Salamu – Mei, 2021

3: MADHARA YA TATU. KUPOKEA KITU BILA KUSIKIA UTAPOKEA SADAKA YA HILA

Unaposoma Biblia unaona umuhimu wa kusikia jinsi ulivyo mkubwa. Moja ya eneo muhimu mno katika kusikia kwetu ni hili la kupokea vitu kutoka kwa watu.

Unajua sisi wanadamu tunapenda mnoo kupokea vitu kutoka kwa watu.. sikiliza si kila kitu tunatakiwa tukipokee. Kuna vitu unaweza kuvipokea kumbe ndani yake kuna hila au kuna madhara..Mungu yeye pekee ndiye ajuaye kitu hicho ukipokeacho kimebeba nini.

Sadaka au zawadi unayoipokea inaweza kubeba baraka kwako au mabaya kwako. Angalia mfano huu uone “Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama BWANA aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwakeBasi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi?Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji. (2Falme 5:20-27).

Sadaka aliyoipokea Gehazi ilikua imebeba ukoma, ukiipitia mistari hiyo unaona Nabii Elisha yeye aliikataa sadaka hiyo, naamini kuwa Mungu alimshitua Elisha asiichukue sadaka hiyo.

Gehazi hakusikia akaichukua sadaka hiyo kilichomkuta ni kuwa na ukoma. Unaweza kupokea zawadi ya nguo na hujui nguo hiyo imebeba upako gani… si unajua Elisha alipoipokea nguo kutoka kwa Eliya akajikuta akikutana na upako aliokuwa nao Eliya?

Fikiria leo hii unapokea nguo kumbe nguo hiyo ina upako mbaya..utajikuta umeharibiwa mfumo mzima wa maisha yako ya kiroho,kiutumishi nk kisa nguo tu uliyopokea.

MFANO WA KUPOKEA KAZI KUMBE MUNGU HAYUMO

Tunahitaji sana kusikia wapendwa..Leo hii unaweza kupokea kazi kumbe ndani ya kazi hiyo Mungu hayumo. Ngoja nikupe mfano huu ulio hai kabisa… ukisoma maandiko unaona mfalme Sauli alipokea kazi ya kuwa mfalme hakujua kuwa kazi hiyo haikutoka kwa Mungu.

Mungu hakupanga kuwapa wana wa Israeli mfalme, Wana wa Israeli wao ndiyo waliojitakia mfalme na Sauli akapata hiyo nafasi au kazi.

Matokeo yake kila mtu anajua kuwa Sauli alijikuta pabaya mnoo… Angalia mfano wa hao wafalme wawili kati ya Daudi na Sauli. Daudi alipewa kazi hiyo na Mungu yaani Mungu ndiye aliyemchagua Daudi na kumpa hiyo kazi..

Neema ya Mungu ilikaa juu ya Daudi. Sauli aliishia kufutwa kazi tu, unapokutana na madhara kazini jifunze kujua chanzo ni nini?

Watu wengi hupata kazi zinazo wakondesha kiroho na kufa kiroho kabisaa.. moja ya sababu ya madhara hayo ni hii ya kupokea kazi bila kumsikia Mungu.

Sikia si kila Cheo unachopewa Mungu yumo ndani yake..unahitaji kusikia mpendwa, kuna vyeo vinakuja kimtego kabisaa..ukikipokea tu, kama haujafa kiroho utakufa kimwili, jiulize swali inakuwaje upokee cheo cha uraisi uishiye kupigwa risasi na kufa? Si mnasikia huko katika mataifa mengine viongozi wakiuwawa madarakani?

Kabla haujakubari kuwa kiongozi ulipochaguliwa iwe kanisani au serekalini nk usikurupke kukubali tu kisa umechaguliwa jifunze kumsikiliza Mungu kwanza. Nakwambia ukweli kuna vyeo ndani yake vimebeba jela na maumivu mengi mnoo…jifunze kusikia kwanza kabla haujakurupuka kukikumbatia cheo chochote

JIFUNZE KUTOKUFANYA MAAMUZI MAGUMU BILA KUSIKIA SAUTI YA MUNGU

Katika maamuzi yako yoote magumu unayotaka kuyachukua..unatakiwa kabla hujafanya hayo maamuzi jiruhusu kumsikia Mungu kwanza. Unaweza kuwa na swali ntamsikiaje sasa? Wewe fuatana nami huko mbele utajifunza tu..nataka nikupe kwanza taadhari ya kuchukua kabla ya kutoa maamuzi. Sikia kutoka kwa Mungu anakushauri nini juu ya hatua unazotaka kuzichukua. Ukijifunza kusikia utafanikiwa mnoo katika kila maamuzi magumu unayotaka kuyachukua.

Sikia unawezakutaka kumfanyia mtu kitu furani hata kama amekosea au la na ukasikia sauti IKIKUKATAZA USIFANYE HIVYO ISIKILIZE SAUTI HIYO HATA KAMA WEWE NI MTU MKUBWA MNOO KICHEO.

Mungu anajua madharaau faida ya maamuzi hayo unayotakiwa uyachukue, usipojifunza kuuliza na kumsikia Mungu nakwambia huwezi kufanikiwa..angalia mistari “Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.”(Yeremia 10:21)

Ukiipitia mistari hiyo utaona wazi kuwa hao ndugu hawakufanikiwa wao na makundi yao kisa hawakumsikia Mungu tu.

Kama wangemwelekeza Mungu shida zao na kutafuta ushauri kwake na wangemsikia katika kile ambacho angewaambia wasingeingia katika hasara wao na makundi yao.

Hebu weka bidii ya kumuomba Mungu akupe sikio la kusikia.

Nimalizia hapo. Tuonane tena kwenye kona hii mwezi ujao.

Barikiwa

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
 9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222