Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.Namshukuru Mungu sana aliyetupa uzima na afya kiroho na kimwili.
Kabla hatujaendelea mbele nichukue nafasi hii kuwashukuru sana kwa ajili ya semina ya Mbalari Chimala..tulikua na semina nzuri sana.
Nimekuletea salamu ya mwezi wa nane.kumbuka tunasomo lenye kichwa
WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO
MTU MWENYE MAJERAHA AU UCHUNGU HAWI KUWA WAZI KWA KITU CHOCHOTE. HUKAA KIMYA
Angalia mistari hii uone.. “Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni- (Ayubu 31:34)
Ukiisoma mistari hiyo unajifunza kuwa mtu aliyeumizwa moyoni mara nyingi hukaa kimya..Au ni mtu asiyewazi kulisema neno lolote.
Watu wa namna hii hupenda kunyamaza kimya kwasababu wana hofu ya kutokuumizwa tena… Watu wa namna hii hata kama wanatakiwa waseme neno lolote liwe la kujitetea,kushauri kuonya kufundisha nk hawawezi kulisema.
Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona mtu mwenye uchungu kwasababu ya kudharauliwa, kushushwa,kusemewa,maneno magumu au kutendewa jambo furani mtu huyo hawezi kuzungumza na watu wengine.
Mtu wa namna hii hukaa kimya na hujificha au mahali pasipo na watu wawaone. Mtu wa namna hii hawezi kuwa wazi,huficha mambo yake ili tu asionekane.
Uchungu huleta hofu..na kumtengenezea mtu kuwa wa kujificha, hata akiwa na nafasi ya kuwa mkuu wa makusanyo hawezi kuipokea hiyo nafasi atakimbia na kujificha.
Hili jambo lina madhara sana, kwasababu mtu asiyewazi hawezi kukuletea faida yoyote.. hujitengenezea faida yake tu..yaani kwakuwa anauchungu na kaamua kuwa kimya mtu wa namna hii hawezi kuwashauri wengine, wala kuwafundisha au kuwapa siri iliyofichika moyoni mwake..
Ukiona wewe ni mtu mwenye tabia ya namna hii ya kujificha kutokuwa wazi fahamu kuna jeraha lipo moyoni mwako na limekutengenezea tabia ya namna hii..
Nirahisi kufikiri kuwa ndipo uliumbwa uwe hivyo mtu kimya..fahamu Mungu hakukuumba hivyo.
Anza kutubu,kwasababu kitendo cha uchungu kukutengenezea tabia hiyo fahamu ni kwasababu umekaa katika uchungu huo muda mrefu.. hiyo kosa. Biblia inatufundisha tusikae na uchungu mpaka jua kuchwa. Ukikalia uchungu huo kwa muda mrefu fahamu utajikuta unatabia mbaya ya namna hiyo.
Jambo la pili samehe. Uchungu huo unakutengenezea hukumu,ukisamehe unaachilia uchungu.. kwa hiyo samehe mapema ili usijitengenezee tabia ya namna hiyo.
Tatu. Omba. Muombe Mungu akuondolee uchungu uliokutengenezea tabia hiyo ya kukaa kimya na kujificha..Mwambie Bwana Yesu Kristo akutengenezee moyo uliowazi na usiokuficha bila sababu za muhimu.
Nne anza kusema acha tabia ya kukufanya ukae kimya wakati unatakiwa useme kwa faida kwa ajili yako na watu wengine na Mungu.
Namini umezipokea salamu za mwezi huu wa nane, na umenielewa,Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona kama hii….
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
- App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
- Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
- YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
- Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
- Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
- DVDs au CDs
- VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
- Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
- Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
- Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
- Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio. mwakatwila. org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222
Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila. ()