Salamu – Septemba, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ninakukaribisha sana ndugu yangu katika eneo hili la salamu za mwezi. Tunamshukuru Mungu sana ambaye ametupatia uzima na amani.

Bila kupotea muda nimekuletea somo la salamu za mwezi wa tisa.kumbuka tuna somo lenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Baada ya kujifunza eneo la kujua madhara ya uchungu ndani ya moyo wa mtu, Ebu tusogee mbele kidogo.

MAMBO YA KUFANYA YA KUISHUGHULIKIA NAFSI AU MOYO

Sikia yapo mambo mengi sana ambayo unatakiwa uyafanye ili upate kuiponya nafsi au moyo wako. Yapo mambo mengi sana ebu tuyaangalie haya machache

  1. OMBA MAOMBI

Naamini huwa unaomba, watu wengi sana ni wanaomba lakini wengi hujikuta wakibanwa na uchungu au huzuni mioyo yao na mioyo hiyo ikawa imeharibika sana.

Sasa ukitaka kuona moyo au nafsi yako ikijengwa unatakiwa uombe.na uombe kwa lugha.

Angalia mistari hii inavyotupa akili. “Nena kwa lugha Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho ya Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.(1Kor14:1-4)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona wazi kuwa nafsi ya mtu inaweza kujengwa. Unaposikia neno kuijenga nafsi fahamu inaweza kubomoka au kuharibika. Kinachoweza kuibomo nafsi ni uchungu au huzuni.

Sasa sikia.nafsi au moyo ukiingia na uchungu kinachoweza kuijenga hiyo nafsi ni maombi ambayo mtu anaomba kwa kunena kwa lugha.

Unapokutana na uchungu moyoni na ukawa unaweza kunena kwa lugha ndipo hujikuta ukijengewa wewe mwenyewe nafsi yako.

Fanya hivi. ukiona unamoyo mzito uwe unajua sababu zilizokupelekea upate huo uzito yaani uchungu anza kuomba na omba kwa lugha.

Unajua uchungu ukiingia moyoni usifikiri ni jambo rahisi kuuondoa. kwahiyo ninaposema omba jifunze kutenga muda mrefu katika kuliombea jambo hili…

Ngoja nikupe mfano mwingine. Angalia mistari hii “Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe. Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka. Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.” (MT 26: 36-38).

 

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona wazi kuwa Bwana Yesu Kristo alikutana na jambo kama hili.Alikutana na huzuni moyoni kwake.Unajua alichokifanya ni kuomba. Aliwatafuta hata wenzake ili waombe pamoja naye…

 

Unapoisoma hiyo mistari unaona nafsi ya Bwana Yesu Kristo ilikutana na majeraha.kiasi ambacho akakutana na uchungu .Ili apate uponyaji nafsini mwake alijua hali hiyo ikitokea inachotakiwa huyo mtu ni kuomba.

 

Kwahiyo hata wewe ukikutana wewe au wenzako wakiwa na uchungu moyoni basi wewe waombed ili Mungu aziponye nafsi zao.

Biblia inasema hivi “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.”(Yakobo 5:16)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unajifunza kuwa kinachoweza kumtengenezea mtu dhaifu awe na uponyaji ni maombi.fahamu hata nafsi ya mtu ikiwa imejeruhiwa ili iponywe cha kwanza cha kufanya ni kuomba uponyaji wa hizo nafsi zilizojeruhiwa.

Ukiona nafsi yako ina huzuni unatakiwa uombe. Biblia inasema hivi. “1Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.”(Yakobo 5:13)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona kuwa mtu akikutana na jambo baya yaani jambo la kuhuzunisha unachotakiwa ukifanye ni kuomba.Omba Mungu aiponye nafsi yako, omba kwa bidii ili Mungu aingilie kati na kukutoa katika teso lako hilo la nafsini kwako.

Namini umezipokea salamu za mwezi huu wa nane, na umenielewa,Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona kama hii.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio. mwakatwila. org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila. ()