utekelezaji wa viongozi wengi wa kiafrika siyo mzuri, Mungu alinipa neno hili moyoni mwangu, tatizo liko kwenye fikira zao!  

Wewe fuatilia nchi zilizondelea utaona hiki ninacho kuambia, Waingeleza wako tayari kumfukza kazi au kumstaafisha kazi haraka sana kiongozi mwenye tuhuma za uzinzi, wana sema hafai, wewe fuatilia uone ndoa nyingi huko zinavyo vunjika kisa ni pale tu, mwanandoa mmoja anapokosa uaminifu kwa mwenzie, hawasamehani kama huku kwetu kulivyo. Huku kwetu kiongozi anajulikana kabisa kuwa anamsululu mkubwa wa nyumba ndogo, na watu hawasemi, wanona ni kitu cha kawaida tu, wewe fuatilia haya ninayokuambia utaona, kwa wenzetu ni shida sana kusikia bosi anatembea na katibu wake, lakini si huku Afrika, ndiyo maana nasema Waafrika Mungu anataka tuzigeuze fikira zetu, kwa kuacha uzinzi, hapo ndipo tutaona maendeleo kwenye nchi zetu hata maamuzi ya viongozi, mipango, na utekelezaji wake utakuwa mzuri, nakumbuka wakati ule ninafanya biashara, ilikuwa ukimpatia mzigo wa kuuza mfanya biashara mwenzako aliye na tabia ya uzinzi, ushishangae atakapokuja na Kiswahili kirefu cha nimeibiwa au mzigo umepotea, tena haupotei wa kwako tu hata wa kwake utapotea, ukianza kufuatilia ulikopotelea ni kwenye uzinzi tu.  

Nenda mashuleni au vyuoni utaona hiki ninacho kuambia, watu wengi ukiwaona maendeleo yao ya darasani yamepungua wewe wafuatilie utaona, wengi wao kilichopelekea kufanya kwao vibaya ni jambo hili la uzinzi, Uzinzi unaondoa na unaharibu fikira zao. Soma Biblia utaona madhara ya uzinzi ulivyo haribu mfumo wa fikira za watumishi wengi wakajikuta wanafanya mambo yaliyo wagharimu hata uhai wao, au uhai wa watu wengine, fikiri mtu kama Mfalme Sulemani ambaye Mungu alimpa akili nyingi kuliko watu wote kipindi kile. Kilicho ondoa fahamu zake ni dhambi hii ninayokuambia ya uzinzi. 

ona “ Mungu akamwambia, kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua hukumu; basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapatakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe” (1FAL 3:11-12). Mungu alimpa mfalme Sulemani akili nyingi sana kwa mujibu wa Biblia isemavyo, sasa sikia ziliondokaje! “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Falao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti; na mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, wasiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuta miungu yao. Sulemanai akaambatana nao na kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria miatatu; nao wakeze wakamgeuza moyo” (1FAL 11:1-3) ona pia mistari hii isemavyo. “ Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,” (1FAL 11:9)  

Mfalme Sulemani alipewa na Bwana Mungu akili nyingi sana, lakini alipokosea tu katika suala hili la uzinzi, akajikuta akigeuzwa fahamu au akiondolewa fahamu zake, mtu aliyekuwa na fikira nzuri sana, gafla fikira zake zinageuzwa na kuwa mbaya mpaka anamuacha Mungu wake aliyemweka kwenye hicho kiti cha kifalme, Neno kugeuzwa moyo maana yake, kugeuzwa nia yake kumbuka neno fikira ni nia, kusudio au akili, ama ufahamu. Anaposema aligeuzwa moyo wake maana yake ni hiyo. Wewe ona leo hii mtu utaoana ana ajiliwa kazi na anapokuja kuajiliwa anakuja mikono akiwa ameiweka nyuma. Sasa akipata kazi na akakutana na kirusi kiitwacho uzinzi, fahamu lazima kitamuharibia mfumo mzima wa kuwaza kwake, ataanza kumdharau hata huyo aliyemuajiri. Wewe ona leo hii ufanisi wa kazi ulivyopungua kwa watanzania wengi, utagundua kirusi kilicho wahabibu hiki kinachoitwa uzinzi. Hata watumishi wa Mungu wengine leo hii wamepoteza uwezo wao ule wa kwanza waliopewa na Bwana, kwa kumuacha Bwana kisa ni hiki kirusi kiitwacho uzinzi kimekula fikira zao, wanazini, huku wakijifanya wanamtumikia Mungu, wewe fikiri kama si kuondolewa akili tu, mtu anajiita mtumishi wa Mungu harafu anazini na wanawake wajao kumtumikia Mungu harafu mtu huyo anakuwa na ujasiri tu wa kumtumikia Mungu, hivi uoni kuwa mfumo wa akili za mtu kama huyo umeharibika, anahitaji kugeuzwa upya? Mfalme Sulemani aligeuzwa moyo wake, kumbuka ndani ya Moyo huko ndiko kuna akali, hisia na utashi, kwa maana nyingine hivyo vitu ndivyo vilivyoharibiwa, mpaka akamsahau Mungu, leo hii usishangae unapomuona mtu amesahau watoto wake au mke wake au mume wake au hata kazi yake kwa sababu ya kugeuzwa moyo wake na dhambi ya uzinzi. 

Ni nina imani kuna kitu umekipata katika ujumbe huu, jiulize ni dhambi gani uifanyayo na imekuharibia mfumo mzima wa fikira zako? Tubu leo, acha kufanya dhambi, kumbuka hili dhambi ni sehemu ya silaha azitumiazo shetani katika kuziharibu au kuigeuza mioyo yetu isiwe kama Mungu alivyotukusudia. Sikia neno hili lisemavyo “…..bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema,ya kumpendeza, na ukamilifu.” (Rum 12:2b) Anza kuomba maombi maalumu Mungu akugeuze hiyo nia yako, mwamini Mungu atakugeuza. 

Mungu akubariki. 

Wako 

Mr Steven & mrs Beth Mwakatwila