Salamu – Machi, 2021

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ninakukaribisha tena katika kona hii ya salamu za kila mwezi. Kumbuka tunasalamu zenye kichwa

VIPAO MBELE VYA MAOMBI YAKO WEKA BIDII YA KUOMBEA MASIKIO YAKO.

Hebu tusogee mbele tena….

KUWA NA MASIKIO SI TIKETI KUWA WEWE UNASIKIA

Biblia inatufundishakuwa mwanadamu tena mtumishi wa Mungu akawa na masikio lakini asisikie “Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona.Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA?Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii.”(Isaya 42:18-20)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona mtumishi huyo masikio yake haya ya kawaida hayakuziba. Yalikua wazi yaani si kiziwi..lakini Biblia inasema alikua hasikii..

Angalia na mistari hii mingine “ Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao; Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote.”(Warumi 11:8-10)

Ukiisoma hiyo mistari unajifunza kuwa unaweza pewa masikio lakini ukatengenezewa nguvu ya kutokusikia kabisaa.. Ukilifahamu hili itakua kwako ni rahisi kumsihi huyo Mungu aliyewatengenezea hao watu mfumo wa kutokusikia akuoe wewe uwezo wa kusikia.

FAHAMU WEWE UNA MASIKIO YA AINA MBILI YAANI SIKIO LA NJE NA SIKIO LA NDANI YAANI ROHONI.

Sikia wewe na mimi tumeumbwa na Mungu katika maeneo makuu matatu.. Angalia mistari hii.. “ “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.” (Ayubu32:8)

Ukiisoma hiyo mistari utaona vitu vitatu vilivyotumika kukuumba wewe.. wewe ni roho, uliyepewa mwili hapo umeitwa huo mwili mwanadamu au mavumbi na ukapewa pumzi ya Mungu iitwayo nafsi.

Sasa sikia roho yako inamasikio na mwili wako huo unamsikio… ngoja nikuoe huu mfano utanielewa angalia mistari hii.. “Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;” (Waefeso 1:15-18)

Sikia kama kuna macho ya ndani fahamu pia kuna masikio ya ndani…yanayotakiwa yazibuliwe.

Mungu ni Roho anapozungumza nasi huzungumza na roho..kwa hiyo hiyo roho yako inatakiwa isikie.. shida tuliyonayo ni namna ya kumsikia Mungu akisema nasi..ni rahisi kuwasikia wanadamu kuliko kumsikia Mungu.

Mungu anataka tumsikie kabisaa asemapo nasi..mfano ukisoma Biblia unaona Roho Mtakatifu aliyendani yetu anasema kabisaa na roho yako..shida ni hayo masikio yako hayamsikii..

Angalia mistari hii. “Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,wakaita; wakauliza kwamba Simoni aitwaye Petro anakaa humo. Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta. Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma.” (Mdo 10:17-20)

Ukiipitia mistari hiyo unaona wazi kuwa Roho Mtakatifu anasema na anaweza kukuongoza kwa sauti yake kabisaaa… Mtume Petro sikio lake lilikua zuri, alimsikia Roho Mtakatifu alipomweleza kabisaa.

Na alijua kuwa anayezungumza naye ni Roho Mtakatifu.hakusita kuchukua hatua kabisaa..

Angalia na mistari hii “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,wakapita Misia wakatelemkia Troa.Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.” (Mdo 16:6-10)

Roho Mtakatifu anasema kabisaa na wewe kwa kutumia masikio yako hayo ya ndani..shida yameziba yanahitaji kuzibuliwa

MUNGU ANAO UWEZO WA KUMFUNULIA MTU SIKIO LAKE LA NDANI USINGIZINI.

Biblia inatufundisha kuwaMungu anao uwezo wa kukuzibuaau kukufunulia wewe masikio yako ya ndani hata ukiwa umelala usingizi ukamsikia. Angalia mistari hii uone..

“Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.” (Ayubu 33: 14-18)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona sikio lako linalotakiwa lizibuliwe ni hili la nje na sikio la ndani..Mungu aposema na wewe na hujali yaani humsikii fahamu atayazibua hayo masikio yako ya ndani na macho yako ya ndani ili uone na umsikie asemapo nawewe.

MFANO KUZIBULIWA SIKIO NA KUANZA KUFUNDISHWA NA ROHO MTAKATIFU

Roho mtakatifu leo yupo tayari kumfundisha kila mtu…shida ipo hapa masikio yetu hayajaziburiwa tu. Ukianza kuombea masikio yako yasikie fahamu Mungu atayashughulikia tu.

Angalia mistari hii “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” (Yohana 14:26).

Roho Mtakatifu anao uwezo wa kutufundisha kabisaa. Kama anauwezo wa yeye kutufundisha fahamu anayo sauti yake ambayo masikio yetu yanatakiwa yamsikilize.

Angalia na mistari hii mingine.. “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.” (1Yohana2:27)

Mafuta ni Roho Mtakatifu..anaouwezo wa kukufundisha mambo yooote…

UKIMRUHUSU AZIBUE SIKIO LAKO ATAANZA KUKUFUNDISHA

Biblia inasema hivi. “Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao. Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma.” (Isaya50:4-5).

Ukizibuliwa sikio utaanza kufundishwa na yeye kabisaa kuhusu mambo yako mbalimbali na ndipo mafanikio yako yatakapo kuja..na ndipo utaanza kupokea masomo yakuwafundisha wengine

JIFUNZE KUWEKA DAMU YA BWANA YESU KWENYE SIKIO LAKO

Sikia katika maombi yako hayo jifunze kuweka damu ya Bwana Yesu Kristo katika masikio yako hayo…

Biblia inasema hivi “Kisha akamchinja; na Musa akatwaa katika damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la Haruni, na katika chanda chake cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kuume.Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya kuume, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kuume; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.” (Law 8:23-24)

Jifunze leo hii kuiweka damu ya Bwana Yesu Kristo kwenye masikio yako hayo ili damu hiyo ilinde masikio yako na ikuwezeshe kuyafunua masikio yako hayo ili umsikie Mungu asemapo na wewe…

Anza kufanya maombi ya namna hiyo kwa Mungu ili umsihi akupatie masikio ya kumsikia.

Kwaleo niishie hapo

Hebu tufuatane katika kona hii mwezi ujao naamini utapata kitu cha kujifunza.

Mungu akubariki sana

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
 9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222