Salamu – Novemba, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. mimi na familia yangu tunamshukuru sana Mungu ambaye ametupa uzima na kutulinda katika mwezi uliopita.

Katika mwezi wa kumi tumekuwa na semina nzuri Chunya,Itigi na Manyoni.Semina hizi zilikua nzuri sana.Tulikutana na changamoto kubwa ya lori letu ambalo tunalitumia kubebea hema kuharibika njiani tukielekea Itigi.

Ilitulazimu kukondi hema huko Itigi ili tupate kimvuli hapo kiwanjani.Tunamshukuru Mungu alitusaidia sana.

Mwezi huu wa kumi na moja nimekuletea salamu hizi.

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO.

Katika kipindi cha mwezi ulipita nilikuonyesha namna ya kulishughulikia nafsi au moyo wako. Katika kipindi kilichopita tulijifunza jambo la pili lenye kipengele hiki jifunze kulisikiliza au kulisoma neno la Mungu.

Hebu tuendelee mbele kidogo.

3: JIFUNZE KUISEMESHA NAFSI ILIYOHARIBIKA

Nafsi iliyojeruhika inaweza kuponywa kwa Kusema kwako au kusemeshwa na mtu

Angalia mfano huu…. “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu. Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.” ((ZABURI 42:5-6).

Kwa mujibu wa mistari hii utajifunza kuwa nafsi iliyoumizwa inaweza kuponywa kwa kutumia maneno ya kujitia moyo na huyohuyo aliyeumizwa moyoni.

Ukisoma Biblia utaona Mungu ametupa maarifa kuwa kile kinachosemwa cha mtu ndicho kitakachoumbwa.

Angalia mistari hii “Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.”(Isaya 57:19).

Mungu anatabia ya kuumba kile kilichosemwa, sasa sikia, ili Mungu akuumbie wewe furaha myoni mwako jifunze kusema maneno ya kujitia moyo wewe mwenyewe.

Mfalme Daudi alipokutana na shida moyoni mwake aliamua kujisemexha yeye mwenyewe.Alisema peke yake kuhusu mambo anayoyatarajia mbeleni.

Angalia mfano huu “Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.”(Mithali 16:23-24).

Kwa mujibu wa misyari hiyo unajifunza kuwa kuna maneno ambsyo wewe mwenyewe uyatamke ili uwe na tabia furani.

Ukikutana na wanajeshi au wacheza ngumi au mieleka, wanatabia ya kujisemesha wao wenyewe ili wavuke kwenye mitihani yao…ili wajitie moyo huwa wanajisemesha wenyewe utashangaa hao ndugu hupata nguvu moyoni na kuvuka mahali walipokutana na shida

Hata kwako jifunze kujisemesha maneno ya kujiponyesha wewe mwenyewe, ndipo utaanza kupata uzima huko moyoni ulikokua umejikatia tamaa na kuwa na uchungu.

Biblia inatupa ufahamu unasema hivi. “Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.” (Yoeli 3:10).

Kwa mujibu wa mistari hiyo utajifunza kuhusu habari ya mtu kujisemesha maneno ya kujitia moyo wewe mwenyewe.

Sehemu nyingine Bwana Yesu Kristo anatufundisha hivi. “33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” (Yohana 16:33)

Tunajitia moyo kwa kutumia njia nyingi tu.moja yakufanya ili uwe na moyo wa kuponywa ni hii ya kujisemesha maneno ya kujitia moyo.Ukianza kuwa na tabia ya namna hiyo utashangaa umeanza kuwa na amani moyoni.

Hebu anza kuyafanyia kazi haya, ndipo utaanza kuponywa nafsini au moyoni mwako.

Naamini umenielewa sana

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
 • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
 • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
 • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila. ()