Salamu – Juni, 2021

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.Ninamshukuru Mungu sana kwa kutupa nafasi ya kuuona mwezi huu. Naamini hata wewe Mungu amekupa nafasi ya kuuona mwezi huu wa sita katika mwaka 2021.

Nimekuletea salamu za mwezi huu wa sita kumbuka tunasomo lenye kichwa

VIPAO MBELE VYA MAOMBI YAKO WEKA BIDII YA KUOMBEA MASIKIO YAKO.

Hebu tuendelee mbele kidogo tena kwenye eneo laJIFUNZE KUTOKUFANYA MAAMUZI MAGUMU BILA KUSIKIA SAUTI YA MUNGU.

Kaka zake Yusufu walifanya uamuzi mgumu mnoo wa kumuuza mdogo wao Yusufu kwa wale Waishmaeli. Unajua hao ndugu walipokua wakifanya maamuzi hayohawakusikia sauti iliyokuwa ikiwakataza wasifanye hayo.

Angalia mistari hii “Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia kwa hiyo shida hii imetupata.Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, msimkose kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo damu yake inatakwa tena.Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao.” (Mwanzo 42:21-23)

Maamuzi magumu waliyoyachukua ya kuuza mdogo wao waliyafanya bila kusikia.. wangelisikia wasingelimuuza ndugu yao.

Kuna maamuzi unayoyaamua ambayo mbeleni utayajutia nakwambia ukweli maamuzi hayo kabla hauja yafanya kuna sauti ilikuonya ila shida ni masikio yako kutokusikia ingawa unayo.

Nakumbuka siku moja nilitaka kufanya jambo furani na niliisikia sauti ya Mungu ikinikataza nisifanye.. ilikua hivi, kipindi kile bado sijaoa nilikua naishi na mdogo wangu wa tatu

Mdogo wangu alikua na marafiki zake wawili wa kiume ambao walipata matatizo katika maisha yao ikabidi waje kuishi nyumbani kwangu. Siku moja nilialikwa kufundisha semina mahali, ilikua ni wiki la Krisimasi…nilianza tarehe kumi na tisa nikamaliza tarehe 26 nakumba hivyo… ni habari ya muda mrefu..sana.. siku chache kabla sijaondoka nilipewa taarifa na mtu mmoja kuwa miongoni mwa kijana ninaye ishi naye anatabia si nzuri ni mzinzi

Niliambiwa kuwa anatembea na binti mmoja mtoto wa tajiri mmoja hapo mjini tunapoishi..baada ya huyo mtu kunipa taarifa hiyo nikaamuakukaa na kijana huyo..nilimuuliza ni kweli habari hiyo?

Alinikatalia kata kata kuwa si kweli kabisa. Nilimfundisha kuhusu madhara ya dhambi ya uzinzi na akaniambia ameelewa na hafanyi jambo hilo.

Baada ya siku chache Nikaondoka kwenda kwenye semina, siku nimeludi nilipofika nyumbani kwangu nilikutana na jambo la kuniudhi sana, nilipofika pale nyumbani kwangu niliukuta mlango haujafungwa na kufuli.

Nikaufungua na nikapita sebuleni nikaufungua mlango wa chumbani, ile kufungua nikakutana na kitu kigumu sana, niliona binti amelala usingizi kabisaa kitandani pangu na ni yule binti niliyeambiwa anatembea na kijana ninaye mtunza nyumbani kwangu.

Nikafanya maamuzi ya kumtandika na nimfukuze hapo nyumbani kwangu. Unajua niliisikia sauti ikiniambia hivi IWENI WENYE HURUMA KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA! Nilipoisikia sauti ile nikajizuia, nikaludi sebuleni taratibu, nikatoka nje, nikaamua kuongea na mama mwenye nyumba. Yule mama aliponiona tu alishituka sana sana. Nikamweleza nilichokutana nacho. akaniambia ni kweli, binti huyo amefukuzwa kwao ana mimba ya kijana huyo unaye ishi naye.

Unajua ilinibidi nifanye kazi ya kuwatafutia chumba, na niliwagawia vitu nilivyokua navyo na unajua yule binti alikuja kuokoka na kusimama vizuri tu na siku anaokoka alisema wazi kuwa ameokoka kwasababu ya mema niliyomtendea. Unajua baadaye nilijiuliza sana kuwa kama nisingemsikia Roho Mtakatifuningejikuta nimeharibu kila kitu.

Watu wengi sana wanajikuta wakifanya maamuzi ya kuondoka kwa waume zao kisa hawafikirii maamuzi hayo magumu wanasikia nini…wanajifanyia tu maamuzi bila kusikia…mwisho wa siku wanajikuta kwenye wakati mgumo mnoo.

UKIONA MTU UNAMWAMBIA ILA HAKUSIKILIZI NA UNAHAKIKA UNAMWAMBIA NENO TOKA KWA MUNGU. FAHAMU MBELE YAKE KUNA MADHARA.

Mungu anapokusikizisha neno furani na hujali (HUKO MBELE NTAKUONYESHA NJIA AMBAZO MUNGU ANAZITUMIA KUSEMA NA WATU) Fahamu mbeleni kutakua na madhara tu.

Watu wengi masikio yao hayasikii na wengi hawana muda wa kuyaombea ili wasikie…matokeo yake hukutana na madhara. Sikia, Mungu akitaka kukuokoa atakuletea neno usipolisikiliza utajikuta kwenye maangamizo. Angalia mistari hii uone.

“Kwa hiyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Amazia, akampelekea nabii, aliyemwambia, Mbona umeitafuta miungu ya watu, isiyowaokoa watu wao mkononi mwako?Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.” (2Nya 25:15-16)

Mungu anaweza kukuonya usiende au usiambatane na mtu na usimsikilize…Utakwama… ukiona umekwama na uligundua kuwa Mungu alisema nawewe hukusikia ludi kaanze kufanya maombi ya Toba.

Naamini umenielewa

Nimalizia hapo. Tuonane tena kwenye kona hii mwezi ujao.

Barikiwa

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222