Bwana Yesu Kristo asifiwe, mwezi huu ni mwezi wa pili wa mwaka huu. Tunamshukuru sana Mungu ametupa mwezi huu wa pili.
Tunamshukuru sana kwa mwezi wa mwanzo wa mwaka, mwezi uliopita tumekua ratiba ya mapumziko kwetu. Na kujipanga kwa ajili ya kazi za mwaka. Tunamshukuru Mungu aliyetupa mapumziko na upangaji wa kazi kwa mwaka huu.
Kumbuka tunaendelea na salamu zenye kichwa
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA
Hebu tuendelee mbele kidogo.
2: ILI UJIFUNZE KUPOKEA VEMA UNABII KUTOKA KWA MUNGU JIFUNZE KUWA NA UPENDO
Jambo lingine muhimu ambalo litakufanya ili upewe karama ya unabii unatakiwa uhakikishe unakua ni mtu mwenye upendo. Biblia inasema hivi “Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora. (1Kor 12:31)
Biblia inasema tumepewa kibari cha kutaka karama zilizo kuu, moja wapo ni karama ya unabii.. Ukiisoma mistari hiyo tumefundishwa kuwa ili tupewe hizo karama zilizo kuu kuna jambo la muhimu ambalo unatakiwa uwe nalo au ulifanye.
Angalia na mistari hii mingine. “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.” (1Kor 13:1-3).
Ili upewe karama ya unabii unatakiwa uhakikishe unakua ni mtu mwenye upendo, yaani wapende watu au umpende Mungu. Sikia neno upendo maana yake ni kinyume cha chuki. Ukiwa unamchukia mtu yoyote fahamu wewe huna upendo na huyo mtu.
Sikia, unaweza ukamchukia Mungu,ukakosa amani naye.. ukiona hivyo fahamu haumpendi. Kwa mujibu wa mistari hii utaona hapo tunaonyeshwa sifa ya upendi angali hapo.
- Upendo haujivuni na kujiona bora. Leo hii angalia ukiwa moyoni mwako unajivuna na kujiona wewe ni bora kuliko mwenzio fahamu wewe huna upendo ni ngumu kupewa karama ya unabii. Angalia tulivyo mtu wa kanisa furani anajiona yeye ni bora kuliko wa kanisa furani. KWA TABIA HII NDIYO MAANA KARAMA HAZIPO NDANI YA KANISA.
- Upendo haushindani..Angalia wewe umepona kwenye eneo la shindana?. Ukiona moyoni mwako unafanya mambo kwa kushindana usitegenee Mungu atakupa karama zilizo kuu.
- UPENDO UNASAMEHE…Angalia moyoni mwako hauna ucgungu dhidi ya mtu furani? Usipojifunza kuwa mtu wa kuwahukumu watu au kuwalaumu weee fahamu wewehauna upendo.
Ukiona huna amani moyoni dhidi ya mtu furani fahamu wewe hauja msamehe na haumpendi. Ukiwa wewe hauna upendo fahamu ni ngumu kupewa karama zilizo kuu.
Naamini umenielewa
Mungu akipenda Tuonane tena mwezi ujao katika kona hii ya salamu za mwezi.
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.