Salamu – Februali, 2024

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. mimi na familia yangu tunamshukuru sana Mungu.
Siku zinakimbia huu ni mwezi wa pili.. Naamini umeanza kuuzoeza na kuona ni nini cha kufanya kwa mwaka huu.

Mwezi uliopita tumekua na semina nzuri sana hapo Iyunga kwenye kanisa la Moravian tulikua na semina nzuri sana.

Nimekuletea salamu za mwezi huu wa pili kumbuka tunasomo lenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO.

Hebu tusogee mbele kidogo, Katika kipindi kilichopita tulijifunza jambo la nne ambalo ni ili usiugue moyoni jifunze kumtumaini Mungu.

Hebu tuangalie jambo la tano

5: JIFUNZE KUTOKUISHI KWA KUTUMIA HISIA ZA UONGO

Sikia Mungu ametuumba katika maeneo makuu matatu. Ametupa mwili(mavumbi).,ametupe roho(mtu),ametupa nafsi au moyo au pumzi hai Angalia mistari hii “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.”(Ayubu 32:8)

Kwa mujibu wa mistari hiyo utajifunza kuwa tumeumbwa kwenye maeneo hayo matstu..utaona kuna mwili yaani mavumbi au mwanadamu,humo ndani ya mwanadamu kuna kitu kaumbiwa ni nafsi au pumzi za mwenyezi Mungu na pia huko ndani mwanadamu tumepewa roho

Sasa sikia humo ndani ya nafsi au moyo au pumzi hai ya Mungu kuna vitu vifuatavyo, kuna Akili, Hisia (mihemko) na Utashi yaani nguvu ya kukuwezesha kufanya maamuzi

Hisia au mihemko inabeba Upendo,chuki,furaha, uchungu, huzuni, tamaa, wivu, husuda, kushangaa,kuumia,kuumwa, kuguswa, hasira,ukali,ghadhabu kunusa,uwepo….nk.

Sikia ukiona huko moyoni mwako unamchukia mtu..fahamu jambo hilo limo moyoni mwako ni rahisi kabisa hata mtu mwingine asijue kabisaa kuwa wewe umechukia au umemchukia mtu..yaani haumpendi….

Ili watu wa nje ili wajue kuwa kwa kweli umechukia na haumpendi huyo mtu..mambo yafutayo yatatokea..moja ni kauli ya huyo mwenye hisia zilizobeba chuki.
Pili, ni hatua ya kupiga au kugombana au kushambulia…tatu ni hali ya kuutambulisha mwili kama kununa au kuchafua sura..

Angalia mistari hii “Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.”(Mithali 29:22). Kama hisia zako zimebeba hasira lazima utakua na ghadhabu,ukali na ugomvi, kila siku ukiongea na watu kidogo tu…Lazima utashusha ugomvi,uwe wa maneno au kupigana ngumi nk

YALINDE MASIKIO YAKO NA MACHO YAKO ILI KUILINDA HISIA YAKO

Mungu akikuonyesha ono ushughulikie masikio yako au macho yako anania ya wewe uanze kuilinda sana moyo wako kwasababu maneno unayoyasikia kiroho au kimwili au macho yako ya kiroho au kimwili kwasababu masikio au macho yako yanaweza kuzalisha hicho kilichomo moyoni mwako utakacho kihisi.

Sikia katika ulimwengu wa roho shetani kila mara huleta sauti zilizo kinyume na sauti ya roho mtakatifu.. Sikia nikwambie.. Roho Mtakatifu hawezi kukuletea wewe sauti zandani za kukutengenezea matokeo ya uchungu na hasira na ghdhabu

Ngoja nijaribu, ninaposema sauti za ndani mimi naita eneo la uwanja wa fikra wazungu wanaita feelings… unaweza kukaa kimya harafu unaanza kusikia huko moyoni kama kuna mtu anakuambia maneno mbalimbali…

Sasa ili wewe uanze kuilinda hiyo nafsi yako isipokee ghadhabu na uchungu na ugomvi jifunze kutokuliruhusu hilo neno ulilolisikia huko ndani na ukaliruhusu likae ndani ya hisia zako na likakubarika na akili yako na utashi ukafanya maamuzi

Nilipokua najifunza somo hili nilishangaa sana niligundua sauti ya ndani ambayo watu wengi wanafikiri ni Roho Mtakatifu anawaambia kumbe ni shetani ambaye usiku na mchana anaziharibu hisia zao na wao wakaona ni sawa tu..

Sikia Biblia inasema hivi.. “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.(Yohana 16:13-15).

Sasa sikia huyo Roho Mtakatifu ambaye asubuhi na jioni kesho na kesho kutwa atakupasha habari yaani huko moyoni mwako…fahamu anayosauti..

Sasa sikia Mungu anasema hivi “lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.”( Mathayo 5:44-45).

Neno hili kila siku Roho Mtatifu huwa anasema na wewe ili hisia zako zipokee hiyo sauti ili akili yako na utashi wako utembee na wewe..

Ngoja nikuambie ukweli kila siku unachokisikia ni hiki…huyu hakupendi,huyu ameniudhi,huyu anakuchukia,huyu mchawi,huyu ndiye chanzo cha matatizo nk…

Sikia ukiona hisia zako zimebanwa hivyo fahamu hisia hizo zimebebwa na ugonjwa… Acha kuishi kwa mfumo wa kimaisha wa namna hiyo..

Sikia hisia za watu wengi hazikai kwenye ukweli..zimebeba uongo…
Cha kufanya tubu..anza kutoishi kwa hisia za uchungu..zikatae hisia hizo..jenga furaha moyoni na amani..

Mjue sana Mungu utajikuta kila wakati una amani.. “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.”( Ayubu 22:21).

Ukiona unasikia kelele za uchungu nenda kwenye neno la Mungu linasemaje..utashangaa utasikia neno la Mungu linasema hivi.. “Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.”( Mithali 3:29)..

Jifunze kusamehe na kutokukaa na uchungu moyoni yaani humo kwenye hisia.

Hisia zako mbaya zigeuze kwa neno la Mungu au nikwambie ikija hisia mbaya igeuze kwa jambo jema..mfano hisia zikikukusukuma kumchukia mtu wewe chukua hisia za wapendeni adui zako…

Ukiishi hivi utashangaa kila wakati hisia za furaha na amani zikikukutawala
Naamini umenielewa..fanyia kazi jambo hili

Mungu akubariki sana, tuonane katika kona hii ya salamu za mwezi ujao

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
 • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
 • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
 • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila. ()