Salamu – Januari, 2024

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. mimi na familia yangu tunamshukuru sana Mungu.

Katika mwezi wa kumi na mbili tumekua na semina ya vijana na semina ya wanaume na kambi letu la maombi ambalo tunalifanya kila mwishoni mwa mwaka. Tulikua na kambi zuri sana..

Nikukaribishe mpendwa mwaka huu 2024 mwezi wa kumi na mbili tarehe 28-31/12/2024 usikose karibu pale St Mary’s Kadege jijini Mbeya

Mwaka huu tutakua na semina vijana na wanaume na wanawake na pia tutakua na semina nyingi sehemu mbalimbali nchini..Semina za Hema na zingine ndani kwenye makanisa mbalimbali.
Tuombeeni ukitaka ratiba za semina 2024 ingia kwenye tovuti yetu www.mwakatwila.org utaiona.

Mwezi huu wa mwaka nimekuletea salamu hizi.. Kumbuka tunasomo lenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO.

Katika kipindi cha mwezi ulipita nilikuonyesha namna ya kulishughulikia nafsi au moyo wako. Katika kipindi kilichopita tulijifunza jambo la tatu lenye kipengele jifunze kuisemesha nafsi yako.

Hebu katika salamu za mwezi huu tuendelee mbele kidogo tuangalie jambo la nne

4: JAMBO LA NNE ILI USIUGUE MOYONI JIFUNZE KUMTUMAINI MUNGU

Sikiliza ili moyo wako au nafsi yako isiugue unatakiwa ujifunze kumtumaini Mungu ndipo utahuishwa nguvu zako na ndipo hautaugua moyoni mwako

“Angalia mistari hii Ulikuwa umechoka kwa ajili ya urefu wa njia yako; lakini hukusema, Hapana matumaini; ulipata kuhuishwa nguvu zako; kwa sababu hiyo hukuugua. (Isaya 57:10).

Kwa mujibu wa mistari hiyo utaona huyu mtu alikutana na taabu moyoni, na taabu hiyo ilikua inampeleka kuugua. Kilichomponya au kumlinda ni hili aliweka matumaini kwa Mungu kuwa atamtoa katika taabu yake

Unaweza ukawa na swali nini maana ya neno tumaini? Tumaini maana yake ni kutegemea,kusubiri,kutarajia au kutazamia.

Sasa sikia. unapokosa tumaini kwa Mungu kukufariji,kukutoa kwenye teso utajikuta teso lako likakutengenezea kufishwa au kupigwa moyoni…

Unapokutana na umivu moyoni, jifunze kumtazama Mungu tu kuwa stakutoa au kukufariji au kukusaidia katika teso lako.. Ukianza kumtarajia au kumtegemea ndipo Mungu huanza kukusaidia katika teso lako

Watu wengi wanapokutana na mateso hawamtazami Bwana Yesu Kristo ili kuwasaidia katika teso lao.

Wengi hujenga matumaini kwa watu au akili au fesha su elimu nk. Kinachokwenda kutokea ni hao watu kujikuta kwenye mateso zaidi..

Wengine wanaugua moyoni ni kwasababu wanapokutana na umivu moyoni wanakata tamaa.. yaani huwa hawana na nani wa kumsaidia hawamuoni wanajikuta wakikosa msaada kwasababu hawaoni au hapa wa kuwasaidia katika teso lao.

Sikia unapokutana na teso ni rahisi sanaaa usione wa kukusaidia.. Angalia mfano huu.. “Basi, tumaini langu li wapi? Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?”(Ayubu 17:15).

Kwa mujibu wa mistari hiyo utaona huyu ndugu alikutana na shida.. aliuliza swali tumaini lake li wapi? Na ni nani atakayeliona?

Watu wengi nafsi zao zinaugua kisa ni hiki cha kutokumuona Mungu kuwasaidia katika taabu zao.

Jifunze kumtumaini au kumtazamia Bwana Yesu Ndiye mwenye kuwatoa kwenye shida zao..

Ukimtumainia atakusaidia na kukufariji, ukianza kuwatumaini watu, au ndugu nk nakwambia ukweli utakutana na kuugua tu., Biblia inasema hivi “Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.”(Waebrania 2:17-18).

Kuhani mkuu anayetajwa hapo ni Bwana Yesu Kristo. Huyu ndiye tunapaswa kumtumaini au kumtazama au kumtarajia au kumtegemea kutusaidia katika siku za mateso yetu.

Anayeweza kukusaidia katika teso ni yule aliyekutana na mateso na akayashinda yale mateso.. Huyu ni Bwana Yesu Kristo, Peke yake ndiye mwenye uwezo wa kukusaidia kwenye mateso yake.

Jifunze kumtumaini wa kukutoa na kukusaidia na kukufariji na kukutia nguvu katika siku zako za mateso…Ebu mtumaini Bwana Yesu Kristo katika shida yenu, ndipo utajikuta ukihuishwa na kuondolewa kuugua kwako huko nafsini

Naamini umenielewa Anza kwa toba, Tubu mahali ulipomkosea Mungu kwa kutokumtumaini, tubu ulipomtumainia mtu,ndugu,akili,fedha au elimu. Anza kumtumaini Mungu kukusaidia katika teso lako

Mungu akubariki sana

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila. ()