Salamu – Mei, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe mpendwa. Namshukuru Mungu sana aliyetupa uzima na afya kiroho na kimwili. Mwezi wa Tano tumeanza semina huko Kigoma. Tumeanza semina vema usiache kutuombea.

Kutoka nyumbani kwetu Mbeya mpaka huko Kigoma ni safari ndefu sana. Tunamshukuru Mungu tumefika salama na tumeanza semina.

Hebu tuanze kupokea salamu za mwezi wa sita. Kumbuka tuna somo lenye kichwa: WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Hebu tuyaangalie madhara ya tisa

9: HUPENDA KUFANYA VITA BILA SABABU

Mtu mwenye uchungu moyoni hupenda vita bila sababu. Mtu mwenye uchungu hujikuta kuingia vita hata ambayo haimuhusu na hana hata faida ya vita hiyo. Angalia mfano. “Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne.” (1Samweli 22:1-2)

Ukiisoma mistari hiyo unaona watu waliokuwa na uchungu moyoni walijikuta kuingia katika jeshi la Daudi. Hebu jiulize kwanini watu hawa walijiunga katika jeshi hili? Hawa watu walikuwa na uchungu moyoni mwao, waliumizwa na watu wengine na tendo hilo liliwatengenezea hao watu kujiunga jeshini na kwenda vitani.

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona mtu akiwa na uchungu moyoni hujikuta kupenda vita. Watu wenye uchungu moyoni hupenda sana vita. Wewe fuatilia mtu ambaye hupenda kugombana wenzake, utagundua anauchungu moyoni uliomtengenezea tabia ya kupenda ugomvi. Hata watu wengi ambao hupenda michezo ya kugombana, utawaona wengi kwasababu ya kuumizwa moyoni hupenda kuanza kujifunza kupenda mchezo wa ngumi ili wakajilinde na kuwapiga hao wanao waumiza moyoni.

Mimi binafsi nilianza kujifunza kucheza karate kwasababu hivi hivi, unakutana na mtu anakupiga bila sababu, unaanza kutafuta uwapate waalimu wa kukufundisha kupigana ngumi. Ili ulipe kisasi au umkute mtu mwingine mjinga mjingaasiweza kupigana umpige weee ili ufurahi tu.

Wewe fikiria hao jamaa walikuwa na madeni, walipodaiwa wakakasirika na kwenda vitani ili tu siku wakiludi kutoka msituni wawapige hao waliokuwa wanadaiwa. Hebu jichunguze ukoje? Kwanini unajikuta tuu unavita na watu wengi tu. unagombana na watu kwa maneno nk. Angalia j

Je? Huna uchungu uliokukalia huko moyoni?

Ukiona una uchungu madhara yake yatakusababisha uwe mpenda vita. Na utashangaa karibu kila mtu uliyenaye jirani hata aliyembali nawe ukigombana naye tu. Nakushauri tubu. acha kitendo cha kukaa uchungu huko moyoni, wasamehe waliokukosea ndipo utakua huru.

Namini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii. .

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio. mwakatwila. org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.