Salamu – Disemba, 2024

BwanaYesu Kristo asifiwe. Karibu sana katika eneo hili la salamu za mwezi. Ni mwezi wa kumi na mbili. Tunamshukuru sana Mungu ametupa mwezi huu wa kumi na mbili ukiwa ndio mwezi wa mwisho wa mwaka huu wa 2024

Kwa hiyo tuta kua na salamu za mwisho wa mwaka. Ni neema tu kuuona mwezihuu.

Kabla hatujaenda mbele na tangazo hili. Kumbuka tarehe 28-31/12/2025 Tutakua na kambi ya maombi. Tutafanyia jijini Mbeya kwenye shule ya St Marys Kadege. Tunaanza saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni Karibuni sana.

Hebu tuanze kuzipokea salamu za mwezi huu wa kumi na mbili

Mwezi huu nimekuletea salamu zenye kichwa

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA

MAONO WAZI WAZI

Sikia tunapo jifunza kuhusu habari za maono na ndoto fahamu. Mungu anaweza kumletea mtu amtakaye unabii kwa kutumia maono ya waziwazi, yaani si kwa kutumia usingizi, yaani mtu akiwa amela usiku au mchana.

Ukisoma Biblia utaona kuna watu Mungu anazungumza nao kwa maono waziwazi. Angalia mifano hii michache “BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?” (Hesabu 12:5-8)

Kwa mujibu wa mistari hiyo utajifunza kuwa Mungu anaweza kumletea mtu unabii kwa kutumia ono lililo waziwazi, bila kulala usingizi..

Angalia mfano huu uone. “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.”( Yoshua 5:13-15)

Yoshua aliona ono hilo waziwazi.. alikutana na amiri wa jeshi la Bwana na walizungumza waziwazi bila kulala usingizi…Akapewa maagizo ya kufanya na alifanya hivyo.

Angalia mfano huu. ”Ikawa katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa, karibu na mto Kebari, mbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu.Siku ya tano ya mwezi, nao ulikuwa ni mwaka wa tano wa kuhamishwa kwake mfalme Yehoyakini,neno la BWANA lilimjia Ezekieli, kuhani, mwana wa Buzi, kwa dhahiri, katika nchi ya Wakaldayo, karibu na mto Kebari; na mkono wa BWANA ulikuwa hapo juu yake.Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu.Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne.Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana.Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi;mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele.Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia.Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao.” (Eze 1:1-11)

Kwa mujibu wa mistari hii utaona kuwa Ezekieli aliona ono dhahiri yaani waziwazi.. Aliliona hilo ono kwupe kabisa. Hakua amelala usingizi, alikua ameketi na watu wengi tu..yeye aliliona ono hilo, hao wengine hawakuona.

Angalia mfano mwingine “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;

nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.” (Kutoka 3:1-8)

Ukisoma mistari hiyo utaona kuwa Musa aliona ono la wazi wazi kabisa, na ndani ya ono hilo kulikua na maelekezo ambayo Musa aliyasikia na kuyatii..fahamu maelekezo hayo ndiyo tunaita unabii, kwasababu neno hilo lilikuwa limetoka moja kwa moja kutoka kwa Mungu….

Mungu alisema waziwazi. Ninachotaka ukione ni hili Mungu alisema kwa kutumia ono la waziwazi si lile la kulala usingizini

Sikia hata kwenye agano jipya Mungu alimtuma malaika kwa Kornelio ili amletee maelekezo yaani unabii kwa kutumia ono lililo waziwazi.

Biblia inasema hivi . “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.” (Mdo 10:1-6)

Kornelio aliliona ono hilo waziwazi, alimwona malaika waziwazi

hakuwa amelala usingizi, ni aliona kwa macho haya haya wazi wazi..

Alipewa unabii na aliutii na akafanikiwa sana. Kumbuka Kornelio hakua nabii ila alikuwa amepewa karama ya unabii.

Sikia hata kwako Mungu anaweza kukufunulia hayo macho yako na ukaona maono ya waziwazi kabisa.Na Mungu akatumia ono hilo ili akupe maelekezo yanayo kuhusu wewe binafsi au watu wengine au kwa ajili ya taifa au kwa ajili ya mambo mbalimbali.

Kwahiyo jifufunze mara kwa mara kuomba Mungu akupe karama za rohoni.

Na amini umenielewa, tuonane katika eneo katika salamu zijazo.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.