Salamu – Juni, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Nichukue nafasi hii kukukaribisha katika eneo hili la salamu za Mwezi.. na salamu hizi ni za mwezi huu wa sita..

Naamini umepata neema ya kuiingia mwezi huu wasita..mwezi ulio katikati ya mwaka.

Kwetu Mwezi wa tano uliopita ulikua mzuri sana, kwani tulikuwa na semina nyingi mnoo..Tulianzia Dodoma huko Kibaigwa katika kanisa la Kkkt..Tulipomaliza tukaelekea huko mkoani Katavi na tulikua pale Mpanda mjini

Tulianzia huko na semina za nje yaani hemani.. Tulipomaliza tukaelekea Sumbawanga…na Tukimaliza Sumbawanga tutakwenda.Tunduma Songwe na Vwawa makao makuu ya Songwe..

Baada ya kukupa ushuhuda huo ebu tusogee mbele…na kuzitazama salamu za mwezi huu wa sita..

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Katika salamu zilizopita tuliendelea kuangalia jambo la pili linaloweza kupelekea jeraha moyoni nalo lilikua ni dhambi.

Katika salamu za mwezi huu nataka tusogee mbele kidogo..

3: JAMBO LA TATU NI HILI: KUFIWA NA MTU MUHIMU KWAKO

Moja ya jambo ambalo linaweza kuwa ni chanzo cha kuijeruhi nafsi ya mtu ni hili la kufiwa na mtu maalumu kwako.

Sikia unaweza kusikia mtu furani kafariki, na ukasikitika kwa kiwango cha chini sana.. na hili linasababishwa na umuhimu wa mtu huyo.

Nimesikia kabisa watu wakisherekea msiba wa mtu furani kwa kunywa pombe huko kwenye mabaa na vilabuni.. Unaweza kujiuliza kwanini mtu afurahie kifo cha mwanadamu mwenzie?

Jibu mojawapo katika majibu mengi ni hili la namna mtu huyo aliyefariki alivyokosa kuwa na umuhimu kwa mtu huyo anayefurahia..

Pia unaweza ukasikia mtu furani kafariki na ukasikia kuona watu wengine wakilia kwa uchungu mnoo na wengine uchungu huo na wao ukawauwa kabisaa.

Nimewahi sikia mtu mmoja alifariki kisa alilia sana kwenye msiba wa rafiki yake… Unajua walipishana kama siku tatu hivi..nilihudhuria msiba wa watu hao..walikuwa huko nyumbani kwao yaani kwa wazazi wao wakiishi jirani sana..na walikuwa pamoja.

Yule ndugu inasemekana aliposikia rafikiyake kafariki alienda msibani na alililia sana,uchungu ule wa kifo cha rafiki yake ulikaa moyoni na kweli hata yeye akafariki..

Unaweza kujiuliza maswali kwanini aliye sana hivyo…? Sikia ni ule umuhimu wa mtu huyo aliyefariki.

Watu wengi leo hii wanaishi na majeraha moyoni kisa ni hiki hiki cha kufiwa na mtu wa jirani mnoo na muhimu mnoo..

Hata ukisoma Biblia utanamna jambo hili lilivyo wasababishia watu wengi maumivu moyoni na kuwatengenezea majeraha makubwa.

Angalia mfano huu, mfalme Daudi alipofiwa na mwanawe ampendaye sana Absalomu alipata uchungu mkubwa mnoo

Angalia mistari hii uone.”Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!“(2Samweli 18: 33) 

Ukiisoma mistari hiyo unaona namna jambo hilo la kufiwa lilivyo mtengenezea mfalme Daudi jeraha lililomuumiza mnoo moyoni mwake.

Kumbuka Daudi alikuwa ni mtu hodari mnoo na shujaa. Lakini aliposikia mtoto wake ambaye alitaka kumuua Daudi amekufa, Mfalme Daudi alilia sana. Na alipatwa uchungu mnoo kiasi alifikiri afe yeye kuliko mtoto wake kufa.

Alijikunja na kulia mbele za watu..Biblia inasema watu wengi waliingia na fedheha kisa walimuona mfalme akilia kwa sauti kuu…

Angalia mistari hii, “Kisha Yoabu akaambiwa, Angalia, mfalme anamlilia Absalomu na kumwombolezea. Na kushinda kwao vitani siku ile kukageuzwa kuwa maombolezo kwa watu wote; maana watu walisikia siku ile ya kwamba, Mfalme anahuzunika kwa ajili ya mwanawe.Watu wakajificha siku ile, wakaingia mjini kama vile watu waonao fedheha wajifichavyo, hapo wakimbiapo vitani. Mfalme akajifunika uso; na mfalme akalia kwa sauti kuu, Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu!“(2Samweli 19: 1-4) 

Ukiipitia mistari hiyo unauona moyo wa mfalme Daudiulivyojeruhiwa mnoo na msiba ule.

Ukisoma maandiko unaona mfalme Daudi aliisha fiwa na mtoto aitwaye Amnoni lakini huoni akilia kwa mtindo huo.. Aliishafiwa na mtoto ambsye Biblia inasema alifunga ili mtoto huyo apone lakini Mungu hakumponya mtoto huyo na akafa.

Biblia inasema Daudi aliposikia mto kafa,wala hakulia na kuumia, aliinuka akaoga,akavaa vizuri akala chakula…

Angalia mistari hii.. “Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto; Daudi akafunga, akaingia, akalala usiku kucha chini.Nao wazee wa nyumba yake wakaondoka, wakasimama karibu naye, ili wamwinue katika nchi; lakini hakukubali, wala hakula chakula pamoja nao.Ikawa siku ya saba, yule mtoto akafa. Nao watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia ya kuwa mtoto amekufa, maana, walisema, Angalieni, yule mtoto alipokuwa angali hai, tulisema naye, asitusikilize sauti zetu; basi hatazidi kujisumbua, tukimwambia ya kuwa mtoto amekufa?Lakini alipoona ya kuwa watumishi wake wananong’onezana, Daudi alitambua ya kuwa mtoto amekufa; basi Daudi akawauliza watumishi wake, Je! Mtoto amekufa? Nao wakasema, Amekufa.Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.Watumishi wake wakamwambia, Ni neno gani hili ulilolitenda? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto, alipokuwa hai; lakini mtoto alipokuwa amekufa, uliinuka ukala chakula.Akasema, Mtoto alipokuwa hai, nalifunga, nikalia; kwa maana nalisema, Ni nani ajuaye kwamba BWANA atanihurumia, mtoto apate kuishi?Lakini sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi.Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake, akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye BWANA akampenda;”(2Samweli 2:16-24)

 Ukiitazama mistari hiyo unajifunza kitu cha ajabu mnoo. Daudi yule aliyelia kwa uchungu mnoo mbele za watu ndiye huyu huyu aliyejizuia kulia alipofiwa na mtoto wake huyo ambaye alimfanyia maombi na alimfungia kabisaa ili apone.

Ninachotaka ukione hapo mpendwa ni hiki..mtu anaweza kujeruhiwa mnoo moyoni kwasababu ya kufiwa na mtu muhimu au yule ampendaye sana..

Watu wengi leo hii mioyo yao imejeruhika mnoo kwasababu ya kufiwa na wazazi,au watoto,au marafiki au vionngozi wao wawe wa serekali au kanisani.

Nakumbuka Watanzania wengi mnooo..waliposikia raisi wao kipenzi Magufuli amefariki..wengi waliumizwa mnooo..nimeonana na Watanzania na watu wengine wasio Watanzania walioumizwa mnoo..

Kuna watu hata kuombea nchi waliacha kabisaa..kisa jeraha..wengi niliwasikia wakisema hawamwelewi Mungu na kiukweli wengi walipoteza matumaini kabisaa na kukata tamaa..

Ukiwaita kwenye maombi unawaona walivyojeruhika moyo. Nilijifunza kitu kikubwa mnoo kuwa nafsi au moyo unaweza kujeruhika vibaya mnoo kwa kupitia shida hii ya kufiwa tu.

Watu wengi wamejeruhika kwa kupitia jambo na wanahitaji msaada mkubwa mnoo kutoka kwa Mungu.

Ngoja nikupe mfano..ukikutana na mwanamke aliyefiwa na mume wake akiwa bado mbichi kabisa fahamu umivu lake ni kubwa mnoo..

Biblia inasema hivi “Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.”(Isaya 54:1-4).

Ukiipitia mistari hiyo unaona huyo mwanamke alikua binti aliyeolewa na akafiwa na mumewe na hakupata mtoto kwasababu alikua tasa.

Uchungu wake ulikua mkubwa mnoo…Mungu aliuona uchungu huo ikabidi aingilie kati.

Naamini umejifunza kitu katika salamu hizi.. Ebu niishiye hapo..tuonane katika kona hii mwezi ujao na tutaangalia kwa undani namna ya kufanya ili moja tusiruhusu umivu katika jambo kama hili likitupata, mbili namna ya kufanya ili uponywe nafsi jambo hili ukikutana nalo.

Mungu Akubariki sana.

Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.