Salamu – Disemba, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. mimi na familia yangu tunamshukuru sana Mungu ambaye ametupa uzima na kutulinda katika mwezi uliopita.

Katika mwezi wa kumi na  moja tumekua na semina nzuri  huko Katesh na Mvumi..Tunamshukuru Mungu alitusaidia sana.

Mwezi huu wa kumi na mbili nimekuletea salamu hizi.. Kumbuka tunasomo  lenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO.

Katika kipindi cha mwezi ulipita nilikuonyesha namna ya kulishughulikia  nafsi au moyo wako. Katika kipindi kilichopita tulijifunza jambo la tatu lenye kipengele hiki jifunze kuisemesha nafsi yako.

Hebu katika salamu za mwezi huu tuendelee mbele kidogo ili tujue namna ya kufanya ili tuiponye nafsi yetu

Tuendelee tujifunze eneo la kuisemesha nafsi yako

Watu wengi kwasababuya kutokulijua jambo hili wanapokutana na maumivu moyoni huanza kusema maneno ambayo yanawa tengenezea mabaya mioyoni mwao.

Angalia mistsri hii “Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.”( Mithali  21:23)

Maneno ya kinywa chako wewe mwenyewe yaweza kukutengenezea mabaya nafsini mwako.

Kumbuka nafsi ni moyo..sasa sikia jifunze kutokusema maneo ambayo yatakufunga wewe mwenyewe nafsini mwako.

Watu wengi leo hii wanataka sanaa kuzilinda nafsi zao lakini hawajui kuwa chanzo cha kuwatengenezea mabaya nafsini mwao ni katika habari za kusema kwao wenyewe.

Angalia mistari hii uone.” Kisha Musa akanena na wale vichwa vya kabila za wana wa Israeli, na kuwaambia, Neno hili ndilo aliloliagiza BWANA.Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.”(Hesabu 30:1-2).

Ukiisoma mistari hii utajifunza kuwa maneno ambayo mtu anaya sema yanaweza kuifunga au kuifungua nafsi ya mtu..

Ngoja nikupe mfano..unaweza ukakutana na magumu mengi sana na magumu hayo yakakutengenezea uchungu..sasa sikia ukikutana na hayo magumu ukianza kutamka maneno magumu magumu hayo yakufunga

Mfano ulikua na mchumba akakukataa ukapata huzuni au dhida ukajisemesha wewe mwenyewe kuwa sitaki tena kuoa au kuolewa.

Kitakacho tokea ni hiki hauta olewa au kuoa..Unanisikia?

Badilika kusema kwako..usiseme maneno ambayo yatakufungia mabaya moyoni.. Anza kunena au kuisemesha nafsi yako maneno yatakayoifanya nafsi yako iponywe.

Fanya hivi.tubu kwa ajili ya maneno uliyoyatamka wewe mwenyewe..na uanze kuisemesha nafsi yako  maneno mema

Hebu anza kuyafanyia kazi haya, ndipo utaanza kuponywa nafsini au moyoni mwako.

Naamini umenielewa.Mungu akubariki sana

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
 • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
 • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
 • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila. ()