Salamu – Julai, 2020

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana, Mimi na familia yangu ni wazima. Tunamshukuru Mungu. Nimekuletea mfululizo wa salamu za mwezi.

Tuna salamu zenye kichwa

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE WOKOVU (ENEO LA KUOKOLEWA KATIKA KIPINDI CHA MAJANGA ULIMWENGUNI)

Katika salamu za mwezi uliopita tuliangalia jambo, la sita nalo lilikua JAMBO LA SITA ACHA KUFANYA MAOVU ILI MUNGU ASIKUPIGE NA TAUNI.

Hebu tuendelee mbele kidogo. Mara nyingi tauni inapotokea wanadamu wanaingia hofu sana. Na hofu kuu ipo kwenye kufa. Wengi huingia kutubu.

Sikia toba lazima iende na geuko. Kama hakuna geuko au watu hawajabadili tabia fahamu ni ngumu Mungu kuponya au kuiondoa hiyo tauni.

MFANO TUNAOMBA TOBA NA NI TOBA YA MUNGU KUTUSAMEHE DHAMBI . NIKUULIZE SWALI , JE! AKITUSAMEHE DHAMBI HARAFU? Utasema aondoe ugonjwa, akiondoa harafu?

Lazima tumhakikishie tuna acha dhambi. Na tumhakikishiye kuwa tunaacha dhambi kiukweli, Mfano wa kumdanganya.

Angalia mfano huu wa hawa ndugu walitubu lakini hawakua wakweli. “Hasira ya Mungu ikapanda juu yao, Akawaua waliokuwa wanono; Akawaangusha chini vijana wa Israeli. Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi, Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu. Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi, Na miaka yao kwa hofu ya kuwasitusha. Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta; Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii. Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, Wakamwambia uongo kwa ndimi zao. Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake, Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote. Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili, Upepo upitao wala haurudi.”(Zaburi 78:31-39).

Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa hao ndugu walitubu ili Mungu asiwaue, lakini hawakutaka kubadilika tabia, hata waliposema wanatubu walikua waongo. Kilichowasaidia ni ile rehema ya Mungu tu.

Mungu anapoleta tauni na hiyo tauni ikaanza kuua watu fahamu ndani yake anataka kuona watu wakilijua kosa lao na waliungame na wageuke kwa kuacha dhambi ambazo ndiyo chanzo cha tauni au nzige hao.

Sikiliza Mungu anapokasirikia wenye dhambi na hao wenye dhambi wakijua kosa lao na kugeuka na kuziacha njia zao mbaya Mungu huwaokoa hao watu na tauni.

Hebu ona mfano huu wa nini ufanye ikitokea tauni, Mungu anasema tutubu na tumludie kwa mioyo yetu yoote.

“Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia; siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi. Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Adeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao. Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopiga mbio. Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu. Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao.Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake; huendelea mbele kila mmoja katika njia yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha, wala hawaachi kuifuata njia yao. Huurukia mji; hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama aingiavyo mwivi. Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;naye BWANA anatoa sauti yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili? Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu? Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao? Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.”(Yoeli 2: 1-18).

Ukiipitia hiyo mistari kumi na nane utaona wazi kuwa Mungu akikasirika anawatuma hao amewaita jeshi lake ili wawaue wanadamu. Hiyo ni tauni na nzige.

Inapokuja hakuna anayeweza kuizuia. Ili izuiliwe mwenye uwezo huo ni Mungu tu, na ameweka utaratibu wawanadamu wafanye nini ili Mungu aizuie hiyo tauni.

Amesema wamludie, tena WAMLUDIE KWA MIOYO YAO YOOTE. Kwa maana nzuri waache dhambi,watubu na walie mbele zake. Ndipo huliondoa hilo jeshi lake lake la ajabu.

Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.