Salamu – Septemba, 2020

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Ninakukaribisha tena katika eneo hili la salamu za mwezi. ili tupate kujifunza somo hili muhimu. Mungu ametupa mwezi huu wa tisa nani mwezi tunamshukuru sana.

Nimekuletea salamu za mwezi huu wa tisa. Kumbuka tunamfululizo wa salamu zenye kichwa.

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE WOKOVU (ENEO LA KUOKOLEWA KATIKA KIPINDI CHA MAJANGA ULIMWENGUNI)

JAMBO LA NANE JIFUNZE KUKIRI USHINDI KWA KINYWA CHAKO.

Mungu ili akuokoe katika majanga kama haya pia atataka kuangalia ukiri wako angalia mistari hii naamini utanielewa vizuri. “Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya. Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe. Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.” (Isaya 16-19)

Mungu anapokasirika na kuadhibu ili aponye fahamu ataangalia maneno yasemwayo na hao watu

Angalia vizuri hapo anasema atamponya huyo aliyempiga na kumletea amani kwa sababu Mungu anayaumba matunda ya midomo.

ILI UTOLEWE KWENYE MAUTI LAZIMA UJIFUNZE KUKIRI HUO WOKOVU

Angalia hii mistari uone: “Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.” (Mithali 18:20-21)

Katika kipindi hiki unatakiwa ubadilike katika kusema kwako. *Anza kukiri huo wokovu usiseme  kwa kinywa chako kuwa utakufa.

Angalia mistari hii: “Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.” (Zaburi 118:17)

Ukitaka upone majanga haya nakushauri jifunze kuukiri wokovu kutoka kwa Mungu. Angalia mistari hii “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!” (Warumi 10:10-15)

Kile unacho kisema au kukikirifahamu ndicho kinaumbwa. katika ulimwengu wa roho fahamu wanafanyia kazi sana matamko yaliyosemwa na mtu au watu.

Iliuokoke leo na tauni au na jehanamu fahamu unatakiwa umuamini Bwana Yesu Kristo kuwa ndiye atakaye kuokoa. Sasa kwa mujibu wa hiyo mistari tunaona kuna mambo mawili hapo.

Jambo la kwanza ni kuamini moyoni,jambo la pili ni kusema au kukiri. Kwa nini unatakiwa ukiri? Kwa Mujibu wa hiyo Isaya na Mithali,unaona yakua wokovu umefungwa pia ndani ya kukiri kwa watu.

Jifunze kuisemesha nafsi yako katika kipindi kama hicho maneno kama haya. “Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa; Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu. Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA. BWANA ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife.”(Zaburi 118:16-18).

Mwimba Zaburi hiyo aliyasema maneno hayo ya ya sintakufa bali ntaishi katika kipindi akitumikia adhabu iliyoletwa na Mungu

Kwanini alisema hivyo? Jibu ni rahisi tu, alitaka Mungu aumbe matunda ya kinywa chake ili apate wokovu asife katika adhabu hiyo.

Hata wewe ukikutana na kipindi kama hiki cha taifa au ulimwengu kuadhibiwa na Mungu, jifunze kusema maneno kama hayo mpendwa.

Usiseme tutakufa,au hatariiiii au mbona tunaishaa nk. Sema sitakufa bali ntaishi.

Naamini umenielewa mpendwa.

Mungu akubariki sana. Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.