Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Naamini unandelea vema..ni namshukuru sana mwezi uliopita tumekua na semina nyingi mnoo..na Mwezi huu wa tano tumeendelea kuwa na Semina nyingi ..
Tumekua na semina Dodoma Kibaigwa na tukaelekea Katavi huko Mpanda na hivi ninavyokuletea salamu hizi tupo Sumbawanga mjini Tunazifanya semina hizo ndani ya hema yetu inayotembea….usiache kutuombea.
Nimekuletea salamu za mwezi wa tano naomba zipokee! kumbuka tuna salamu zenye kichwa
WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO
Katika salamu za mwezi uliopita tuliendelea kuangalia eneo lile la vitu vinavyoweza kupelekrkea nafsi ya mtu kujeruhiwa.
Tuliangalia eneo lile la Dhambi na tuliitazama dhambi ya uongo na chuki…
Katika Salamu za mwezi huu nataka tuangalie dhambi nyingine inayoweza kutumika kuijeruhi nafsi yako, nayo ni dhambi ya Kuabudu miungu mingine au kuabudu sanamu.
Angalia mistsri hii uone madhara ya dhambi hii katika eneo la kuijeruhi nafsi..
“BWANA akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri Tena BWANA akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.(KUTOKA 32:7-10)
Ukiitizama mistari hiyo unajifunza kuwa kitendo cha mtu kuabudu miungu au sanamu kinapelekea watu hao kujitengenezea uharibifu nafsini au moyoni..
Unapomuacha Mungu na kujitafutia miungu tu…. fahamu nafsi au moyo wa mtu huyo unaharibiwa…
Ngoja nikufundishe kitu… unajua unapo itolea hiyo sanamu sadaka na ukaibeba hiyo miungu fahamu unakua unayatolea sadaka mashetani na pia unapoibeba unakua unayabeba mashetani..
Angalia mfano huu. “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.”(1Kor10:19-21)
Kwamujibu wa mistari hiyo unaona wazi kuwa siku ile wale ndugu walipoitolea ile sanamu sadaka walikua wanatoa sadaka zao kwa mashetani…na pia kwa mujibu wa mistari hiyo unaona walijenga ushirika na hayo mashetani..
Unajua kwa macho ya nyama hao ndugu utaona walikua wanaitolda sanamu ya ndama sadaka zao..kwa macho ya kiroho kulikua na mashetani au mapepo mengi kwelikwe kwenye hiyo sanamu ya ng’ombe.
Sasa angalia kilichotokea..kitengo kile kiliwaunganisha au kuwatengenezea ushirika na mapepo hayo..kwa maana nyingine mioyo yao ilikaliwa na mashetani..
Unaweza kuniuluza ulijuaje? Nilijifunza kwa kuiangaliaile mistari ambayo Mungu anamwambia Musa kuwa kitendo cha watu hao kuabudu mashetani hayo kimewapelekea kuziharibu nafsi zao..
Ukisoma Biblia mashetani ni maharibifu mnoo..na moja ya eneo wanalolilenga kuliharibu ni moyo au nafsi ya mwanadamu.
Ukifuatilia kwa umakini utaona mashetani yana haribu Mfumo mzima wa akili,utashi,na hisia za mwanadamu..
Angalia mfano wa mistarihii uone..”Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”(2Kor4:3-4)
Mungu anaydtajwa hzpo ukimwangalia ameandikwa kwa herufi ndogo mungu.. huyu ni shetani..kazi yake ni kuziteka fikra za watu..kwa lugha nzuri anaiharibu mioyo ya watu..si fikra zinakaa huko moyoni au nafsini?
Sasa sikia wana wa Israeli walipo iabudu miungu tu…ikakimbilia kuziharibu fikra zao..yaani akili, hisia,na utashi wao uliharibika kabisa….
Naamini umenielewa..jilinde mpendwa usiabudu miungu mingine ili uilinde nafsi yako na maangamizi.
Kama unaona ulikosea kwa kuitenda dhambi nakushauri tubu..ondoa kila ulichopewa kama ni hilizi ichome moto..navitu vingine vichome moto..pia usiitolee wala kuisujudia sanamu yoyote..
Omba msamaha na muombe Mungu akusamehe na kuitengeneza nafsi yako iliyoharibika.
Tuonane tena katika salamu za mwezi ujao. BARIKIWA.
Mungu akubariki sana.
Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
- Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-
+255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako
Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.