Kila Kitu Kuhusu Wokovu

Kwa Nini Wokovu?

Inakupasa ndugu kuupokea wokovu kwa sababu ndio mapenzi ya Mungu, Watu wengi sana wamezoea kusema hayakuwa mapenzi ya Mungu, au wengine kuomba hivi “Mapenzi ya Mungu yafanyike” tena wengi wameizoelea ile sala kuu kila waendapo kwenye makusanyiko mbalimbali huisema ile sala kuu na katika hiyo sala kuu kuna eneo ambalo wanaomba wakisema “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni” (MT 6:10). Ninaamini hata wewe sala hii unaifahamu na unamuomba Mungu kila mara mapenzi yake yatimizwe hapa duniani au kwako,kwa jamaa zako na ndugu zako, Lkini nikikuuliza swali je! Unayajua mapenzi hayo ya Mungu amabayo unataka yatimizwe hapa duniani! Bahati mbaya watu wengi hawayajui hayo mapenzi ya Mungu.   

Ukisoma maandiko matakatifu utaona kuwa miongoni mwa hayo mapenzi ya Mungu, hili la kila MTU aokolewe au AOKOKE! Ebu sikia maneno haya ya semavyo “Hili ni zuri,nalo la kubarika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja,mwanadamu Kristo Yesu, ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake”. (1Timotheo 2:3-6)  Kama kuna jambo ambalo limepata kibari au limekubarika na Bwana Mungu na  yeye analiona ni zuri, hili la watu waokolewe, na mtu huyo ni wewe!  Kwa nini wewe uokoke? Jibu mojawapo ni hili una kuwa unayatimiza mapenzi ya Mungu. Mungu anataka wewe uokolewe na Mwokozi ni mmoja naye ni Yesu Kristo.  

Usipookoka fahamu una kuwa kinyume na mapenzi ya Mungu, na mtu yeyote yule asiye ya tenda yaliyo mapenzi ya Mungu hata upata uzima wa milele, kwa hiyo na kushauri leo kubali mapenzi ya Mungu ya timizwe kwako, au kwa ndugu na jamaa zako. Watu wengi wanayazuia mapenzi ya Mungu yasifanyike kwao,au kwa watu wengine, lakini kwa bahati mbaya huwa hawajui kuwa wao ndio kizuizi cha mapenzi ya Mungu kutimizwa kwao au kwa watu wengine, unaweza kusema una maana gani?

Sikiliza, unapokataa au unapokataza  watu wengine  wasiupokee wokovu unakuwa unayazuia mapenzi ya Mungu, na jambo hio ni dhambi. Watu wengine huwazui watu wasiokoke, wewe unapolizuia jambo hilo kwa kulikataza, unakuwa kinyume na mapenzi ya Mungu, kumbuka Mungu anasema jambo hilo yeye analikubali,na  ni zuri kwake. “Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe….” (1Timotheo 2:3-6), Kwa ufupi unatakiwa leo ujue kuwa unapaswa kuupokea wokovu kwa sababu ni mapenzi ya Mungu, si mapenzi ya watu fulani au ya dhehebu Fulani,  wokovu ni mapezi ya Mungu kwa kila mtu, Swali langu kwako, je! Umeokoka? Kama bado fahamu unayazuia mapenzi ya Mungu nakushauri yaruhusu leo mapenzi ya Mungu yatimizwe kwako, kwa kuupokea huo wokovu.