Salamu – Octoba, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana..Tunamshukuru Mungu atupae uzima na furaha na amani. Nimekuletea salamu za mwezi wa kumi naomba zipokeee

Kwanza nianze kuwashukuru kwa maombi yenu na sadaka mnazozito kwa ajili ya kazi ya Mungu aliyotupa.

Tumekua na semina nzuri huko Makete Njombe, Tukuyu, na Chunya.. Semina hizo zilikua nzuri sana. Tumemuona Mungu akituhudumia kwa mafundisho na kujenga kanisa lake..

Hebu pokea salamu za mwezi huu..kumbuka tuna salamu zenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Katika salamu za mwezi uliopita tulianza kuangalia madhara ya kuhifadhi uchungu moyoni..tuliangalia madhara yakwanza ni kukuzuia kuusikia…Sikia ni ngumu kumsikia Roho Mtakatifu ukiwa na uchungu moyoni.. Pia ni ngumu kuwasikia watu ukiwa na uchungu moyoni.

Hebu tuangalie madhara ya pili

2: UCHUNGU HUTUMIKA KUKUHARIBU USO WAKO

Watu hasa wanawake wanatafuta kila siku kuhakikisha wanazitengezea ngozi za uso wao ziwe nzuri..

Kwa lugha mzuri niseme mara nyingi unautafutia uso wako uzuri au afya nzuri

Sasa sikia, unapokua na uchungu moyoni, kinachotokea ni kuutengenezea uso wako ugonjwa…yaani unahuribu uso huo kwa kupitia tendo la kununa..

Angalia mistari hii…“ Nikisema, Mimi nitasahau kuugua kwangu, Nitaacha kununa uso nikachangamke moyo;Mimi huziogopa huzuni zangu zote, Najua kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia. (AYUBU 9:27-28)

Kitendo cha kununa au kukunja uso kinapelekea mtu huyo kuuzesha uso wake mapema sana.. misuri ile ya usoni inapokunjwa kwa kutumia kununa fahamu hukomaa na kupelekea ngozi kujikunja na kusinyaa mapema..

Uchungu hutengeneza udhaifu au ugonjwa katika uso wa mtu..Angalia mistarihii utamuona Daudi akilisema jambo hili. “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.”(Zabibu 42:11)

Uchungu uliokuwa ndani ya moyo wa Daudi ulimtengenezea kuipoteza afya ya uso wake..

Daudi aligundua kuwa anashida katika eneo la afya ya uso wake.. Na aligundua kuwa kinachosababisha aikose afya ya sura yake ni uchungu moyoni.

Daudi bahati nzuri aligundua kuwa afya ya uso wake ni Mungu , na aliona kitendo cha yeye tokuzitazama shida zake na akaze kumtumainia Mungu kumtoa katika shida hizo na kwa kutokuhifadhi huzuni hizo basi kitakachotokea ni Mungu kumpatia afya njema usoni pake.

Biblia inasema hivi.. Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.”( Mithali 15:13)

Ukiwa na furaha moyoni uso wako utakua na afya nzuri sana..

Basi mpendwa ondoa uchungu moyoni ili Mungu akupatie afya nzuri usoni pako..Tubu kwa kununa kwako na. Wasamehe waliokupelekea unune…

Mungu akubariki sana sana.

Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.