Salamu – Juni, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe mpendwa. Namshukuru Mungu sana aliyetupa uzima na afya kiroho na kimwili. Tunamshukuru Mungu mwezi huuwa sita tumekuwa na semina nne kubwa, tumefanya semina kigoma, Katavi hapo Mpanda, Sumbawanga na Tunduma.

Semina hizo zilikuwa vema sana. Tumemuona Zmungu katika semina hizo. Mwezi huu tuna semina moja Mbarali huko Chimala mkoa wa Mbeya. Tuombee!

Kumbuka mwezi ujao wa nane tutakuwa na semina Ya watumishi. ukiwa mchungaji, mwinjilisti, mwalimu, nabii, mtume, mwimbaji, mwombaji nk karibu sana. Tutaifanya semina hiyo Jijini mbeya pale Maghorofani ile njia iendayo hospitali ya mkoa wa Mbeya. Tarehe 17-19/8/2023 Kila siku saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.

Hebu tuanze kupokea salamu za mwezi wa saba. Kumbuka tuna somo lenye kichwa WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Hebu tuyaangalie madhara ya kumi

10: MTU ALIYEJERUHIKA NAFSI HUTAFUTA KUMPENDEZESHA KILA MTU

Mtu aliyena uchungu moyoni hujikuta hupenda kujipendekeza kwa kila mtu ili upewe nafasi ya kufarajiwa. Unajua nirahisi sana ukiwa na uchungu kujikuta unawatafuta hata watu ambao kwa kweli hawavai hata wawe watu wa karibu nawewe. kisa ili tu upewe moyo wa kukupoza. Angalia mistari hii inasema hivi “Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.” (1The 2:5)

Kwa mujibu wa mistari hiyo utajifunza kuwa mtu mwenye uchungu hupenda kujipendeza kwa watu ili tu wakusaidie na kukufariji, au kumpata mtu mwingine wa kumwisha mzingo wa uchungu wako.

Mtu wa uchungu hupenda kuwapelekea watu maneno maneno. ili tu wajipendekeze, usishangae hao watu hawamkubari huyo mtu, laki huyu mwenyeuchungu wa mamneno maneno mengi atamtafuta tu ili awe jirani naye.

Jifunze mpendwa kutokuwa na tabia ya kujipendekeza pendekeza, ukiona umeumizwa moyoni achana na tabia ya kutafuta kujipendekeza kwa watu na kuwapelekea maneno mengii. Mtu aliyena tabia ya uchungu wengi huwana tabia ya kumsimulia kila mtu ili tu upate faraja kutoka kwa huyo mtu ili tu upate kuushusha mzigo wako.

Hebu badilika tubu. acha tabia ya kujipendekeza pendekeza kwa watu. ondoa uchungu moyoni utajikuta umeiacha tabia ya namna hii. Namini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio. mwakatwila. org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.