Salamu – Octoba, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ni neema kubwa tumepewa na Mungu na kutupa nafasi ya kuuona mwezi wa kumi.

Mwezi huu nimekuletea salamu hizi.

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Salamu za mwezi ulipita nilikuonyesha namna ya kulishughulikia nafsi au moyo wako.Tuliona ili tuwena Moyo au nafsi iliyojeruhika iponywe au ilindwe tuliona kuomba.

Hebu tuangalie jambo lingine la kufanya ili nafsi yako ikae sawa.

2: (A) JIFUNZE KULISIKIZA AU KULISOMA NENO LA MUNGU

Angalia mistari hii “Nafsi yangu imeambatana na mavumbi, Unihuishe sawasawa na neno lako.” (Zaburi 119:25)

Kwa mujibu wa mistari hiyo tunajifunza kuwa moja ya jambo linaloweza kuihuisha moyo au nafsi ya mwanadamu ni neno la Mungu.

Neno la Mungu linatufundisha kuwa maneno mema yanwezs kuiinua nafsi ya mtu aliyeumizwa na kuchoka. Biblia inasema hivi “Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.” ( Methali 16:24)

Neno linalopendeza kwa mtu ni neno la Mungu.ndani ya neno la Mungu kuna kutiwa moyo,kupewa maarifa ya nini ufanye na kupewa matumaini mapya. Sasa sikia ili mtu aliyeumizwa moyoni, kinachoweza kumponya na kumuhuisha ni neno la Mungu tu.

Neno la Mungu linaweza kuiponya nafsi ya mtu. “Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.” (Zaburi 107:20).

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona kuwa neno la Mungu linaweza kuiponya nafsi ya mtu iliyojeruhiwa.

Sasa ili uiponye moyo wako jifunze kutafuta neno la Mungu linavyokuelekeza kuhusu uishi unapokutana na maudhi au uchungu.

Angalia mfano huu wa neno la Mungu linavyosema kuhusu uchungu “Muwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;” (Waefeso 4:26 na 31)

Ukiwa na uchungu moyoni jifunze kutafuta mistsri kama hiyo… isome iludie ludie weee!! Kitakachotokea utajikuta unapokutana na uchungu neno hilo linaanza kukulinda ili usiikalishe uchungu huo.

Angalia mstari mwingine “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.”(Wafilipi 4:4).

Kinyume cha furaha ni uchungu au huzuni.sasa ukiiweka hiyo mistari utajikuta kila wakati unapokutana na huzuni ukianza kutafuta kufurahi.

Angalia hkatika maisha yako jifunze kutafuta wewe mwenyewe kusikiliza au kusoma maneno yenye kukuinua moyoni mwako. Tafuta mistari ya namna hiyo Angalia mistari hii isemavyo “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.”(Isaya 41:10-14).

Ndani ya mistari hiyo unayapata maneno yenye kukuinua na kukuponya kabisaa.

Naamini umenielewa anza kuiponya nafsi yako kwa mfumo huo. Mungu akubariki sana

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio. mwakatwila. org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.